Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Hilo siwezi kulisemea kwa sasa. Tuone kwanza utendaji wake, hapo ndio tutaweza kutoa hukumu.
wasiwasi wangu ni kuwa Mizengo alishangiliwa sana hata zaidi ya huyu lakini mwisho wa siku tumejionea wenyewe, mimi nafikiri watanzania tuache kuwa na expectations kubwa na hawa wateule na wachaguliwa kwani mwisho wa siku wanatuangusha vibaya
 
Ona jinsi hii nchi ilivyo ya hovyo.

Huyo Kassim keshateuliwa na ndo imetoka hiyo.

Hakuna cha kuthibitishwa na kamati ya bunge wala bunge lenyewe.

Ukishateuliwa tu ndo basi.

Ovyo kwa lipi? Ulitaka achaguliwe na udaku wa magazetini? Huyo ndiye Magufuli kachagua mtu ambaye hajachakachuliwa.
 
Huu mfumo unakatisha tamaa hata vijana yani vigezo vinakuwa ukabila,ukanda, ujinsia,udini eti kubalance mambo na nchi !wtf! Haya angalia watu waanza kusema 2025 muislam pasipo kujua atakuwa na uwezo au vp? Mbona nyerere aliwajaza wachaga maofisini kwa sababu walikuwa wamesoma! Kenya hamnna ujinga huo km unajua unanguvu pambana sio kubalance mambo! Unamuachaje mwigulu, muhongo, mwakyembe, unamleta majaliwa ili iweje? Yawezekana leo ikawa turning point yangu kutoka ccm au kuacha kufikiria km ntaingia siasani ! Km jpm maguli ni jembe kaogopa nini kuchagua majembe menzake? Hapa kinana kaniangusha
 
Nasubiri kumfahamu waziri wa fedha, maana taifa limeishi miaka 10 bila ya kuwa na waziri wa fedha aliyethabiti mwenye kuiongoza wizara kitaalamu na badala yake tumeona mawaziri wa fedha wakiiendesha taasisi hiyo kisiasa na kiuswaiba na hatimaye kuuvuta shati uchumi wa Taifa letu.
 
Swalia alilouliza angela kairuki kuanzia leo nimemtoa thaman.Et magdalena sakaya ww ni cuf spika ni ccm sasa ukpata ucpka mtafanyaje kazi wakat vyama tofaut.
 
Baada ya Rais kupendekeza jina la Kassim Majaliwa kwa nafasi ya U-pm.

Kama atapita anaenda kuwa Waziri Mkuu wa 11 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo ndio atakuwa mtendaji mkuu wa shughuli zote za serikali. Waziri Mkuu akichemsha, Serikali nzima imechemsha.

Mawaziri Wakuu wengine waliomtangulia ni Jk Nyerere, RM Kawawa, EM Sokoine, Cleopa Msuya, Salim A Salim, Warioba, Malecela, Sumaye, Lowassa na Pinda.

Ipi ni top 3 ya Mawaziri Wakuu bora wa wakati wote ambao walipiga kazi iliyotukuka katika Nchi hii.

hivi Kambona alikua nani vile maana hata kwenye vitabu hatumuoni
 
Back
Top Bottom