Rais Magufuli amnyooshea kidole Mwele Malecela asema alitumiwa na mabeberu kutangaza ugonjwa 'hewa' wa Zika

Hata dengue pia ilikimbia???

usipime dengue ilikimbiza na iliondoka na roho za watu dar, sema taarifa za uwepo wake ziliminywa ikawa mara kipindupindu mara malaria.

Watu wakaambiwa ukijisikia hivyo tumia panadol na maji kwa wingi
 

Watoto wote ni halali.... Unless you are not a parent
 
Mzee ana chuki na kila mtu, kumfuta kazi kwake ndo alitegemea na Mungu afute ridhiki yake ama,yaan utadhani yeye ndo mtoa ridhiki
Bilashaka alitegemea Mwele kwenda kumuomba msamaha nakujipendekeza,kupata kazi kwingine ni dhahiri kakwazika.
 
Mwele alikuwa na mamlaka ya kutangaza hali ya hatari ya ugonjwa kama huo? Au kuna utaratibu ilitakiwa afuate? Shida Tz tunaingiza mambo mengi sana na Siasa na tunaanzia hapo kukwama
 
Kwani magu anaguataga utaratbu atakapoamkia siku hiyo ndio utaratibu utakavyokuwa. Tatizo lipo kwa kiongozi wa muhilimili uliojichimbia chini,nchi inazama kama MV bk vibaraka wake wanashangilia na kupongeza ujinga
Kwa nini Mwele hakufuata utaratibu wa kawaida wa kumuarifu Waziri wa afya kabla hajatoa lile tamko!?
 
Kwani hyo magu huwa anafuata utaratbu, anapoamkia siku hiyo ndio utaratibu utakavyokuwa. Tatizo lipo kwa kiongozi wa muhilimili uliojichimbia chini,nchi inazama kama MV bk vibaraka wake wanashangilia na kupongeza ujinga
 
Walimu 4000 wanahitajika,waombaji 91000.
 

Hakukuwa na mlipuko wa Zika. Rais hskuelewa taarifa hiyo ya utafiti na hakuwa na subira ya kueleweshwa. Kilichoripotiwa ni matokeo ya utafiti ni kuwa kuna baadhi ya watu wanayo chembechembe za kinga (antibodies) dhidi ya virus vya Zika. Tafsiri ya haraka haraka ni kuwa watu hao walipata kukutana na virusi hivyo. Inasikitisha sana Rais kuendelea kuxungumzia tukio hilo ambapo watu wengi hawapendi hata kukumbushwa licha ya mhusika kutuhumiwa bila ushahidi wa maana. Hata kama husika za rais zina ukweli hastahili kuwasilisha kwa njia aliyotumia.
 
Inawezekana hakutumiwa, lakini blunder aliyoifanya ikaacha nashaka hayo...

Hapo hakuna blunder iliyofanyika. Hiyo ndiyo kazi ya wanasayansi; hawapaswi kuomba idhini ya watawala kutoa matokeo ya utafiti wao.
 
Sometimes it needs to be smart or intelligent enough to understand the intelligent person.

Pia,wakati mwingine inahitaji uwe expert kumuelewa expert.
Kwani haiwezekani kwamba Mwele alikuwa anatumiwa?It is very possible.Nadhani inahitaji mtu mwenye akili pia kujua kwamba Mwele alikuwa anatumiwa.Tuliona upuuzi Marekani na WHO waliokuwa wanataka kuufanya kuhusu Ebola.Where is it.Tusingecharuka wakajua kwamba tumejua plans zao, inawezekana leo tungekuwa na Ebola nchini.Wake up fella.
 
Na yeye mwenyewe mbona mara nyingi amesema uwongo lakini sisi wananchi ambao waajiri wake, hatujamfukuza?

Kuna wakati mtu anaweza kutoa taarifa isiyo sahihi kutokana na taarifa alizopewa na wasaidizi wake.

Neno vita ya uchumi linatumiwa vibaya.

Please Bams, haya ni mambo ya kisayansi yanahitaji kutafsiriwa kitaalam. Taarifa ya Mwele iko sahihi mpaka kesho. Taarifa haikusema kuna ugonjwa wa Zika. Taarifa hiyo ilionyesha tu kuwa baada ya vipimo vya damu kuchukuliwa kuna watu ambao wameonekana miili yao ilipata kukutana na virus vya Zika na kuacha alama/nyayo. Mambo haya hufanyika duniani kote na hata hapa kwetu yamekuwa yakifanyika miaka yote. Tatizo hutokea tu pale viongozi wa kisiasa wanapokuwa hawapati au hawatafuti ushauri wa kitaalam.
 
wivu wa kike,

Nappe- "ushamba tu"

Januaru "Mshamba sana"
 

Siyo vimelea vya Zika virus bali nyayo zake; kwamba mtu huyo alishapata kukutana ni hivyo vimelea. As simple as that!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…