Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Sio yeye, kwenye hili la uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM iko nchi nzima, hivyo wagombea wake wamejaziwa na fomu zao zikahakikiwa. Hata hivyo tulituma ombi hili kwa rais Magufuli na likakubaliwaKama kweli tumemkubali watanzania wote, ni kwanini basi anaogopa uchaguzi ulio huru na wa haki, ili wananchi ndiyo wachague viongozi wao wanaowataka katika uchaguzi ulio huru na haki??
Utasemaje kuwa watanzania ndiyo tulioamua kurudi kwenye mfumo wa chama kulimoja, wakati figisu figisu zikionekana dhahiri kwa wagimbea wa upinzani zaidi ya asilimia 95, fomu zao zikikataliwa kuwa eti zimejazwa vibaya, wakati wenzao wa CCM wakiwa wamejaza kwa usahihi wa asilimia 100??
Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi
Wanabodi, Tangu kuanza kwa pilika pilika za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sijawahi kuzungumza lolote kuhusu uchaguzi huu kutokana na kuwa bize na shughuli za kitaifa, kwanza ni Wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika kitaifa mjini Bariadi Mkoani Simiyu na kufuatiwa na Wiki ya Azaki...