Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo amewasilisha bungeni jina la Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alipokea barua iliyotoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa watumishi wa chombo hicho cha kutunga sheria na baada ya kuifungua ndipo aliposoma ujumbe huo uliotaja jina la Majaliwa ambaye alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.

Baada ya tangazo hilo ambalo lilipokelewa kwa shangwe na wabunge wengi, Spika Ndugai aliahirisha bunge kwa dakika arobaini na tano kuwapa nafasi wabunge kutafakari uteuzi huo kisha kumthibitisha bunge litakaporejea.

Waziri Mkuu huyo mteule alizaliwa Disemba 22, 1960 na kupata elimu katika Shule ya Msingi Mnacho kati ya mwaka 1970-1976 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Kigonsera kati ya mwaka 1977- 1980.

Mwaka 1991-1993 alijiunga na Chuo Cha Ualimu Mtwara. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1994 na kuhitimu mwaka 1998 kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Stockholm nchini Sweden kwa masomo ya juu.

Amehudumu katika nafasi mbalimbali tangu mwaka 1984 alipojiunga na utumishi wa umma kama mwalimu mkoani Lindi, Katibu wa Chama cha Waalimu Wilaya, Katibu chama waalimu Mkoa na Mkuu wa Wilaya.

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kabla ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumteua mwaka 2012 kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu.

/Mwananchi Digital.

 
" Uteuzi uliofanywa ni makini na sahihi"-Lukuvi
 
Hongera kwake ila kiukweli mambo bdo magumu tz

Huyu mteule aliuwa deputy wa shemeji yake mwingine kikwete (ghasia) Tamisemi. Na wote tunafahamu namna ambavyo Tamisemi ya kikwete ilivyokuwa hopeless then Tamisemi hiyo hiyo inatupa PM- nchi hii vituko havitaisha na maendeleo tusahau jumla at least kwa generations kadhaa.
 
"Wabunge wote hawajawahi kugombana na Ndugu Majaliwa"-Lukuvi
 
1447921044311.jpg
 
Kama unataka Kaanani nenda Kwa MZEE WA MISUKULE aka MSHENGA....
 
MTAJIBEBA NA MBEREKO!!!! Hii ndio CCM chama cha Kitaifa..... Team inapangwa kwa kuzingatia Uwezo, Matabaka, Kanda, na Jinsia...... Rais - Kanda ya Ziwa (Mwanaume)..... Makamu - Zanzibar (Mwanamke)....Speaker....kanda ya kati (Mwanaumeme) ......Naibu Speaker Nyanda za juu kusini (Mwanamke)...... Waziri Mkuu ....Kusini Pwani (Mwanaume)...... CCM ni Raha tupu.....purely Scientific........ Walee jamaa Zetu Wanazidi kupagawa!!!

Hebu zirudie tena kuzisoma hizi pumba kama zina maana
 
Wazir mkuu mteule akitaka kusikia wasifu wake akiwa marehemu, basi awasikilize wanafiki wanavyompamba leo, hata akijamba watasema marashi, teeh teehtee
 
" Jambo la leo ni la kikatiba na kikanuni nimpongeze Rais kwa kutekeleza jukumu hili kwa umakini mkubwa sana"- Mhagama
 
" Hakuna mbunge atakayesema hapa Majaliwa si muadilifu au ana kashfa katika suala la uongozi"- Mhagama
 
Uteuzi uuu mmmh tunazid kuona watu Wa awamu ya 4 naweza ungana na msemaji aliyepita kuwa bado c than make now kuna miemko mingi ya kisiasa anapidi ajipange kukabiliana na lissu,mnyika kubenea na mdee plus msigwa na sugu naiman watamsumbua sana na hapa atuitaj majibu mepesi unaulizwa swali unasema Mara tuko atua za mwisho Mara ntaunda tume ichunguze plus upembuz yakinifu no tunaitaji vitendo na sikukanusha kazi njema pm.
 
We si ulisema Mwigulu ni genuine pekee aliyebaki??!!
Mkuu OLESAIDIMU, rejea bandiko lile niliposema Mwigulu is the best, if the best if what Magufuli was looking for!. Japo Magufuli ni mtu mwingine lakini CCM ni ile ile!. Magufuli ameshauriwa kuweka boya he can push around atakavyo!. Angemuweka Mwingulu au Prof. Mhongo hawa ni watu real and genuine!, you can't push them around kuwaswaga tuu kama ling'ombe.

CCM ni ile ile kuwachagua watu fulani fulani kwa sababu za kijinga jinga tuu!. Kikwete mwenye GPA ya 2.1 alisimama na Prof. Mwandosya mwenye best brain ya GPA ya 4.5!, na Dr. Salim hata kwa macho tuu anaokena intelligent!. Sisi wengine vilaza unawaona kwa naked eyes. Kati ya watatu hao, kilaza wao ndio alikuwa JK, lakini ndie aliyechaguliwa na sababu zikatolewa ni 'mtu wa watu', ana 'sura nzuri', ana 'cheko na bashasha' hivyo anapendwa na watu na anachagulika kuliko hizo best brain!. Hizo ndizo zilizomfanya JK apete na matokeo tumeyaona!.

Ndani ya CCM kuna vichwa, vilaza na magarasa!, mtu anapoacha kuchagua vichwa na badala yake kucheza na magarasa, then lets hope hivyo vichwa kama Mwingulu, amemsave the best for the last kumleta kwenye wizara ya Fedha na Uchumi au Viwanda, Biashara na Uwezeshaji!. Na Prof. Mhongo kwenye wizara ya Nishati na Madini!.

Haijalishi PM ni nani, bali the reasons behind kwa nini ni fulani!.

Lowassa alipokuwa PM alimu outshine vibaya JK!, kwa sababu EL was was dominant gene na JK was weak!, hivyo kumfix was appropriet!. Ben was dominant Sumaye was weak!. Magufuli is dominant, Majaliwa is weak! tena usikute its true ni shemeji wa JK kama ilivyo kwa Hawa Ghasia au Shukuru Kawambwa!, pia tujiandae kwa R1 kupewa u Deputy, 2020 full minister ready for 2025 ni zamu ya Muislamu!.

Pasco
 
Ndugu yangu usipoteze muda wako kusifia huu uozo, hapo hakuna jipya anafanyia kazi maelekezo ya Msoga!! Ningemwona hatabiriki kama angemwibua mtu kama Livingstone Lusinde, Steven Ngonyani, Jah People (ha ha ha haaa utani mkuu). Sasa hapa katumia ushauri wa Msoga ili kuwapoza na maumivu ya kuukosa urais kama walivyokuwa wamejipangia (mama Salma huyo). Gufuli naye afanye kwa kujitegemea bwana, hiyo nafasi ajue kabisa hakuipata kwa hisani ya watu wa Msoga (vinginevyo atatufanya tuamini kwamba alikuwa amepigwa kwenye sanduku la kura, akabebwa na Msoga - ingawa kuna kachembe ka ukweli).

UKIWA msipoteze muda! ni wakati wenu kijipanga ...la Kwanza mchagueni MAMVI awe officially Kiongozi Mkuu wa chama ili aweze kufarijika na mahela aliyoyapoteza..... Pili mjiulize sababu za msingi na kisayansi za wananchi kutokuwa na Imani na nyinyi! Jogooo linaendelea kuwika..... na NYUMBU wanazidi kutawanyika na kutahayari!
 
" Kwa kasi ya Rais tunahitaji umri wa ujana na Majaliwa anaweza kufanya kazi hii kwa viwango hivyo"- Mhagama
 
Back
Top Bottom