Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masale atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.

Hebu weka picha zao nilinganishe na nione maana siwajui hata walivyo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]Nazidi kukicheka Chama cha wazazi wangu,nakilicho npa Elimu kwenye zle shule zao zajumuiya yawazazi.nahc uyu mgombea wachama cha wazazi wangu amepoteza dira,,,,, Unawezaje kutuambia sisi wanachi kuwa tukuchagulie mbunge ata asie faa ili wewe ukambane uko?umesahau kuwa wewe niRais nautakua bze nashughul nyng ndio maana katba ikaelekeza kuwe nawawaklsh wawanachi kutoka majimbon,Nivp utudanganye utampangia kazi nyingne mkuu wa mkoa au balozi Kwan sisi wakat tunamtuma kuchukua fom ya ubunge hatukujua kua kunakaz zngne atafanya huo ubalozi utakao mpa utatusaidia nn sisi wanachi waShinyanga mjn.usituabishe kabsa sisi tulmtaka katka kazi ya ubunge ndio maana Babu zetu ambao niwajumbe wakamkata....ata sisi hatumtaki uyu katambi na tulianza kumkataa toka akiwa Chadema au mkuu umesahau kama niwewe ndio ulio tuamnsha 2015 katambi hafai kututumikia?Leo umekula nn muheshimiwa.....kwakua utakua nakaz nyingi zakununua ndege nakujenga madaraja nahc tunahc utasahau kumbana,,acha tu tumkate tuwape wapinzani ambao itakua rahc kuwakumbuka maana nivgum kumkubuka rafki unaeish nae kulko adui unae msikia......tena kwachuki za kuhadsiwa
Kwa uandishi huu kweli umesoma shule za jumuiya ya wazazi. Ulifika darasa la ngapi?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa uandishi huu kweli umesoma shule za jumuiya ya wazazi. Ulifika darasa la ngapi?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
😂😂😂Unashangaa au unaulza?hii ndio Elimu niliopewa nachama chako mzgo....we Unashangaa mm kuwa nauandshi wako ila unasahau kumshangaa kiongozi wako ambae anaelimu yajuu kabsa lakn anashndwa simamia maneno yake.sio bure brother inatakiwa ukapmwe ubongo...kama ulsha pmwa ubongo bac we utakua milembe day😃😃😃na unaendelea nadozi.maana we Unashangaa mm wakat ata mm najishangaa kwaelimu wanayojsfu wameboresha wakat imeshndwa kutusaidia.
 
Kwa uandishi huu kweli umesoma shule za jumuiya ya wazazi. Ulifika darasa la ngapi?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Wakati mwngne huwe unafikilia chakucoment kabla,nakama upo kazini we ni hewa apa Chama chetu kinakupa Elfu15 yabure tu.apa hakuna shindano la insha,,,ungekua ukunielewa usingechosha dole gumba lako kwenye coment yangu....ila kwakua umeelewa naunataka tutambue upo kazn ndio maana umeleta kihelehele.....ata mm nlkua boya kama wewe tangu mwaka2010.Sasaiv naangalia Sera ata rungwe Nampa staki kutumika kawewe
 
Hapo ndo mjue Raisi Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
Dah! Astakafirulahi... Huu ujiniaz ni wa kiwango cha bwawa la Nyerere
 
Wanaosema Magufuli hana nia njema na Tanzania sijui kwa nini watu wanashindwa kuwaelewa.
Eti haya ni maneno ya mgombea urais na ambaye amekuwa rais kwa miaka 5 iliyopita.
Magufuli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji. MTU asiyetaka watu wenye weledi waingie bungeni ni MTU wa aina gani kama sio kichekesho?
Na jee wanao mpa kura MTU wa aina hiyo tunapaswa kuwaitaje? Mimi jibu ninalo lakini ngoja nili hifadhi kwa sasa kwani NITAFUNGIWA na kuikosa JF week hii wakati naihitaji
Ndiyo maana anawakata watu kama Masele anawaacha akina Msukuma, Kibajaji na Mlinga!!
 
Hapo ndo mjue Raisi Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
Mkuu hiyo nchi ya SADC ipo bara gani hapa duniani?
 
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masale atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
Kwamba kazi ya Magufuli ni kugawa vyeo,no wonder uchumi wetu umeanguka
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapo mwisho ulivyomalizia, imebidi nicheke tu
Shinyanga Masele hajawahi kushinda alipogombea na Shelembi alishindwa na alipogombea na katambi alishindwa zote wameiba na hata Salome atamshinda huyu mtu wa Geita katambi ccm sijui yapoje wizi tu

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masale atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
Mzee Baba ameshapaniki. Hizi ahadi za vyeo ktk kipindi hiki muhimu cha kampeni za uchaguzi wa nafasi ya uraisi ni sawa kabisa na matendo najisi ya rushwa. Unataka kumuhonga Lissu kwa uteuzi sasa unaendeleza hata kwa huyu Masele!
 
Back
Top Bottom