In Principle Magufuli ni Rais wetu na tutakuwa nae mpaka November 2025 wakati Rais mwingine atakaechaguliwa 2025 October akichukua kijiti toka kwake.
Tanzania ni nyumbani na kwa wengi wetu hatuna 2nd home country ili kuishi;
John Pombe Magufuli ni mwanadamu kama tulivyo mimi na wewe na njia pekee ya kuishi nae ni kumheshimu kama mwanadamu mwenzetu then kumheshimu pia kwa nafasi yake ya Rais wa JMT ambae pia kikatiba ni mkuu wa nchi na amri jeshi mkuu.
Yet sheria za uwekezaji Tanzania na policy ni zilezile ambazo Mkapa na JK waliziacha. Sanasana TIC kaiweka chini ya OR na kuteua waziri wa uwekezaji ili Tanzania ya kesho iwe bora kuliko leo.
Kuna pahala kwenye biblia Mungu alizungumza na wanadamu kupitia nabii Isaya kwa kumwambia mwanadamu "come and let us reason together"
Njia pekee ya kumshawishi mkulu ni kutafuta platform za dialog kwa staha na kuja na proposed solutions ambazo wananchi watapata na serikali ambayo lengo moja wapo ni kukusanya kodi za kuendeshea nchi nao wapate.
Let us come with facts na tuseme, with time mambo yatabadiika.
Zamani ukifungua biashara, hata kupata TIN bila kishoka au kutoa kitu kidogo TIN ulikuwa haupati kirahisi hata kama ni TIN kwa ajili ya leseni au kadi ya gari. Leo unaingia online website ya TRA inapata TIN.
Hebu tujenge hoja, namna gani tufanye ili serikali ipate na wananchi wapate kwa kujenga uchumi jumuishi na endelevu. Kuna wakati wafanya biashara wa madini walilalamikia kodi na tozo chungu mzima kwenye mfumo wa biashara ya dhahabu, kwa sasa uwazi, usalama na uhakika wa kuuza dhahabu ni mkubwa kwa mchimbaji, broker na dealer hali kadhalika.
kwa upande mwingine, serikali ije na strategic investment models kwa hii miaka 5 ya mwisho ili kuvutia mitaji toka nje kwa kutumia local guarantee.
Mathalani, kuna Mtanzania mwenzetu namfahamu, alipata fursa ya kupata mkopo wa machine/equipments za kuzalisha viwatilifu (agro-inputs) vya mashambani. Ofcourse hakuna na fedha ya kununua machine/equiments, ila ana akili ya kuweza kushawishi kupata mkopo. Soko la viwatilifu Tanzania lipo na ni la hakika iwe kwa ajili ya pamba, chai, tumbaku, kahawa na kila mwaka tuna import.
Kwenye model kama hii, hutu mtu na kampuni yake wanahitaji dhamani toka hazina, wizara ya kilimo (TPRI) kumhakikishia soko na signature ya mwanasheria. Fedha zinalipwa toka banks za nje ili machine na equipment zije, then kwa kuzalisha ndani tuna-cut down imports ya viwatilifu, vijana wanapata ajira, serikali inapata tozo na kodi tokana na uendeshaji wa kiwanda, huenda mkulima akanunua bei nafuu agro-inputs kwa kuwa uzalishaji wa ndani unapunguza costs za usafirishaji kama ni toka india, China au Egypt.
In less than 4 years mkopo ulikuwa unarejeshwa na mzunguko wa ndani unaongezeka. Fedha za kujenga majego waliokuwa wanafanya NSSF na PPF au LAPF kwa sasa PSSSF zingeweza kukopeshwa kwa wekezaji kama huyu jamaa ninaemfahamu na NSSF pia anakua na hakika ya kuongeza wanachama ambao watakuwa wanafanya kazi kwenye hii industry.
That is being smart.
Ila honestly, enzi za JK kulikuwa na watu wa kati wakisikia ua good investment proposal walikuwaga wanaipiga juu kwa juu baada ya kupata blue print.
Kwa sasa ni ngumu kumpata Mkulu ila kama kuna wasaidizi wake wana open mind, uwekezaji wa sasa duniani hautegemei sana cash in hand au bank aliyonayo mwekezaji but rather mahitaji ya soko.
Tunapoingia 2021, let us reduce complains, ila tuje na mada za kujadili na kukosoana kwa what can be done ili tuwe bora zaidi na Tanzania isonge mbele.
Hakunaga single model iliyo sawa 100% kwenye uwekezaji.
Hata katani ambayo ililetwa Tanzania toka Mexico iliingia kwa njia haramu (sisal seedilings was was smuggled) ila baadae katani ikawa na mchango mkubwa kwenye kujenga uchumi wa Tanganyika chini ya Ujerumani, Mwingereza na baadae Tanzania.
Kama kitengo cha TIC wangekuwa na akili za kutafuta new idea, new projects na kufanya kila tuwezalo tuwekeze kama namna wahalifu wanavyosakwa na polisi, TCRA, Financial Intelligrnce Unit, PCCB; tungekuwa na chombo cha ku-extract nini kifanyake na kwa kasi kiasi gani, bila shaka 2021 na kuendelea tungefanya vema zaidi.
Heri ya mwaka mpya 2021 wakubwa