Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

DT125

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
437
Reaction score
637
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masele atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
 
Anajua anaowahutubia upeo wao wa kufikri anatoshana nao hivyo hawawezi kuhoji.
 
Kwa hiyo anataka sisi mjini tuchague polygon? Haiwezekani hata mara moja! Katambi hashindi labda akapige mswaki kwanza ili meno yawe meupe?
Makalai imekula kwake Kama lijuakali
 
Hapo ndo mjue Rais Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
 
Hapo ndo mjue Raisi Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.
Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
Mbona kawasahau waunga juhudi kuwapigania Kama alivofanya chaguzi za marudio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…