Rais Magufuli anaingizwa 'mkenge' na washauri?

Haieleweki unaandika kusukumwa na ukada miwani ya mbao uliyo vaa ivue utaona mbali
 
Nafurahi kuona bado kuna watanzania wenye maono na uchungu na nchi. Mungu ibariki Tanzania.
 
Utamlipa nini wakili Na hauna pesa.
 
Nakumbuka Kuna Jamaa alimshauri kuhusu Halmashauri/Agents wa serikali kuondoa fedha Banks Binafsi na zote kuzipeleka BOT itaathiri Uchumi aliongea saa mbili ilivyofika saa 6 usiku akatumbuliwa.

Mwanamama Dr Mwele Ntuli Malecela alitoa taarifa ya ugonjwa wa ZIKA kuingia nchini(Na ndio ulikuwa ukweli maana mama alikuwa NIMR) kilichotokea kila mtu anajua,ni sawa kwasasa kama kuna mtu yeyote aseme kwamba nchini kuna corona ,huyo mtu/mtumishi ataishia msitu wa PANDE au MTO RUVU kwenye kiroba.
 
Mwele mna mpamba tu kuwa NIMR hakumpi nafasi ya kutangaza Ugonjwa kama huo bila kufanya Assessment ya kutosha hasa kwa kuangalia athari za kiuchumi baada ya tangazo ilo, Mwele alitumika tu
 
Mwele mna mpamba tu kuwa NIMR hakumpi nafasi ya kutangaza Ugonjwa kama huo bila kufanya Assessment ya kutosha hasa kwa kuangalia athari za kiuchumi baada ya tangazo ilo, Mwele alitumika tu

Yaani ufiche Magonjwa kwa kuogopa uchumi utaathirika? Uchumi na Uhai kipi bora? Uchumi ukipiga mweleka ni rahisi kuurudisha ,vipi Uhai ukiondoka utaurudisha? Yaani ulitaka tumsubiri Ummy mwalimu aje kutulisha TANGO PORI LA ZIKA badala ya Wataalamu wa NIMR? Ummy ni mwanasiasa Mtu wa lONGOLONGO while Mwele ni MTAALAMU mtu wa Facts.
 
Nyerere is overrated.

Mkapa so far was the greatest president ever in Tz.

Nyerere ni hovyo kuliko hata Meko.

Sent from my SM-A720F using JamiiForums mobile app
 
Ahsante mkuu,kitu kidogo tu napenda kufahamu hapa...je ni ipi nafasi za ilani ya uchaguzi ya chama katika hili!?
 
Toka Magufuli aingie ameleta Kodi ipi mpya na amefuta Kodi ipi??
Suala la kurukia akaunti za watu kienyeji,waziri mpango juzi amelikemea na kulitolea maelekezo
Kuna maafisa wa TRA zaidi ya 50 nchi nzima chrismasi wamekula wakiwa hawana kazi
 
Toka Magufuli aingie ameleta Kodi ipi mpya na amefuta Kodi ipi??
Suala la kurukia akaunti za watu kienyeji,waziri mpango juzi amelikemea na kulitolea maelekezo
Kuna maafisa wa TRA zaidi ya 50 nchi nzima chrismasi wamekula wakiwa hawana kazi
Hawana kazi tu badala ya kuwa jela? Kuna watu wameandama kupinga wizi wa kura wako ndani mpaka leo, lakini waliovamia account za watu hawana kazi! Hapo utasema hajui kinachoendelea?
 
Weka ushahidi? Vinginevyo ni majungu.
Ushahidi gani unataka wakati yeye mwenyewe alikwishasema yeye ni JIWE na ukimshauri hatekelezi

Au Yusuf Manji hajui nini kilimtokea? Walipishana kauli wakati wa Kikwette, kauli tu lakini alichomfanyizia wote tunakijua. Yusuf Manji kafilisiwa na kafunga biashara zake zote. Ila waathirika ni wafanyakazi wake zaidi ya 3,000 na wakulima wa Mbezi na ufuta.

Imagine kodi ambayo TRA ilipoteza kutoka kwa wafanyakazi hao naexport levy ya ufuta. Ndivyo sasa TRA lazima wapambane kuipata kutoka mifumo mwingine.
 
