Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

Nani atakakiwa kumsimamia mwingine?

Rais kumsimamia Mbunge au Mbunge kumsimamia Raisi?

Mambo yanakorogeka.
 
Katambi hakubaliki hapa Shinyanga, sijui hizo kura tutaibaje ,tupigwa gap la kura laki moja kwa elfu kumi.
 
Wajumbe tunaendelea kuwakataa wote Waliopita kimazaBe
Nalog off
 
Tatizo la meko anaona wananchi kama simbilisi tuu.
 
Hapo ndo mjue Rais Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
Daaah huo ndio ujiniasi!!!
 
Unamjua Katambi wewe ? Na unamjua hutu Masele ?unaropoka na hujui kitu. Wewebsubiri hiyo tarehe 28/10 Katambi anashinda kwa kishindo !
Huo ukuu wa mkoa kwanini asipewe Katambi? Magufuli sometimes anachemka mnoo
 
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masele atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
Kwa nini huo ukuu wa mkoa au Ubalozi asimpe Katambi??

Chaguo la wananchi sio katambi.

Rushwa ya madaraka imeshamiri sana awamu hii na kuliingizia hasara kubwa Taifa kwenye chaguzi zisizofuata sheria .

Tuwakatae wote wanaolifanya Taifa letu kuwa Mali binafsi.
 
Unamjua Katambi wewe ? Na unamjua hutu Masele ?unaropoka na hujui kitu. Wewebsubiri hiyo tarehe 28/10 Katambi anashinda kwa kishindo !
Sawa Shekhe Yahya. Tarehe 28 October sio mbali.
 
Magufuli hatoshinda uchaguzi huu , huo ukuu wa mkoa atakaompa Masele atautoa wapi ?
Duh...!. Hivi kuna watu wanaamini kabisa kuwa Magufuli hatashinda uchaguzi huu?!.
Yaani ushindanishe matokeo chanya ya maendeleo ya kuonekanika vs ahadi hewa, na bado ahadi hewa zikashinda!.

Oktoba 28 ni mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa?, Je, Watanzania watachagua nini kati ya visible tangible Deliverables vs The Empty Promises?.

Haya lets assume ni kweli CCM iko hoi sana, swali ni nani sasa wa kumkabidhi nchi?,
Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...

Haya na tusubiri
P.
 
Hapo ndo mjue Rais Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
Jamaa wewe unayumba sana ,sasa huo ndoo ugenious ? hilo lina ubunifu gani au uvumbuzi gani au ugunduzi gani mpaka useme ni genius?
 
Shinyanga na wana shinyanga hawana mambo ambayo wangependa yatatuliwe badala ya kunadi sura za watu?
 
Hata kama kwenye maisha kuna bahati mbaya, huwa najiuliza ilikuwaje huyu jamaa akawa rais?
Siyo wewe pekeyako unayejiuliza hivyo. Hakuna asiyejua madudu ya huyu mgombea hata kabla ya kupata u Nyerere. Meli ya samaki wa mchina, Mv Dar, Kugawa nyumba za serikali kwa hawara zake, Usimamizi wa barabara zilizo chini ya viwango. Kweli wa Tz aliyeturoga kafa.
 
Sura yenyewe ya katambi ndio iyo
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masele atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
IMG_20200723_165300.jpeg
 
"Wachague wabunge na madiwani wa ccm ili niweze kuwabana vizuri."
Hapo nimepaelewa sana wananchi jiongezeni
 
Back
Top Bottom