Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

DT125

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
437
Reaction score
637
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masele atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
 
Wachagua wapuuzi tu eti kwakuwa atawabana!!! Daaaaaa

Wananchi sijui wamemwonaje huyu baba!!!

Ameamua kusema atampa ukuu wa mkoa ama ubalozi...mkoa upi uko wazi? Na wananchi je wao ubalozi au ukuu wa mkoa wa Masele utawasiaidia nini??

Huyu baba aache bangi
Anajua anaowahutubia upeo wao wa kufikri anatoshana nao hivyo hawawezi kuhoji.
 
Hapo ndo mjue Rais Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
 
Hapo ndo mjue Raisi Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.
Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
Mbona kawasahau waunga juhudi kuwapigania Kama alivofanya chaguzi za marudio
 
Back
Top Bottom