Rais Magufuli amnyooshea kidole Mwele Malecela asema alitumiwa na mabeberu kutangaza ugonjwa 'hewa' wa Zika

Rais Magufuli amnyooshea kidole Mwele Malecela asema alitumiwa na mabeberu kutangaza ugonjwa 'hewa' wa Zika

Hata dengue pia ilikimbia???

usipime dengue ilikimbiza na iliondoka na roho za watu dar, sema taarifa za uwepo wake ziliminywa ikawa mara kipindupindu mara malaria.

Watu wakaambiwa ukijisikia hivyo tumia panadol na maji kwa wingi
 
Sijui dr Mwele alimkosea nn mh Raisi?! Dr Mwele atumwe na mabeberu ili iweje ? Kwa uchumi upi tulionao adi hao mabeberu waweke vita na Tanzania? 😰😰

Hisije ikawa Lemutuz alimfitinisha dada yake wa kufikia kwa Mh Raisi kwa kupitia Bashite

Lemutuz na watoto halali wa Malecela hawaelewani kwa Sababu ya tabia zake

Watoto wote ni halali.... Unless you are not a parent
 
Mzee ana chuki na kila mtu, kumfuta kazi kwake ndo alitegemea na Mungu afute ridhiki yake ama,yaan utadhani yeye ndo mtoa ridhiki
Bilashaka alitegemea Mwele kwenda kumuomba msamaha nakujipendekeza,kupata kazi kwingine ni dhahiri kakwazika.
 
Mwele alikuwa na mamlaka ya kutangaza hali ya hatari ya ugonjwa kama huo? Au kuna utaratibu ilitakiwa afuate? Shida Tz tunaingiza mambo mengi sana na Siasa na tunaanzia hapo kukwama
 
Kwani magu anaguataga utaratbu atakapoamkia siku hiyo ndio utaratibu utakavyokuwa. Tatizo lipo kwa kiongozi wa muhilimili uliojichimbia chini,nchi inazama kama MV bk vibaraka wake wanashangilia na kupongeza ujinga
Kwa nini Mwele hakufuata utaratibu wa kawaida wa kumuarifu Waziri wa afya kabla hajatoa lile tamko!?
 
Kwani hyo magu huwa anafuata utaratbu, anapoamkia siku hiyo ndio utaratibu utakavyokuwa. Tatizo lipo kwa kiongozi wa muhilimili uliojichimbia chini,nchi inazama kama MV bk vibaraka wake wanashangilia na kupongeza ujinga
 
Kwa hiyo unafuta kauli ya Rais muwekezaji ktk miradi isiyo na return, kutoa "Elimu ya hovyo kupata kutokea"?
Na unaamini Elimu bora inaweza kutolewa bila ya ujenzi wa miundo mbinu niliyotaja ili kuweka mazigira mazuri kumuwezesha mwanafunzi kujifunzia na kuongeza idadi ya waalimu wa kutosha?
Hata hivyo haya hapa majibu yake kwa miradi unayodai haina returns:

Walimu 4000 wanahitajika,waombaji 91000.
 
Hivi Tanzania mamlaka huwa zinafanyaje kazi?

Mathalani kama kuna mlipuko wa ugonjwa mkubwa kama Zika, si kwamba kabla ya kujulikana kwa wananchi Rais inabidi afahamishwe na waziri husika?

Ilikuaje Mwele kutangaza tamko kubwa kama lile pasipo kuwa na backup ya waziri wake?

Hakukuwa na mlipuko wa Zika. Rais hskuelewa taarifa hiyo ya utafiti na hakuwa na subira ya kueleweshwa. Kilichoripotiwa ni matokeo ya utafiti ni kuwa kuna baadhi ya watu wanayo chembechembe za kinga (antibodies) dhidi ya virus vya Zika. Tafsiri ya haraka haraka ni kuwa watu hao walipata kukutana na virusi hivyo. Inasikitisha sana Rais kuendelea kuxungumzia tukio hilo ambapo watu wengi hawapendi hata kukumbushwa licha ya mhusika kutuhumiwa bila ushahidi wa maana. Hata kama husika za rais zina ukweli hastahili kuwasilisha kwa njia aliyotumia.
 
Inawezekana hakutumiwa, lakini blunder aliyoifanya ikaacha nashaka hayo...

Hapo hakuna blunder iliyofanyika. Hiyo ndiyo kazi ya wanasayansi; hawapaswi kuomba idhini ya watawala kutoa matokeo ya utafiti wao.
 
Sometimes it needs to be smart or intelligent enough to understand the intelligent person.

Pia,wakati mwingine inahitaji uwe expert kumuelewa expert.
Kwani haiwezekani kwamba Mwele alikuwa anatumiwa?It is very possible.Nadhani inahitaji mtu mwenye akili pia kujua kwamba Mwele alikuwa anatumiwa.Tuliona upuuzi Marekani na WHO waliokuwa wanataka kuufanya kuhusu Ebola.Where is it.Tusingecharuka wakajua kwamba tumejua plans zao, inawezekana leo tungekuwa na Ebola nchini.Wake up fella.
 
Na yeye mwenyewe mbona mara nyingi amesema uwongo lakini sisi wananchi ambao waajiri wake, hatujamfukuza?

Kuna wakati mtu anaweza kutoa taarifa isiyo sahihi kutokana na taarifa alizopewa na wasaidizi wake.

Neno vita ya uchumi linatumiwa vibaya.

Please Bams, haya ni mambo ya kisayansi yanahitaji kutafsiriwa kitaalam. Taarifa ya Mwele iko sahihi mpaka kesho. Taarifa haikusema kuna ugonjwa wa Zika. Taarifa hiyo ilionyesha tu kuwa baada ya vipimo vya damu kuchukuliwa kuna watu ambao wameonekana miili yao ilipata kukutana na virus vya Zika na kuacha alama/nyayo. Mambo haya hufanyika duniani kote na hata hapa kwetu yamekuwa yakifanyika miaka yote. Tatizo hutokea tu pale viongozi wa kisiasa wanapokuwa hawapati au hawatafuti ushauri wa kitaalam.
 
Akielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.

Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!

Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.

'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.
wivu wa kike,

Nappe- "ushamba tu"

Januaru "Mshamba sana"
 
Inaonekana uelewa wako ni mdogo sana katika masuala ya afya.

Dr. Mwele hakuwahi kusena kuwa Tanzania kulikuwa na ugonjwa wa zika bali alitoa taarifa ya matokeo ya tafiti ambapo ilionekana kwenye sample za zilizochukuliwa kwa baadhi ya watu kuna vimelea vya vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa zika.

Tusiwe wendawazimu wa kujifanya tunaelewa kila kitu. Na wala tusiwe wapumbavu wa kudanganywa na maneno ya wanasiasa laghai.

Siyo vimelea vya Zika virus bali nyayo zake; kwamba mtu huyo alishapata kukutana ni hivyo vimelea. As simple as that!
 
Back
Top Bottom