Ahsante mkuu,kitu kidogo tu napenda kufahamu hapa...je ni ipi nafasi za ilani ya uchaguzi ya chama katika hili!?
Mkuu JokaKuu, kuna msemo nitaokautafsri kwa kiswahili kisicho rasmi

'' Niambie unachotaka kusema na si kile ninachotak kusikia'' . Vongozi makini huuzingatia sana usemi huu

Pili, The Boss anasema Rais anaingizwa Mkenge! sikubaliani na hoja kwa sababu zifuatazo
Ukimwacha Nyerere aliyetoka 'nowhere' na kuwa Rais, waliofuata walipata experience kwanza
1. Mzee Mwinyi alikuwa Waziri kamili, Rais wa Znz halafu wa muungano
2. Mzee Mkapa, alikuwa waziri kamili tena senior kwa awamu mbili
3. Mzee Kikwete alikuwa Waziri senior , wa fedha na mambo ya nje katika awamu mbili
4. Rais Magufuli amekuwa naibu waziri na waziri kamili katika awamu mbili mfululizo

Kwa mtazamo huo, uzoefu(experience) inakuwa wapi hadi kiongozi aingizwe mkenge na Washauri?

Tatu, JokaKuu anasema chombo cha kusimamia au kushauri ni Bunge. Ni kweli na ndivyo taasisi zilivyojengwa katika kumsaidia kiongozi wa nchi. Bunge hasa likiwa na Wapinzani linaiamsha serikali.

Bunge la chama kimoja ni 'caucus' kama halmashauri kuu au uvccm au uwt. Havina nguvu za ushauri na ni tatizo

Nne, nini nafasi ya ilani ya chama kama alivyouliza Ghwakukajha ? Well, chama kina ilani, wanaotekeleza ilani ni serikali kupitia Bunge. Unapokuwa na Bunge la chama kimoja ni sawa na 'kujitekenya halafu ucheke''

Tano, hoja ya mleta mada ina mashiko ukiitazama kwa jicho mujarabu.
Hakuna investment panapokuwa na mashaka. Kwa siku za karibuni kuna sheria zinatumika '' Arbitrary'' .

Mathalani hili la money laundering, kwa definition ni sheria inayotumika kwa malengo fulani si kwa kusudio lake.

Kuna sheria zinatoa nguvu kwa TRA kuingia na kufilisi.
Hata kama kuna ukweli, bado mtu makini atajiuliza sana ikiwa ni salama kuweka fedha nchini.

JokaKuu unakumbuka sheria za uhujumu uchumi zilivyolazimisha watu kuficha pesa.
Serikali ililazimika kubadili pesa ili watu wazitoe kwenye magodoro. Nadhani hatupo mbali na hatua hiyo.

Lakini kwa Wawekezaji ( FDI) mashaka tu yanatosha kuweka pesa zao nchi jirani au kutowezekaza kabisa
 
Mchane live huyo kima wa (MACHAGA)
 
Kwa hiyo Mwalimu utamuangalia kwa eneo hilo moja tu unalodhani wewe hakufanya vizuri?

Ni aibu sana kuendelea kuwa na kizazi kinacholalamikia mambo ya miaka 50 iliyopita.

Na ni nini ilikuwa nafasi yenu kama Wananchi iwapo kama mlikosa sabuni na dawa ya mswaki?.

Hivi ni Mwalimu aliwazuia Wananchi kutumia akili na kubuni/kutengeneza sabuni na dawa za mswaki?...ilikuwa ni lazima zitengenezwe na Wazungu ndio tuletewe tutumie?..vipi kama Wazungu wasingekuwepo ndio kusema Ngozi nyeusi tusingeyamudu kabisa maisha?.

Sehemu kubwa ya falsafa za Mwalimu zilikuwa zina make sense kwa wanaotumia ubongo vizuri. Kutofanikiwa ni sehemu ya matokeo maana pia huwezi kujua kufeli au kufaulu kwa jambo bila kufanya.

Hizo foleni za sabuni na sukari au kuvaa viraka zilipaswa kuwa ni kianzisho cha Vijana kubuni bidhaa zao...ndio maana alijenga vyuo vya ufundi kila Mkoa...ingawa hivyo viraka vilikuwepo hata wakati wa ukoloni.

Hii yote ya kuamini kuwa pesa ndio kila kitu kwa maisha ya binaadamu ni dhana za Wazungu ambayo Mwalimu hakutamani na sisi tuende huko. Sasa yeye akajaribu alivyojaribu kama ilishindikana basi tusonge mbele na si kubaki kulia lia miaka nenda rudi.
 
Hayo makampuni ya Iran na Venezuela sio Makampuni kwako?umeona Microsoft tuu.
 
Hawa MACHAGA tatizo lao hawadadavui mambo kwa kuzingatia Historia husika..wamejazwa miemko tuu.
 
Nadhani Magufuli Aendelee kukaza kamba ili mfe.
Ndo mtakuwa na akili.
alafu Leo ndo mwisho wa mwaka[emoji847][emoji847][emoji847].
Tunaingia mwaka wa 1.bado Kama 4 hivii.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Toka lini maiti ikawa na akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…