Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amnadi Patrobas Katambi, aahidi kumpa kazi nyingine Stephen Masele

Wehu mtupu.....huyu mgombea ana nuka rushwa....siku ya ngapi tangu kampeni zianze anaahidi kugawa vyeo?
ni muda muafaka kwa Jiwe kwenda kumuuguza msukule wake huko chato
 
HII TABIA YA KUTEMBEA NA RUSHWA YA HONGO YA VYEO NI UDHALILISHAJI ......MAANA KILA MAHALI NI KUAHIDI U RC ,DC , NA UBALOZI ....KATIBA MPYA IKIJA IONDOE HIVI VYEO .....KILA MKOA UWE NA MEYA au GAVANA atakayekuwa responsible na maendeleo ya mkoa , ili kuleta umoja wa kitaifa na kuondoa ubaguzi ....RAS ambaye atakuwa chief of staff wa ofisi ya GAVANA wa mkoa yeye ataendelea kuteuliwa na RAIS ili kuwe na utii na coordination ,ajira ziendelee kuwa central coordinated .....yeye kazi ya GAVANA iwe tu kusukuma maendeleo
Ni vizuri Magufuli akafikiri kwanza, U-RC, U-DC au Ubalozi anaoahidi una ushawishi gani kwa wajumbe na wananchi mgombea wao aliyekatwa licha ya kuogoza kura za maoni?
 
Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masele atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Sasa huu ukuu wa mikoa atawaahidi wangapi ambao wamewanyimwa uteuzi ili hali waliongoza kwenye kura za maoni? Sawa atamteua Masele kuwa Mkuu wa mkoa wa CHATTO anaotaka kuuanzisha, na hao wengine wakina Chenge atawapa mikoa gani?
 
Mkienda kugombea mnaenda kusaka vyeo?
Hapo ndo mjue Rais Magufuli ni genius, unaweza ukazani kamsahau mtu ama kamuonea kumbe anampango naye mwingine mkubwa, mfano ni huyo Steven Masele.

Ambaye anaweza kuwa balozi kuwakilisha nchi kwenye taifa jingine, ama SADC, AU, na UN.
 
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masele atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
Mkuu hakuna mahali JEMBE ametamka rasmi aina ya wadhifa atakaompangia Maselle zaidi ya kusema ameonana nae na kuahidi kumpangia majukumu mengine.
Tusimamie ukweli,hii habari yako inaonekana chadomo bado mna kidomodomo na #katambi
 
Rushwa kakatwa chenge itakuwa na Masele ? Kwa Hiyo apewe mtoa rushwa?
Mwenyekiti kasema atampangia kazi nyingine,kumbe hakuna vita dhidi ya Rushwa?Kama Maselle kakatwa kugombea ubunge kwa sababu za rushwa,vipi tena anateulika?Magumashi ya CCM ni mengi kiasi kwamba hata wanasahau kufuta nyayo za waliyoyatenda kwa hila.
 
DC wa makao makuu ya nchi na Katibu Mkuu wa BAVICHA. Atakuwa mtoto wa SANGOMA
MAGUFULI KUNA WATU ANATAKA KULAZIMISHA WAPITE IWE JUA AU MVUA....MFANO KUNAMBI KULE MLIMBA WANATUMIA NGUVU SANA ....HAPO UBUNGO NA MAENEO MENGINE AMBAKO KUNA WATU WAKE ......HII SIO SAWA KABISA ...NI LAANA
 
Akihutubia wakazi wa Tinde huko Shinyanga, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa. Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana.

Zaidi amedai kuwa aliyeongoza kura za maoni Ndugu Steven Masele atampangia kazi ya ukuu wa Mkoa au ubalozi. Picha inayoonekana tayari kuna ugumu katika jimbo hilo kwa kutokukubalika kwa mgombea aliyepitishwa kinyume na pendekezo la kura ya maoni.

Ameendelea kudai kuwa wasiangalie sura nzuri hali iliyoonesha kuwa kwa mtazamo wake Masele anasura nzuri ukimlinganisha na Katambi.
"mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM amesisitiza wananchi kutomchagulia wagombea wa Vyama vya Upinzani hata kama wanafaa".

Halafu bado mnatuimbisha kwamba maendeleo hayana vyama? Yaani tuchague tu mtu hata kama hana sifa lakini bora tu awe ni wa ccm?

"Amedai kuwa wamchagulie madiwani na wabunge wa CCM kwa sababu ataweza kuwabana".

Kumbe tunayo yaona yote tulikuwa tunashangaa kwani kama nchi tumefikia hapa, kumbe kuna walio banwa ili wapitishe tu hata sheria mbovu mbovu, washangirie tu kila vitendo hata vile vilivyo vuruga umoja wa kitaifa.
 
Kwa hiyo rais anajua kuwa wa kwakr hafai???Katambi si analipwa kwa sababu amekuwa fundi wa kutakana Mbowe na Chadema!!! Scheme on him uwongo utamwua!
 
Back
Top Bottom