Rais Magufuli anaingizwa 'mkenge' na washauri?

Rais Magufuli anaingizwa 'mkenge' na washauri?

..mimi kwa uelewa wangu ni kwamba Raisi au kiongozi yeyote huwa ana AGENDA / VISION anayotaka kuitekeleza.

..Na agenda / vision hiyo hutokana na mambo mengi ikiwemo experience ktk makuzi na maisha, exposure, na elimu, ya Raisi au Kiongozi.

..kiongozi / Raisi anapochaguliwa na kuingia madarakani hutafuta watu ambao anaamini ni sahihi kumsaidia kutekeleza agenda / vision yake.

..kwa uelewa wangu kiongozi / Raisi huchagua watu " like minded " au wenye mitizamo kama ya kwake ili kumsaidia kuendesha serikali na nchi.

..tukirudi kwa Jpm, Watanzania tunapaswa kuelewa kwamba wateule wake ni watu ambao wako " like minded " au wana mitizamo kama ya aliyewateua.

..Wateule wa Jpm wanapofanya maamuzi na wasipochukuliwa hatua au hata kuonywa hadharani basi tukubali kwamba maamuzi hayo yana baraka za Jpm / aliyewateua.

..Kwa maoni yangu, ni makosa kuamini kwamba Jpm anaingizwa mkenge na wasaidizi ua washauri wake. Raisi na timu yake ni watu ambao wana mitizamo inayofanana, na wanatekeleza mambo ambayo wanaamini[ kutokana na experience, exposure, kujifunza] yanafaida kwa taifa.

Nani au Chombo gani kinapaswa kumrekebisha Raisi na Wasaidizi / Washauri wake?

..Kwa maoni yangu wanaotakiwa kumrekebisha Raisi na Serikali ni BUNGE. Hao ndio waliopewa dhamana kikatiba kufanya kazi ya kuisimamia na kuirekebisha serikali.

..Zaidi ya bunge, wananchi kupitia asasi mbalimbali, pamoja na vyombo vya habari, wanajukumu la kuisimamia, kuikosoa, na kuirekebisha, serikali iliyoko madarakani.

CC Gwakukahja
Kabla sijaanza ibaada ya kumshukuru Mungu na kuomba rehema zake kuingia 2021 naomba kuchangia.

Nadhani sio mawaziri "wote" wako like minded na mkulu;
Mathalani Wizara ya viwanda na biashara kwa miaka 5 ya kwanza ni kama ilikosa waziri ndio maana kwa miaka 5 amekuwapo
Mwijage
Kakunda na
Bashungwa, nadhani hawakumsaidia mkulu kwenye kuja na strategy ya viwanda na kukuza biashara ndio maana hakuna aliedumu; hata huyu wa sasa kama atakosa strategy ya kukuza biashara na kuvutia ujenzi wa viwanda bila shaka nae ataondoka.

Wizara ya kilimo nayo imekosa "mwenyewe"
Alianza Mwigulu akaja Tizeba then akamalizia Hasunga, kama wange-deliver nadhani wasingeondoshwa ndio maana sasa tuna waziri mpya.

Nadhani ni mawaziri kushindwa ku-tap nini mkulu anataka na basically mkulu kama haoni deliverable bila shaka mawaziri lazima waondoke.

Mhe. Bashe ni kama anajitahidi ila sasa bado anakosekana strategy ya project investment financing ili CAPEX na OPEX ilete results za haraka.

Unless Waziri wa Fedha/hazina/BOT wakija na right project management investment financing tutatoboa.

Ila wakibakia na policy na sheria za miaka 1997-2003; tutashangaa miaka 5 imepita hamna kilichofanyika.

Mwisho, kama Mawaziri wanakosa vision bila kujali elimu zao; na wakashindwa kupata watu hata kama ni outsiders kwenye gov circles ili PPP strategy iwe executed, tutashangaa miaka 5 imepita.

