Rais Magufuli amuapisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,895
Reaction score
20,392
RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba akila kiapo cha maadili ya viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimkabidhi kitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimuapisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016.Kushoto akisimamia zoezi hilo ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju na Katibu Mkuu kiongozi Engineer John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016.

Chanzo: Michuzi Blog
 
Hongera sana.Yaani wamependeza
Jina lake hapo limekosewa anaitwa KIPILIMBA sio KAPILIMBA .
 
Kila rakheli Dr Kipilimba!
Taifa letu kipenzi liendelee kuwa salama!
 
Kwa hiyo ndiyo ofisi zake kuanzia leo zitakuwa pale oysterbay jirani na kwa mtoto wa Bharessa.
 
Wazee hao wa kuhakikisha nchi iko salama full time 24 hours.Hawalali wanakesha kuhakikisha sisi raia tunalala usingizi mnono.Kikosi kizima hicho hapo.Mwenyezi Mungu awabariki sana tena sana kwa kazi yenu iliyotukuka mnayofanya.


Ila kule Kagera kuna wananchi 56 wameuliwa lakin hawa wamekaa kimya.
 
Wazee hao wa kuhakikisha nchi iko salama full time 24 hours.Hawalali wanakesha kuhakikisha sisi raia tunalala usingizi mnono.Kikosi kizima hicho hapo.Mwenyezi Mungu awabariki sana tena sana kwa kazi yenu iliyotukuka mnayofanya.

Safi sana. Chini ya hawa watu tuna kila sababu ya kulala usingizi
 
Ila kule Kagera kuna wananchi 56 wameuliwa lakin hawa wamekaa kimya.

Una andika utafikiri una ushahidi! Habari ambayo haijathibitishwa unatakiwa useme kwa habari ambazo hazijathibitishwa inasemekana watu 56 WALIULIWA.Unabeba chochote barabarani na kukiweka kama habari ya uhakika.Utakuja fungwa kwa umbeya na uwongo.Shauri yako.
 
Mkuu, hawa watu kazi yao ni kuropoka tu
 

Labda uko kwenu Lumumba ndio haijathibitishwa. Kwasababu nyie mmekaa kifisadi amuwezi kujali wananchi,ila policcm wakiuliwa mmaweweseka sana.
 
Safi sana. Chini ya hawa watu tuna kila sababu ya kulala usingizi
=======
Kule somalia, Misri, Israel, Alfghanstan, Libya na sasa Uturuki, hawa wapo na vifaa vya kisas kuliko vyetu, lakini usingizi hata wa kununua hakina madukani.
 
Naomba kazi yake ya kwanza iwe kutoa discipline kama ile ya Pemba mwaka 2001. Hakutakuwa na maandamano tena kama leo hii Pemba.
 
Kutoka benki kuu,kwenda Tume ya uchaguzi kipindi nyeti,nida,tiss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…