Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amepania kurejesha kwa nguvu mfumo wa chama kimoja nchini

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amepania kurejesha kwa nguvu mfumo wa chama kimoja nchini

Mystery,

Dunia nzima inashuhudia ukiukwaji mkubwa wa katiba ya CHADEMA unaofanywa na Ayatola Mbowe, asiyetaka kabisa kuachia uenyekiti wa CHADEMA. Niongeze volume or?
 
Dunia nzima inashuhudia ukiukwaji mkubwa wa katiba ya CHADEMA unaofanywa na Ayatola Mbowe, asiyetaka kabisa kuachia uenyekiti wa CHADEMA. Niongeze volume or?
Wewe upo nchi gani??

Kwani hujasikia kuwa Chadema wanafanya uchaguzi ulio huru na wa haki hapo Desemba 18 mwaka huu??
 
Pania lakini kwa hoja na kuridhika kwa wananchi kutokana na mafanikio yako na sikulazimisha kwa mtutu WA bunduki hapo haikubaliki na utaondoka na vyama utaviawacha hapahapa ukapita wewe.
 
Mbona nasikia ni nchi ya vyama vingi lakn inaendeshwa kwa mfumo wa chama kimoja???
 
Pania lakini kwa hoja na kuridhika kwa wananchi kutokana na mafanikio yako na sikulazimisha kwa mtutu WA bunduki hapo haikubaliki na utaondoka na vyama utaviawacha hapahapa ukapita wewe.
Ndicho nilichokisema

Ikiwa wananchi watapiga kura katika uchaguzi ulio huru na haki na kusimamiwa na Tume huru ya uchaguzi, wananchi hao wakisema tunataka mfumo wa chama kimoja, tutaafiki

Lakini si katika hila hizi za kipuuzi kabisa, ambapo majina ya viongozi wa upinzani yanakatwa kwa maonevu makubwa

Wakati huo huo majina ya wanaccm yanaonekana kama ya "malaika" ambapo hakuna hata mgombea mmoja, anayekosea kujaza hizo fomu, kwa hiyo wagombea wake wanapitishwa bila kupingwa!
 
Anajaribu tu lakini hawezi kurudisha mfumo huo kamwe!!
Anachoweza ni kuzuia shughuli za vyama hivyo kwa mabavu..kuwapa kesi kesi na kuwatisha vongozi wao, kuwarubuni baadhi kwa pesa nk
Ni kweli vitadhoofu kwa kuminywa huko lakini akithubutu tu kuwapa room ya kufanya siasa kwa haki sawa basi CCM inaondoka madarakani the next day na ....yeye na CCM wanalijua fika.

Sasa matokeo yake wananchi wataacha kupira kura kama ilivyokuwa miaka ya nyuma...yaani ukajisumbue kupanga mistari wakati wao wameshakuchagukia mtu wanayemtaka wao..hivi utakuwa sawa kichwani kweli.
 
FUSO,
Wewe unadhani, nini kitaendelea baada ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa??

Jibu langu ni kuwa anataka ashinde kwa asilimia 100, ili aihadae dunia kuwa hapa nchini hakuna upinzani dhabiti, bali kuna wapinzani dhaifu sana!

Ili atimize ajenda yake ya siri, ya kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja na kumfanya yeye kuwa Life President wetu
 
Kalamu1,
Umenikumbusha enzi za mwalimu alivyowaweka ndani wenzake waliopigana naye kutafuta uhuru kama Bibi Titi Mohamed, Kambona na wengine wengi ambao walikuwa karibu naye. Watu kama akina Sykes huwa hatuwasikii kwenye historia ya chama. Tukae tusubiri cha Pombe atakavyoanza fukuza fukuza ndani ya chama chake akishanogewa.
Eeenh, napinga mlinganisho huo.
Yule ,Mama' wa 'Nobel' mbona siku hizi hasikiki, au kwa vile mlimpa ulaji kajisahau?
 
Kalamu1,
Mkuu watu wazima wazipopiga Kura,watoto wa shule ya msingi watalazimishwa kupiga kura na matokeo yatatangazwa ,mshindi atapishwa na maisha kuendelea,
"Kunyima ushirikiano" ni zaidi ya kupiga kura. Watu wakiamua kufanya hivyo hali itabadilika haraka sana.
Inawezekana hata hao watoto wazazi wakawakataza kwenda shule. Watawaweka wazazi wote mahabusu?
 
Mystery,
Historia haionyeshi keshawahishindanishwa amekuwa akipita bila kupingwa ajazoea hawezi upinzani
 
FUSO,
Wewe unadhani, nini kitaendelea baada ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa??

Jibu langu ni kuwa anataka ashinde kwa asilimia 100, ili aihadae dunia kuwa hapa nchini hakuna upinzani dhabiti, bali kuna wapinzani dhaifu sana!

Ili atimize ajenda yake ya siri, ya kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja na kumfanya yeye kuwa Life President wetu
Kaka dunia kwa sasa ni ya utandawazi tena mkubwa mno; hakuna nchi duniani iliyo na interest na siasa za nchi yetu eti haijui nini kinachoendelea, tangu ununuzi wa madiwani, kuwadhoofisha viongozi wa upinzani, kuwapa kesi kibao ili badala ya kutumia muda kujenga vyama vyao basi watumie muda huo kushinda mahakamani. . Kuwatisha tisha nk

Kifupi atakwama, hatuwezi kurudi tukotoka.
 
IMG_20191120_191001.jpg
 
Binafsi naamini Rais Magufuli hatafanikiwa kuviua vyama vya upinzani. Sidhani kama Watanzania wenye akili zao timamu ambao wamehangaika kwa zaidi ya miaka 30 wakivijenga vyama vyao kwa jasho na damu, watakaa tu pembeni wakishuhudia mtu mmoja akiviharibu vyama hivo kwa raha yake tu ya kutawala bila bugudha!!! Siamini hata kidogo. Naamini watachukua hatua. Ni hatua ipi, mimi sijui!!!
 
Upinzani unatakiwa kuwa na nguvu ya kuihoji serikali kuanzia matumizi ya pesa mpaka nidhamu ya viongozi hata kwa maisha yao binafsi.

Sasa wabunge wa upinzani wanapounga mkono juhudi baada ya kutembelewa na katibu muenezi inamaliza nguvu ya upinzani.
Hayo ni mawazo yako au ndio katiba inavyosema?
 
Back
Top Bottom