Lazima wapatikane watu wenye ujasili wa kukaa na mkulu (japo nadhani ugumu upo kwa mkulu kuwa accessible) ili ku-share nae what is most feasible strategy to make things happen kwa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kwa kutumia fedha za ndani na za nje ili ku-drive change.

Kujenga uchumi jumuishi na sustainable ni vita, policy na sheria ziko too visible na kwa hizo hatuwezi kuzitumia pekee kutoboa. Strategy has always been invisible and sometimes covert, ili siku mambo yaki-surface kuna hatua tu kama formality ya execution.

Heri ya mwaka mpya 2021
 
Rais ni binadamu, sioni kama yeye kuwa na hicho kitabu ni tatizo. Muda mwingi anatumia Ofisini, so muda mwingine kusoma vitu vya kujiburudisha baada ya kazi sioni tatizo.
EEEE Bhwanahm anajiburudisha kwa kusoma Kamasutra? Mimi sijui kama ni kweli hicho kitabu kimo ofisini mwake! Nanukuu tu niliyosoma hapa.
 
Kanda ya ziwa ndio mwanzo mwisho hawatapata Rais nchi hii mpaka mwisho wa dunia na mawaziri mtaokoteza kwenye serikali zijazo. 2025 kutakuwa na visasi vya wazi poleni kwa wajayo. Mungu awasaidie
Tukitengeneza uhalisia wa kutotaka viongozi kutoka kanda ya ziwa, tusishangae suala la kuongeza muda likapamba moto.
 
Kabla sijaanza ibaada ya kumshukuru Mungu na kuomba rehema zake kuingia 2021 naomba kuchangia.

Nadhani sio mawaziri "wote" wako like minded na mkulu;
Mathalani Wizara ya viwanda na biashara kwa miaka 5 ya kwanza ni kama ilikosa waziri ndio maana kwa miaka 5 amekuwapo
Mwijage
Kakunda na
Bashungwa, nadhani hawakumsaidia mkulu kwenye kuja na strategy ya viwanda na kukuza biashara ndio maana hakuna aliedumu; hata huyu wa sasa kama atakosa strategy ya kukuza biashara na kuvutia ujenzi wa viwanda bila shaka nae ataondoka.


Lazima wapatikane watu wenye ujasili wa kukaa na mkulu (japo nadhani ugumu upo kwa mkulu kuwa accessible) ili ku-share nae what is most feasible strategy to make things happen kwa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kwa kutumia fedha za ndani na za nje ili ku-drive change.

Heri ya mwaka mpya 2021

..nakubaliana na wewe kwamba Mwijage hakuwa " like minded " na Jpm.

..Mwijage alikuwa analaumiwa kwa kuwa "laini-laini" kwa wenye viwanda. Sina uhakika kama ni Mwijage, au waziri mwingine, aliyeambiwa hadharani na Jpm kwamba anamkwaza.

..Vilevile wizara hiyo imekuwa na mawaziri wanne mpaka ktk miaka mitano. Sasa kama mawaziri wamebadilishwa lakini matokeo sio mazuri, labda ni vizuri tukachunguza kama vision ya Jpm haina mushkel.
 
Huwa nacheka Sana mtu akilinganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa nchi kama Kenya, Rwanda nk, hear wa kwetu ni viumbe tofauti....ni aina nyingine ya wezi kwa mgongo wa biashara..janja janja nyingi, kupendwa kutajirika kwa muda mfupi, nk kumbuka walivyokuwa wametengeneza zengwe la sementi! ndio maana serikali wanatumia njia maaalum kwa ajili ya aina yetu ya wafanyabiashara!
Mleta mada hawa Hawa wafanyabiashara unaoeatetea wakienda nchi nyingine kueekeza huwa wanashindwa na kurudia na mifani tunayo!
Mwongo halafu huna heshima kwa wafanyabiashara. Fuatilia mchango wa sekta binafsi katika pato la serikali yako kisha uwaheshimu pamoja na mapungufu yaliyopo.
 
