Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Watu wa Mipango Miji nchi hii nadhani ndio idara inashida zaidi..Masquatter ni kila sehemu katika nchi hii.unashindwa kuelewa hawa jamaa huwa wapo kweli kazini???
 
Hapa Jiwe anatuonesha kua yeye ndo kila kitu akiamua itabomolewa naasipoamua haitabomolewa...kazi kweli kweli alichokua anakitaka tu ashukuriwe.
 
Watanzania wengi wamefurahishwa na hatua ya Rais Magufuli ya kusimamisha nia ovu waliyokuwa nayo watendaji wa serikali ya kutaka kubomoa hoteli maarufu ya aliyekuwa mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu.

Kwa bahati nzuri huyo Sugu ameeleza kuwa hoteli yake hiyo ilikuwa na vibali vyote vya mamlaka zinazohusika za kukamilisha ujenzi huo.

Swali linakuja hao watendaji waliotaka kuibomoa hotel I hiyo, walipata wapi kiburi hicho cha kutaka kuibomoa hoteli hiyo, wakati wakijua fika kuwa mwekezaji huyo ana vibali vyote vya mamlaka husika?

Kama hao watendaji hawajapata kiburi hicho kwenye mamlaka za juu za nchi, basi tunategemea hao watendaji waliokuwa na nia hiyo ovu watumbuliwe mara moja.

Kinyume cha hapo tutakuwa tunajenga nchi ambayo baadhi ya watendaji wanaweza kujiamulia mambo yao kwa lengo la visasi tu kwa ajili yakuwakomoa baadhi ya wananchi.

Kama kweli Rais Magufuli ameitoa hiyo kauli bila unafiki wowote, basi tunamtegemea awatumbue haraka hao watendaji wa serikali waliotaka kuibomoa hiyo hoteli, kinyume cha taratibu kwa lengo tu la kutaka kumkomoa Bwana Sugu.

Kwa kuwa sisi wananchi tunamjua Rais wetu kuwa ni mtu asiyetaka masihara hata kidogo na ni mwepesi sana wa kuwatumbua watendaji wake hata kwa "vijikosa" vidogo, basi tunatarajia kwa hawa watendaji wake ambao walitaka kubomoa hiyo Hoteli ya mamiloni ya shilingi za mwwkezaji mzawa wa kitanzania, ambaye amefiata taratibu zote za uwekezaji, basi tunatarajia atawatimbua mara moja ili kuondoa fikra za wananchi wengi kuwa huyo Sugu alitaka kukomolewa kwa kuwa ni kiongozi wa Chadema, hasa tukitilia maanani usemi maarufu wa Rais wetu Magufuli kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA
Wazo la kubomoa hoteli ya sugu lilianzia katika inner circle zao gvt na CCM hivyo hata wazo la kutokuibomoa limetoka kwao na sababu zaweza kuwa hizi.

1.Wamepima upepo wa kisasi wawatu wa mbeya Kama wangebomoa hiyo hotel.

2. Kupata political mileage ndio ile twasema tengeneza tatizo Kisha litatue upate maujiko.
 
Sasa hili swala linamhusuje rais mpaka yeye ndiye aingilie kwa kuagiza isibomolewe kwani alijengaje kama ujenzi kwenye eneo hilo ilikuwa hairuhusiwi kwani ina maana hakuwa na hati.

Mambo mengine yanatengenezwa tu ili watu wengine wapate kiki za kipuuzi na labda ili huyo anayetaka kubomolewa nyumba afikirie kubadili msimamo wake wa kisiasa. Nothing more.

Hii ndio kazi inayofanywa na huu utawala ni Blackmails tu na wala haina ajenda yoyote ya kuiletea nchi hii maendeleo. Bure kabisa.
 
Angezuia na billicanas isivunjwe au ndio anajisafisha kwa wananchi tumuone mpenda haki na mwenye huruma.....
 
Daniel mgogo ktk moja ya hotuba yake mbele ya John Joseph alipata kumwambiwa kuwa

Serikali inatoa kubali eneo fulani kujengwe jengo fulani.

Serikali hiyohiyo inakuja kustuka kuwa alaah kumbe hapa tulipaswa kupitisha nyaya za umeme wanakuja kubomoa.

Akatoa ushauri kuwa ni vyema kuhakikisha unapotoa vibali ujue kabisa miaka 40 ama 50 mbele eneo hilo litakuwaje. Isije kuwa serikali ya kujenga na kubomoa na kulipana fidia.
Huu ni mchango bora wa mwaka kwa kweli. Ni wachache wanaweza kumpatia magu kaushauri kenye masimango ndani yake.
 

Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.

Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.

Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.

Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Maendeleo hayana chama

View attachment 1659613
Huenda Chalamila ndiye aliunda Zengwe la hiyo Hotel kutaka kubomolewa
 
Haaa imeisha iyoo.
hapo Sugu kalainishwa tayari,tena ameshatoa na shukrani za dhati kwa muheshimiwa Rais ambae awali akutambua ushindi wake.
Tuhesabu siku.
Akuna mkate mgumu mbele ya chai.
Pale inapofikia nchi kuendeshwa kwa haramu na vitisho na baadhi ya wajinga kuona Ni halali na ujanja.
 
Nemc hivi wanajielewa kweli ifike hatua mambo ya kipumbavu wasiwe wanatueleza
Yaan mtu anunue eneo wanamuangalia tu aanze kujenga wanamtazama tu amalize ujenzi wapo tu then wanakuja kutueleza mtu yupo ndani ya hifadhi ya maji
Siku zote walikua wapi
Na je inafaida gani kuita vyombo vya habari na kutueleza hayo
Sisi watanzania wengine hatutaki uiinga huo wamalizane wenyewe huko
Mh JPM kafanya kweli na Mungu analiona hili.
Kuna wafanya kazi serikalini kazi yao ni kukomoa biashara.
 
Back
Top Bottom