The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,320
- 117,674
- Thread starter
- #121
Rais mwenyewe anawashauri washauri na kasema hapangiwi.
Nichukue mfano mmoja tu kuelezea jinsi kuwalaumu washauri kunavyoweza kuwa kile waingereza wanachokiita "blaming the victim". Kumlaumu muhanga.
Kuna mshauri mmoja anaitwa Lawrence Mafuru. Alikuwa Msajili Hazina. Moja ya kazi yake ni kumshauri rais mambo ya fedha. Jamaa ni banker mzuri wanamfahamu mpaka London Charter of Bankers.
Magufuli alikuwa anataka hela zote za serikali ziwekwe BOT.Mafuru akamwambia si vibaya, ila zoezi inabidi lifanywe kwa awamu, kwa sababu kuondoa hela zote kwa mpigo kutaharibu mzunguko wa fedha. Huo ulikuwa ushauri mzuri tu kitaalamu.
Tafsiri ya Magufuli ilikuwa kwamba Mafuru anajifanya mjuaji. Mafuru akatolewa kwa style ya "atapangiwa kazi nyingine". Style mbaya sana. Unalipwa mshahara, lakini kazi hufanyi unakuja ofisini kusoma magazeti kila siku.
Sasa hapo washauri wengine wakiona mwenzao kapigwa daflao hivyo kwa kushauri kitaalamu, na wao wanazipenda kazi zao, unafikiri watashauri kitaalamu au watakubali anachotaka Mzee Baba tu?
Sasa kibaya zaidi baada ya kulazimisha mashirika ya umma na taasisi ziende BOT..
Anatolea udenda pesa za NMB na CRDB..
Ndo unaona kinachotokea..
Yaani anajipiga risasi mwenyewe ya mguu halafu anashangaa why hawezi kukimbia..
Mind you wakati taasisi za umma na mashirika ya serikali zinazuiliwa kufanya biashara hata na Nmb na CRDB huku serikali ni mwanahisa huko pia na faida zinawatoa udenda...