Rais ni binadamu, sioni kama yeye kuwa na hicho kitabu ni tatizo. Muda mwingi anatumia Ofisini, so muda mwingine kusoma vitu vya kujiburudisha baada ya kazi sioni tatizo.
Je unajua hicho kitabu kinafundisha nini?
 
Tumeandika sana lakini nataka tupate elimu nzuri kwa kutoa mifano halisi ama kinyume na Mkulu au kuunga mkono mkulu.

Yote tutakoyo andika hapa naomba yawe matokeo ya buashara ya uhalisia, naomba wanao fanya biashara zenye references za wazi ndio wawakilishi michango yao hapa ili tuzungumzie uhalisia na sio maneno ya kubumba.

Naamimini Serikali ya Magufuli ndio serikali iliyo nyooka kwa wafanya biashara walionyooka na walipa kodi.
 
Mkuu

Infact jamaa hua hapokei ushauri wa yeyote...

Hizi zote ni fujo za ubongo wake binafsi kabisa

We are in deep shit aisee
NAANDIKA KWA UWAZI ILI KUWA SHAHIDI WA KWELI, NA HUMU NDANI YA MITANDAO WAPO WENYE KUNIFAHAMU VIZURI TANGU MIAKA HIYO MPAKA LEO HII. NA NINASEMA KWA WALIO NYOOKA MAGUFULI NDIO BORA KIBIASHARA KAMA NA WEWE UMENYOOKA.
 
A MFANO HALISI WA KIBIASHARA KABLA NA BAADA YA MH . MAGUFULI:

Mwaka 2006, Wilaya ya Same na Mwanga tuliianzisha biashara ya Nguzo za Umeme na simu.

Tulikata nguzo kama laki 7 hivi , na tuliziuza Keya na ilikuwa kama 65% ya Country wide Electrification project in kenya.

Tulisumbuliwa sana ila mpaka leo naamini waziri aliye kuwa na muono wa kuendesha shuguli za serikali kibiashara alikuwa Mh. Diallo Mwandu ambae mwaka 2006 alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Tulipata taabu sana kupata vibali lakini tuliiulizwa soko lipo? Na bei gani kwa nguzo? Tulimwambia soko la Kenya lilikosa mzalishaji wa nguzo, na soko linahitaji nguzo million 2, na uwezo wetu ni kama nguzo laki 7 mpaka laki 9.

Bei ni 105 USD kwa Jumbo size na USD 95 kwa Standard size au distribution poles.
Alitoa permits zote in less than 1 hour.

Lakini Exports receipts zilipo fikia 67 million USD tulianza kusumbuliwa tena sana.
Permits zilikuwa cancelled na biashara hiyo wakapewa Nyanda za Juu hasa Njombe.
Na kipindi hicho kodi tulilipa, wananchi walilipwa, na gharama zingine za kutayarisha na kuchemsha nguzo tulilipa kikamilifu.

Lakini kitendo cha kuuza 67 million USD kilisumbua sana baadhi ya watendaji, kiasi hatujafahamu kwa nini? Ná walitaka nini?.

Leo hii Serikali ya Mkulu Magufuli unauza Nguzo unavyo weza ili mradi ziwe na ubora, zifike kwa wakati muafaka na ulipe kodi..

Na waliokuwa wanauza nguzo leo wamepata pesa mara 6 ya pesa tulizo pata wakati huo.
Wenye nguzo tunalipwa kwa muda muaafaka na bila kufuatiliwa kiasi gani tumehifadhi Benki na tulichowekeza kwenye miradi mingine baada ya kulipwa na Serikali (Tanesco).

NA RURAL ELECTRIFICATION UMEKWISHA ZAILISHA ZAIDI YA BILLIONAIRES 55 WA TSHS. AU MILLIONAIRES ZAIDI YA 45 WA USD..
 
