Rais Magufuli anaingizwa 'mkenge' na washauri?

Nadhani hujaielewa vyema concept yangu.

Mwenye wajibu huo yupo lakini nachoona hapa ni kuwa haufanyi ipaswavyo.
 

Hili limeshaanza kutokea
 
Wabongo sisi Ni shida...
Asipopokea ushauri tunakasirika na akipokea ushauri anaingizwa mkenge. Daah!
 
Asipopokea ushauri tunakasirika na akipokea ushauri anatiwa mkenge. Daah!

Yes, he is between a rock and a hard place!!! Haya mapungufu ni matokeo ya kuokota washauri toka majalalani. Jiwe chagua wasomi wanaojiamini na kujitambua ambao hawana njaa kama washauri wako huwezi kuyumba.! Usiogope umri, jifunze toka kwa Obama aliyezungukwa na washauri vijana na wazee kuliko yeye na akanufaika na busara zao. Diversity gives you a winning mix.
 
Ju

Jiwe haambiliki kila kitu anafanya mwenyewe kwa kutumia akili yake
Ukimshauri utakua matatani Ndio maana hata ofisi yake ipo shaghalabaghala
Rais anakitabu cha kama sutra ofisini shida tupu
Rais ni binadamu, sioni kama yeye kuwa na hicho kitabu ni tatizo. Muda mwingi anatumia Ofisini, so muda mwingine kusoma vitu vya kujiburudisha baada ya kazi sioni tatizo.
 
Menyrere alikuwa na akili za kimasikini
 
Kuna mtu anaona Sawa kuanza kuweka Kodi Kwa wafuga kuku
Hajui kinachofata ni kuku kupanda bei
Hata hivi vifurushi vya mtandao vimepanda sababu ya kodi ila Waziri wa Mawasiliano eti juzi anawaagiza TIGO, VODACOM, AIRTEL na Hlotel wateremshe ndani ya miezi 3. INSANE
 
Kanda ya ziwa ndio mwanzo mwisho hawatapata Rais nchi hii mpaka mwisho wa dunia na mawaziri mtaokoteza kwenye serikali zijazo. 2025 kutakuwa na visasi vya wazi poleni kwa wajayo. Mungu awasaidie
 

..mimi kwa uelewa wangu ni kwamba Raisi au kiongozi yeyote huwa ana AGENDA / VISION anayotaka kuitekeleza.

..Na agenda / vision hiyo hutokana na mambo mengi ikiwemo experience ktk makuzi na maisha, exposure, na elimu, ya Raisi au Kiongozi.

..kiongozi / Raisi anapochaguliwa na kuingia madarakani hutafuta watu ambao anaamini ni sahihi kumsaidia kutekeleza agenda / vision yake.

..kwa uelewa wangu kiongozi / Raisi huchagua watu " like minded " au wenye mitizamo kama ya kwake ili kumsaidia kuendesha serikali na nchi.

..tukirudi kwa Jpm, Watanzania tunapaswa kuelewa kwamba wateule wake ni watu ambao wako " like minded " au wana mitizamo kama ya aliyewateua.

..Wateule wa Jpm wanapofanya maamuzi na wasipochukuliwa hatua au hata kuonywa hadharani basi tukubali kwamba maamuzi hayo yana baraka za Jpm / aliyewateua.

..Kwa maoni yangu, ni makosa kuamini kwamba Jpm anaingizwa mkenge na wasaidizi ua washauri wake. Raisi na timu yake ni watu ambao wana mitizamo inayofanana, na wanatekeleza mambo ambayo wanaamini[ kutokana na experience, exposure, kujifunza] yanafaida kwa taifa.

Nani au Chombo gani kinapaswa kumrekebisha Raisi na Wasaidizi / Washauri wake?

..Kwa maoni yangu wanaotakiwa kumrekebisha Raisi na Serikali ni BUNGE. Hao ndio waliopewa dhamana kikatiba kufanya kazi ya kuisimamia na kuirekebisha serikali.

..Zaidi ya bunge, wananchi kupitia asasi mbalimbali, pamoja na vyombo vya habari, wanajukumu la kuisimamia, kuikosoa, na kuirekebisha, serikali iliyoko madarakani.

CC Gwakukahja
 
P
 
Naunga mkono hoja.
P
 
Nadhani hujaielewa vyema concept yangu.

Mwenye wajibu huo yupo lakini nachoona hapa ni kuwa haufanyi ipaswavyo.
Sasa unatafuta wa kumlaumu, na kumwacha mhusika mwenyewe.

Hii ni kawaida kwa mtu aliyepotoshwa na mahaba mengi kupita kiasi kwa mtu anayempenda sana. Wengine wataona 'chongo, yeye anasema hayo ni makengeza tu!
 
Mbona yeye mwenyewe ameshasema ukimshauri ndio unaharibu kabisa, hivyo hakuna anaemshauri
 
..Kwa maoni yangu wanaotakiwa kumrekebisha Raisi na Serikali ni BUNGE. Hao ndio waliopewa dhamana kikatiba kufanya kazi ya kuisimamia na kuirekebisha serikali.
Na kama Bunge ni mali yake..., kwa maana kwamba wabunge wote wamepatikana kutokana na ufadhiri wake?

Je, Chama chake hakina nafasi ya kumkanya na kumshauri... Je, na kama ngazi zote za uongozi katika chama na wote wanaoziongoza wanamtegemea yeye kwa nafasi walizonazo, wataanzia wapi kumkanya au hata kumshauri?

Rais akiwa amechukua madaraka yote na kutumia 'dola' kuhakikisha kwamba matakwa yake yanatekelezwa, kuna mtu gani anayeweza kuwa na ujasiri wa kushauri na kukanya, hasa kama unajua tabia ya muhusika haina uvumilivu katika mambo hayo?
 
Mkuu hana washauri huyo. Yeye kwa kuwa ana hiyo Phd yake UCHWARA anadhani anajua kila kitu duniani. Kumbuka alipoingia tu AKAKURUPUKA na kutaka taasisi zote za Serikali Nchini zihamishe fedha zao kutoka bank accounts kwenye benki za biashara na kupeleka BoT na hivyo kusababisha matatizo makubwa sana ya liquidity Nchini hadi bank kushindwa kutoa mikopo.

Je, aliomba ushauri kwa wataalamu wa mambo ya pesa na uchumi? Hapana ALIKURUPUKA tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…