Rais Magufuli amuapisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba

Rais Magufuli amuapisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba

Huyu nae alikuwa pandikizi! Amewafanyia kazi nzuri tume ya uchaguzi NEC sasa amepewa zawadi yake ya kustaafia!! Hongera Dr....kazi na malipo yake
 
Tanzania regime... Tenda wema uende zako...

Huyu si katokea kule kwenye kshfya ya Vitambulisho? mmmh Mbona kama Mambo ni yale yale kosea huku pelekwa kule ukaharibu nako
 
Kha! Tunataka viwanda alivyoviahidi na sio mapicha picha, hayo mapicha na mateuzi yataleta viwanda?
 
Amani ni tunu ya pekee ya Taifa letu.

Mungu amtangulie, haya ni maombi yangu kwake.
 
Naipenda Tanzania yangu pamoja Na figusi zake.!
 
RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA
dg3.jpg

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba akila kiapo cha maadili ya viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
dg4.jpg

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimkabidhi kitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
dg5.jpg

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimuapisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016.Kushoto akisimamia zoezi hilo ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
dg6.jpg

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju na Katibu Mkuu kiongozi Engineer John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
dg7.jpg

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016.

Chanzo: Michuzi Blog
hapa nampa pongezi mh.magufuli kwa uteuzi wa mkurugenzi mpya wa TISS mr.kipilimbi ni mcha MUNGU na amekua akijihusisha sana. na kazi za kumtumikia muumba wake....inshort ni mcha MUNGU vibaya mno
 
Wazee hao wa kuhakikisha nchi iko salama full time 24 hours.Hawalali wanakesha kuhakikisha sisi raia tunalala usingizi mnono.Kikosi kizima hicho hapo.Mwenyezi Mungu awabariki sana tena sana kwa kazi yenu iliyotukuka mnayofanya.

dg7.jpg
msaada tafadhali. Wa kwanza kutoka kulia mwanamama ni mkuu Wa nini? Je na huyo anaemfuatia ni mkuu Wa nini? Hao wengine kwaanzia Mangu, mheshimiwa Rais, Kipilimba, Mwamunyange na mkuu wamagereza nawafahan nyadhifa zao. Msaada Hao wawili kutoka kulia dhadhifa zao.

Natanguliza Shukrani
 
Huyo mmama anawakilisha Uhamiaji, sijui kama ndo mkuu wa Uhamiaji.

Huyo wa kulia kwake ni kamishna wa zimamoto nchini.
 
Huyo mmama anawakilisha Uhamiaji, sijui kama ndo mkuu wa Uhamiaji.

Huyo wa kulia kwake ni kamishna wa zimamoto nchini.
Vick Lembeli mwanamama aliyevaa nguo za rangi ya dark blue ni Kaimu Kamishna jenerali wa Uhamiaji,Thobias Andengenye ni kamishna jenerali wa Zimamoto.
 
hapa nampa pongezi mh.magufuli kwa uteuzi wa mkurugenzi mpya wa TISS mr.kipilimbi ni mcha MUNGU na amekua akijihusisha sana. na kazi za kumtumikia muumba wake....inshort ni mcha MUNGU vibaya mno
Hongera yake
 
Back
Top Bottom