Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
- Thread starter
- #101
Maelezo marefu sana, lakini ulichoongea ni pumba tupu...........Kwanza nakupa hongera kwa kupenda kuchukuwa mawazo ya upande mmoja nakuyafanya ndio sahihi bila ya kuyabalance.Pili ningependa kukuweka sawa hakuna Rais ameeonekana au kusikika akiwapa maelekezo watendaji wake kuhusiana na uchaguzi, ninavyojua ni pale Rais anapokuwa ziarani na kutaka kujua kero za wananchi halafu mhusika hayupo hapo utakuta lipo chini ya vyama pinzani sasa huoni hizo ni dharau Rais atawezaje kuwasaidia wananchi wakati wawakilishi wao hawapo na ndio maana anakuwa anatoa kauli za kuwataka wananchi kuchagua viongozi wanaofaa sasa hapo ni kosa. Kuhusu fomu kumbuka vyama pinzani vilishasusia kabla hata ujazaji fomu kuanza huoni kuwa walikuwa na lengo la kususa kabla ya kujaza fomu?hapo walishaona mambo mazuri yanayofanyika wakaona watumie mbinu hizo ili ionekane wanaonewa kwa kuwaweka wagombea wasiowapa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu na pia kila chama kina mwanasheria wake na ilikuwa unavyojaza fomu unatakiwa ugongewe mhuri na katubu wake hilo nalo utalizungumziaje. Wagombea wa ccm waliweza kujaza fomu vizuri ni kutoka na kupewa maelekezo mazuri na wanasheria wao. Pia kumbuka vyombo vya ulinzi na usala vipo kwa ajili ya usalama wa wananchi wake na sio ccm pekee, hao wengine wanavunja sheria na ndio maana unaona kama wanaonewa. Hivyo nakushauri uwe unajitahidi kutafuta taarifa vizuri na kuzilinganisha la sivyo baadae utakuja kujilaumu na muda utakuwa umeshapita.
Hivi wewe ni kipofu hata ushindwe kubaini aliyetoa maagizo ya kipuuzi ya kuvuruga uchaguzi wa Serikali ya mitaa ni Jiwe mwenyewe??