Rais Magufuli amteua Dkt. Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

Rais Magufuli amteua Dkt. Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

Mkuu Froida katika mazingira kama haya unaweazaje kutofautisha udukuzi na kuhusika? Au tuweke hivi alidukua kwa kuhusika.

Mtu anayepaswa kushika ukuu wa idara nyeti moyo wa nchi kama TISS hawezi kuwa kipilimba ambaye amehusishwa na kuiba kura na kuiibia umma na jeshi la polisi fedha za Lugumi haiwezekani yeye mwenyewe ajiuzuru kwa sababu ataleta madhara makubwa nchi hii kama kiongozi huyo hana intergrity na watu wengi wanajuwa maovu yake watakosa imani na chombo chao
 
Nimekusoma vizuri, ila kuna sababu ya Dr Kipilimba kuzungukazunguka kila idara.

Halafu, unafikiri mheshimiwa raisi amekosea uteuzi au vipi?
mara nyingi rais amekosea kwenye teuzi zake kuanzia wakurugenzi wa halmashaurii.wakuu wa wilaya ndio maana wengine wametenguliwa muda mfupi baada ya kuteuliwa
 
Binafsi nimefurahi sana kuteuliwa mtu ambaye alikuwa anafanyia nje sijui wanaitwa undercover agents au field officers.Nadhani Rais anajua anachokifanya.
Nasikia hata miaka ya utawala wa Mwinyi kuna mjeshi mmoja alikuwa ni mkuu wa mkoa akateuliwa kuwa mnadhimu mkuu wa jeshi. Yaani waliokuwa jeshini hawakumfikiria kabisa na alivyoanza majukumu yake akaimarisha utendaji na nidhamu
 
Huyu ni jipu lenye usaha w a kilo mia mtu si msafi kabisa mtuhumiwa kwa kiwango kikubwa kama cha huyu mtu hawezi pewa idara nyeti kama hiyo hana intergrity katuhumiwa kuiba kura katuhumiwa kufanya biashara ovu na akina Lugumi halafu unampa kitengo nyeti kama hicho halafu Magufuli anadanganya umma eti anatetea watu anyone kweli serikali ya CCM ni ya mafisadi mwendo mzima
Hujitambui mkuu. Pole sana.
 
Waambie hao. Mkapa alikuwa paparazi, na mzee Mwinyi alikuwa mwalimu, Marehemu Filikunjombe alikuwa polisi. Kazi ya zamani hai-determine utakuwa nani huko mbeleni. NUKTA.
na Mbowe alikuwa Dj...ahahahaaa
 
Miaka hamsini madawati mashuleni hamna hayo si maajabu ya dunia tena tuna misitu ya kutosha.
yani issue ya upungufu wa madawati ndio kwako ni issue ya kukufanya useme bado tupo pale pale baada ya miaka 50 ya uhuru? mafanikio yaliyopatikana huyaoni? kumbe wewe bado sanaaaaaaa.............
 
yani issue ya upungufu wa madawati ndio kwako ni issue ya kukufanya useme bado tupo pale pale baada ya miaka 50 ya uhuru? mafanikio yaliyopatikana huyaoni? kumbe wewe bado sanaaaaaaa.............
Ukishindwa kwa kitu kidogo usitegemee mafanikio ya vtu vingine. Nusu karne ni miaka mingi mno ukicompare na nchi tulizokuwa nazo sawa kiuchumi na sasa zimepiga hatua kubwa kiuchumi had kuingia level nyingine.
 
Kuna wengine wanashindwa kujua TISS inafanyaje kazi, ni kama mkondo wa umeme, negative in mhimu kufikia malengo. Wengine naona wanashupalia mbona vile mbona hivi kwa kuangalia positive side, ila
wanasahau kujua mission ilikuwa ni nini. Tusifunze kusoma kutoka kulia kwenda kushoto, sio kushoto kwenda kulia muda wote, ili kuongeza
maarifa, na muda mwingine tuwe wasomaji tu, sio kila uzi tuchangine hata kama uzi umetuzidi uwezo. Naomba niishie hapo.

Mkuu uko sahihi kuturekebisha na pengine hilo neno Mission tutakwambia ni RC mission ya peramiho hatujui maudhui, muda, maadili, mamlaka na kazi za hao jamaa
 
Ukishindwa kwa kitu kidogo usitegemee mafanikio ya vtu vingine. Nusu karne ni miaka mingi mno ukicompare na nchi tulizokuwa nazo sawa kiuchumi na sasa zimepiga hatua kubwa kiuchumi had kuingia level nyingine.
dada yangu, mafanikio siku zote hupimwa kwa kuangalia wapi mtu alipotoka na alipofikia ndani ya kipindi fulani cha muda (ulikuwa unaogeshwa ila sasa unaoga mwenyewe, hayo ni maendeleo) and the same principle applies kwenye kupima maendeleo ya nchi. nchi haziwezi kufanana hata siku moja. japan ilivyo leo hii haiwezi kufanana na U.S.A ingawa zote zinasemekana ni nchi za dunia ya kwanza
 
kazi gani wakati mashirika ya umma yanakufa? Hawana faida yoyote kwa Taifa
Mtu aliye timamu hutumia ubongo wake kufikiri. Nakushauri, jua kwanza kazi zao na kisha soma sana lakn ukishindwa, usijibu maana utaonekana jinsi usivyo muelewa kwenye uzi muhimu kama huu. Ni vyema kuelewa na sio kushabikia.
 
Back
Top Bottom