Rais Magufuli amedhihirisha kuwa ni kinara wa kutetea Haki za Binadamu kwa vitendo kwa jinsi anavyoshughulikia janga la COVID-19

Hajapanic, vipi bado upo?
 
Baada ya vifo mfululizo vya viongozi wa nyadhifa za juu, inabidi nikupongeze kwa kuliona hilo!
 
Mmeumbuka sasa

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Wewe upo Tanzania? Upo kwenye lockdown? Unadhani kati ya wewe na hao unaofurahia vifo vyao ni nani yuko kwenye risk kubwa ya kupata maambukizi?

Kuwa mwenye afya na nguvu za kutype hapa sio uwezo wako ni uwezo wa yule aliyeruhusu wengine watangulie mbele ya haki, ambae akiamua hata wewe uende sasa utaenda tuu

Chukua tahadhari na umuombe Mungu wacha kujimwambafy kwa uhai usiojua mwisho wake ni lini.
 
mama D, mzima? Hali imekuwa sio hali!
Mimi mzima kwa majaaliwa ya muumba
Tuendelee kuchukua tahadhari na kumwomba Mungu sana
Tuwaombee familia za wote waliofikwa na majanga pia🙏
 
Nadhani wewe hufuatilii Mambo ya nchi hii.
Toka mwanzo wa hili janga watu wa kada mbalimbali walitoa mawazo tofauti tofauti jinsi tunavyoweza kujikinga na Corona.

Lakini mamlaka zikapuuza kwa majigambo makubwa, kejeri na matusi.
Janga likaingia kwa Mara ya Kwanza, katka kuhangaika kujiponya wengine walishauri tuweke lockdown( hii ingetuua Zaidi) lakini hawakupaswa kutukanwa,lakini walipokea mitusi na kejeri nzito

Vijana wa ccm, kina polepole na makonda walikuja na maneno machafu utadhani wenzao siyo watanzani.

Ndg bulembo kwa kulamba viatu vya mwenye nchi nae akaja na yake. Nk, nk

Walamba viatu kina Paskali mayalla, bia yetu, yehoyada magonjwa mtambuka na wengine, wakaja humu na sifa tele za jinsi mkuu anavyopambana na covid, WAKAMWITA SHUJA MZALENDO, NA ATAIBUKA MSHINDI DHIDI YA COVID

Mara ndege ikatumwa madagaska kuchukua miti shamba, ikawa mshikemshike wa kujimwambafy kana kwamba kuwakomoa walioshauri njia mbadala ndiyo walioleta covid.
Kina kabudi na wengine walikunywa mitishamba huku wametoa mimacho kujimwambafy mbele ya camera za wanahabari

Tumeona wabunge wamejifunika mashuka kupiga nyungu huku wameita waandishi wa habari kama hawana akili.

Kama una akili timamu utaona palitengenezeka makundi yenye kuhasimiana. (Uadui)
Wenyekushauri walionekana kushindwa,.

Tusikumbushe mengi, muda hautoshi.
WASWAHILI WANASEMA ADUI YAKO MWOMBEE NJAA. hujawahi sikia hivyo?

Samson wa biblia alipotobolewa macho na wafiliti, alimwambia Mungu kuwa amlipizie kisasi kwaajili ya macho yake, na afe pamoja na adui zake. Ikawa hivyo.
Jiulize kwanini waarabu hujivika mabomu?
Ukipata jibu nirudie

Sasa wewe unakuja kulaumu watu hapa, unapochangia humu uwe na uhakika na mjadala ulikotoka vinginevyo utaonekana utopolo tu

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Kule nyuma vipi mnatusikiaaa ...[emoji378][emoji378][emoji378] au tuongeze sauti haya sikiki vizuri

Chamwino mnasikia huko au bado tutupie lingine [emoji378][emoji378][emoji378]

Jamani sinauliza huko mnasikiaaa ... !!!

Hayupo!!!!??? Kwani kaenda wapi??? Mh! au karudi CHATO ???

Maaana msibani pia hayupo ... Pemba sijamuona wala Dom hajaonekana [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Hivi aanaomlaumu rais wanamlaumu kwa lipi?

Watanzania ukiwatia moyo ni tatizo! Pia ukiwavunja moyo ni tatizo, 😕
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…