Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Siyo kweli, Jiwe linatafuta kick tu, Sugu kasema hotel imejengwa kwa kufuata vibali vyote. Na kama hao mburula wangeamua kuvunja ni ukweli husiotia shaka Sugu angefungua kesi mahakamani na hata mahakama ingemuabudu Jiwe kuna siku haki ingetendeka tu, bila shaka lingekuwa swala la muda tu. Kwani Jiwe ni nani bhana? Angekaa madarakani muda wote?
Wakati Rais Magufuli akiwa ziarani Mbeya mwaka jana Sugu alipanda kwenye gari ya mh Rais na kupewa kipaza sauti kisha akawatangazia wana Mbeya kwamba anamuunga mkono Rais Magufuli kwa 100%

Sitashangaa kumuona Sugu CCM!
 
Yaani Sugu amefuata taratibu.na sheria zote kujenga hoteli yake, leo anaonekana shujaa yule aliesema hoteli isibomolewe, na chakushangaza zaidi, wavivu wa kifikiria wanamuona shujaa alietoa tamko hoteli isibomolewe!.

Naona kama taifa tunaanza kurudi nyuma sasa, sio kiuchumi na mambo mengine pekee kama utawala bora, bali hata uwezo wetu wa kufikiri nao umeathiriwa na awamu hii ya tano.
Ukumbuke alieshukuru ni Sugu mwenyewe tena bila shurti.Labda kama wewe unalijua zaidi swala la hotel ya Sugu kuliko Sugu mwenyewe utueleze
 
Wakati Rais Magufuli akiwa ziarani Mbeya mwaka jana Sugu alipanda kwenye gari ya mh Rais na kupewa kipaza sauti kisha akawatangazia wana Mbeya kwamba anamuunga mkono Rais Magufuli kwa 100%

Sitashangaa kumuona Sugu CCM!
Utasubiri sana, kwani Magu akitumia kodi za watanzania kuleta maendeleo kwa kufuata utaratibu CHADEMA wana shida? Don't miss the point, CCM ni chama tu, na Magu ni bindamu kama wewe anaenda chooni kama wewe kukata gogo na kuna siku isiyokuwa na jina nafsi yake itaonja umauti vilevile na Tanzania itabaki pale pale. Yaani tuache kumtukuza Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi tuanze kumtukuza Magu. Kama unajitambua utakuwa umenielewa!
 
Tanzania sio nchi tena tumeshuka mpaka kuwa familia, ni mwendo wa maagizo tu hata kama hayafuati utaratibu ila ni maagizo tu
 
Mambo kama hayo ya kutofuata taratibu na mtu mmoja kuamua kuwa juu ya katiba yakifanyika kwenye vyama vyenu vya siasa hamkemei ndio kwanza mnashabikia tu.

Weka mfano ili tuanzie hapo.
 
Makamanda uchwara wataita huo ni usaliti.
Kushukuru ni jambo jema
Ila watanzania wajifunze kupitia sugu
Wawekeze nyumbani maana kna mijitu inakwapua hela inaficha nje hela zingine wanakula na familia yao

Ova
 
Shukrani hizo zimekuja baada ya mheshimiwa rais kumtuma mkuu wa mkoa wa Mbeya kuzuia ubomoaji wa hoteli ya Desderia iliyokua inadaiwa ujengwa eneo la chanzo cha maji

Rais Magufuli amesema Sugu kama muwekezaji aliyeamua kuwekeza mbeya pia apewe kipaumbele kwenye maeneo mengine ya uzunguni aweze kuendeleza uwekezaji

Maendeleo hayana vyama

Utamaduni mpya wa kupenda kiki walitaka kumfanyia ya Mbowe ili wapewe vyeo lakini wameona itakuwa wazi sana
 
Utasubiri sana, kwani Magu akitumia kodi za watanzania kuleta maendeleo kwa kufuata utaratibu CHADEMA wana shida? Don't miss the point, CCM ni chama tu, na Magu ni bindamu kama wewe anaenda chooni kama wewe kukata gogo na kuna siku isiyokuwa na jina nafsi yake itaonja umauti vilevile na Tanzania itabaki pale pale. Yaani tuache kumtukuza Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi tuanze kumtukuza Magu. Kama unajitambua utakuwa umenielewa!
Mbona maneno mengi bwashee?!!!

Hapo Chadema asiyeitamani CCM ni Tundu Lisu pekee waliobaki wote mnafanana na Halima James Mdee!
 
Mbona maneno mengi bwashee?!!!

Hapo Chadema asiyeitamani CCM ni Tundu Lisu pekee waliobaki wote mnafanana na Halima James Mdee!
Maneno mengi unaleta wewe na upumbavu wako wa kumtukuza binadamu aliyezaliwa na mwanamke kama wewe.
 
Nime
Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.

Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.

Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.

Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Maendeleo hayana chama

View attachment 1659613
Ngozi nyeusi tuna roho mbaya sana
 
Maneno mengi unaleta wewe na upumbavu wako wa kumtukuza binadamu aliyezaliwa na mwanamke kama wewe.
Aliyeshukuru kwa RC Albert Chalamila ni mbunge mstaafu wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Kama hutaki kunywa pipa la mbege kwa hasira!
 
Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.

Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.

Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.

Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Maendeleo hayana chama
Yale yale ya kikokotoo.Kawatuma watu wake watikise na kupima upepo kisha anajitokeza kuagiza vinginevyo.Kiki za hovyo kabisa!
 
Aliyeshukuru kwa RC Albert Chalamila ni mbunge mstaafu wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Kama hutaki kunywa pipa la mbege kwa hasira!
Kwa hiyo akishukuru tayari anamkubali Jiwe siyo? CCM mnafeli wapi?
 
Ingebomolewa ungesema ni uonevu sasa haijabomolewa unatukana. Hivi ulitaka nini haswa?

Rais wetu ni wa kila chama, kila kabila, kila dini, kila rangi, kila mkoa

Nchi yetu sio takataka mkuu ila mawazo yako uliyoyaandika hapa ndio takataka
Issue siyokubomolewa au kuachwa, issue ni sheria na taratibu tulizojiwekea.

Hata huyo Magu anatakiwa kufuata taratibu na sheria. Ndio maana sheria zipo mpaka namna ya kusamehe wafungwa.

Sasa yeye aseme, Sugu alikiuka taratibu zipi wakati wa ujenzi na hao NEMC walikuwa wapi wakati anajenga?

Huyo Magu anaesema kwa HISANI YAKE tu kwamba Jengo lisibomolewe kwahiyo siku akikosana na Sugu wanabomoa ???

Anyway, hivi ile nyumba ya Marehemu Mch Rwakatale mlishabomoa.

RIP UTAWALA WA SHERIA. Mamboya Cherry Picking.

Watu wa Kimara, bomoa Nyumba hata kama wana COURT INJUCTION, watu wa Airport Mwanza hao msibomoe ndio walinipa KULA.

Aibu ya MTU MWEUSI.
 
Back
Top Bottom