Kama watanzania wote 84% na wengine bado watakua wanamuhitaji lazima atakua amekua msaada kwao. Yeye ndio ataona afanye nini ili hao watanzania wapate wanachokitaka

Mungu ibariki Tanzania

Madictator wote duniani hujitengenezea mazingira ya kuonekana wanakubalika.
 
Na huu ndio uthibitisho ambao hauwezi kupingwa kwa kuwa ukweli huu umepatikana kutokana na utafiti.

A recent wealth report by Knight Frank shows the tally of Tanzania's super-rich stood at 5,668 at the end of 2019 compared to Kenya's 2,942. This includes 5,553 who are dollar millionaires - worth Sh100 million and above, another 114 billionaires, worth Sh3 billion and above and one that is worth over Sh100 billion.Mar 8, 2020



www.standardmedia.co.ke › article

Kenyans richer but Tanzania home to more millionaires - The
 
Duuh .!!
Bora hata Putin walimkuta na Window XP
Huyu wa kwetu hata kompyuta hajui kutumia
Mzee wa kufotokopi kwa kwenda mbele
Na hili pozi la kuongea na simu kama picha za studio miaka ile




1609453119762.png
 
Maswala ya uchumi duniani kote Yana kanuni zake ..ukitaka kuharibu uchumi basi Anza kupeleka mambo kipolisi polisi. Mara kodi hazieleweki

Mara account zimekuwa freeze za wafanyabiashara.

Mara Kodi mpya hadi za wanaofuga kuku wawili majumbani.

Mara hiki mara kile.

Mazingira yakishaanza tu kuwa 'unpredictable' .. kinachofata watu hukimbia na pesa zao..

Wengine watakaa nazo majumbani wakiona hata Bank hakuna usalama. Wengine wataacha kuanzisha biashara mpya..wakihofia Hali hii ya kutotabirika.

Wengine wata wekezs nchi za nje na nchi jirani.. mwisho WA siku uchumi utaporomoka tu.

Cha kushangaza Tanzania tuliwahi fanya haya makosa Sana wakati wa Nyerere. Why yanajirudia?

Washauri wanafanya kusudi Rais achukiwe apewe lawama?
Majungu hayo, nani ametangaza kodi ya kuku? Msione vinaelea vimeundwa, waliozoea wakati wa rukhsa na mzee wa Msoga zama zao zimepitwa. Nchi inatakiwa isonge mbele hapa Kazi tu! Rais ni taasisi.
 
RAIS HASHAULIKI, na ukimshauri ndiyo anafanya tofauti. Halafu ukimshauri ndiyo mwisho wa kazi yako. Mbona kwenye uchumi na fedha yuko na mtaalamu anayetambuliwa na WB na IMF, huyu Dr Philip Mpango.

Jamaa ameharibu uchumi kwa kuwanyanyasa Sekta Binafsi hususan matajiri wakubwa akina Yusuf Manji, Mo Dewji, Dangote, Ally Mufuruki nk.pamoja na hao wengine ndiyo nchi ingekuwa inakusanya kodi kwa 80% ila sasa wengine wamefunga biashara, wengine wamepunguza uzalishaji na wengine wamekufa.

Matokeo yake sasa Serikali inanza kuhangaika na kodi za sekta isiyo rasmi kama machinga, wafuga kuku na mama ntilie. STUPID
Weka ushahidi? Vinginevyo ni majungu.
 
Mtu anayelala na kuota bila kufikiria athari za ndoto zake kiuchumi ni hatari kwa ustawi wa nchi.

Daraja la Busisi litabeba mahela mengi ila ni useless

Kuhamia Dodoma was a stupid idea
 
Nadhani Magufuli Aendelee kukaza kamba ili mfe.
Ndo mtakuwa na akili.
alafu Leo ndo mwisho wa mwaka[emoji847][emoji847][emoji847].
Tunaingia mwaka wa 1.bado Kama 4 hivii.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
4.10 [emoji25][emoji26]
 
Back
Top Bottom