Uchaguzi 2020 Rais Magufuli anaomba kuongeza mkataba wa kazi na Tundu Lissu anaomba kazi kwa upya, ipo tofauti hapo

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli anaomba kuongeza mkataba wa kazi na Tundu Lissu anaomba kazi kwa upya, ipo tofauti hapo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli kuomba kuongeza mkataba wa kazi ni tofauti na kuomba kazi kwa mara ya kwanza.

Rais Magufuli ana sifa nyingi za ziada katika kinyang'anyiro cha urais ukilinganisha na washindani wake akina Lissu nk.

Dr Magufuli anazungumza habari ya "nimefanya" wakati Tundu Lissu anazungumza habari ya "nitafanya"

Dr Magufuli anazungumza kwa kutuonyesha ushuhuda na mifano lakini Tundu Lissu anazungumza kinadharia zaidi na hata tukienda pale Ufipa hatuoni mifano hata midogo midogi ya matumizi bora ya ruzuku.

Nitaendelea...

Maendeleo hayana vyama!
 
Kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli ni miundombinu,yaani reli, barabara, na ndege, barabara za juu licha ya hayo bado watu hali yetu ni mbaya kiuchumi tuna njaa hatuna pesa, mishahara hafifu mzee ana shangaa yote niliyowafanyia bado hawana shukurani anasahau kuwa ni maendeleo ya vitu na si watu.
 
Mimi sina chama ila nikiangalia Ccm inapendwa sana na Magufuli anapendwa sana

Ninaona dalili kuwa CCM itashinda sana
Uungwana ni pamoja na kuheshimu mawazo ya mwingine hata kama hukubaliani nayo na isilete chuki baina yenu.

Mh. Rais amefanya aliyojaaliwa kuyafanya na yeye ni binadamu kama wengine na anazo sifa za kibinadamu.
 
yan mim ni jembe ni jembe jongwe.ila kila nikiend Ufipa yan nakata tamaa kwa kweli
 
Kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli ni miundombinu,yaani reli, barabara, na ndege, barabara za juu licha ya hayo bado watu hali yetu ni mbaya kiuchumi tuna njaa hatuna pesa, mishahara hafifu mzee ana shangaa yote niliyo wafanyia bado hawana shukurani ana sahau kua ni maendeleo ya vitu na si watu.
Maendeleo ya mtu yanapatikana darasani.

Elimu ya chini bure.

Elimu ya juu mikopo kibao.....unataka nini tena manka?!
 
Kiukweli kuomba kuongeza mkataba wa kazi ni tofauti na kuomba kazi kwa mara ya kwanza.

Rais Magufuli ana sifa nyingi za ziada katika kinyang'anyiro cha urais ukilinganisha na washindani wake akina Lissu nk.

Dr Magufuli anazungumza habari ya "nimefanya" wakati Tundu Lissu anazungumza habari ya "nitafanya"

Dr Magufuli anazungumza kwa kutuonyesha ushuhuda na mifano lakini Tundu Lissu anazungumza kinadharis zaidi na hata tukienda pale Ufipa hatuoni mifano hata midogo midogi ya matumizi bora ya ruzuku.

Nitaendelea...

Maendeleo hayana vyama!

Ni wazi, huyu ameshapewa mamlaka na madaraka, huyu mwingine hajapewa! Aliyekwishapewa, atasema aMEfanya na ambaye hajapewa atasema nitafanya.

Hata hivyo kuna ambayo huyu ambaye hajapewa amefanya, hasa yale yaliyo ndani ya uwezo wake na taaluma yake. Ni kukosa busara kama tutasema Lisu hajajenga barabara, hivyo hafai. Lakini Magufuli kama hajajenga tutamlaumu.

Suala la ufipa sikulielewa vizuri, ila kama ni udogo wa ofisi, ni kweli ni ndogo na labda hailingani na hadhi ya chama, lakini hizo za CCM zilijengwaje? Una historia ya ujenzi wa ofisi ya CCM Dodoma? Fedha zilitoka wapi!
 
Ni kweli kuna tofauti kubwa saana
Nimefanya
Nitafanya
Nimetengeneza
Nitatengeneza
nakadhalika

Lakini ieleweke nimefanya au nitafanya ni tafauti kweli lakini umefanya nini? au atafanya nini?
Yawezekana uliofanya yakawa ni maumivu au atafanya yakawa ni matibabu
 
Kila mmoja kati ya "mitano tena" na mitano kwanza ana advantages na disadvantages

Mitano tena kweli kafanya na anayo ya kuonyesha kwa hiyo atapimwa kwa kigezo cha aliyoyafanya kayafanya sawa? Yanatosha kulingalisha na "rasilimali na nyezo alizokabidhiwa kama dhamana? Amekidhi matarajio ya Watanzania kuleta umoja, udugu na mshikamano? Amefuata katiba aliyoapishwa kuilinda na sheria zake?

Mitano kwanza yeye ana ainisha makosa na mapungufu ya mwenzake. Je mapungufu hayo ni makubwa kiasi cha kufanya wananchi wamuelewe kua mitano tena hafai kuongezewa?

Yote kwa yote mitano tena ana kitu wanachoita incumbency advantage na mitano kwanza ana imani na huruma ya watu
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Katika vitu ambavyo jiwe amefanikiwa kuvifanya nchi hii ni kuiharibu nchi, Jiwe hafai hata kuwa kiongozi wa familia.
 
Kwani mwaka 2015 tulipomchagua alikuwa ameshatekeleza mambo yapi?? Mwajiri anaweza kukuongezea mkataba au kuusitisha kulingana na jinsi ulivyoutumikia sambamba na kutimiza malengo ya taasis.
Tulimpa mkataba ili atutumikie kama wananchi tupande maendeleo halisi ya wananchi, yeye kaendeleza vitu! Yupo tayari akajenge flyover watumishi na familia zao walale na njaa, watoto waache shule, watumishi wakaishi nyumba za kupanga! Je kuna sheria gani inamlazimisha kujenga flyover??? Lakini haki na stahiki za hawa watumishi mbona zipo kisheria? Kwanini anacha kutimiza mabo ambayo yapo kisheria anakimbilia vitu ambavyo halamishwi na sheria??? Miaka mitano kabomolea watu nyumba bila fidia, tena kukiwa na zuio la mahakama, je huyu bado tumpe mkataba mwingine??? Tangu yeye mwenyewe akiwa waziri wa uvuvi serikali imekuwa ikawachomea nyavu wavuvi kwa madai ya uvuvi haramu, je mpaka sasa bado hajaona namna ya kuwakwamua hawa wavuvi ili waweze kupata vibali. na hapa bado tumpe miaka mingine 5 ??? Tangu tupate uhuru wa nchi yetu tulitangaza kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu, lakini mpaka leo soko la mazao limekuwa ni lakubahatisha, hakuna njia wala mbinu mbadala iliyobuniwa na serikali hadi sasa, wakulima wanakopwa mazo yao wanabaki kusotea malipo! Je bado tuumpe mkataba mwingine!???
Hapana , nazani hapa ni bora tukampa kazi mtu mpya aliyeonyesha maona na mtazamo mpya wa kutuvusha tulipo kwama!
 
Sisi body ya wadhamini tumeamua hatutaongeza mkataba wa huyu mkurugenzi anaemaliza muda wake kwani kwa miaka mitano hatujapata divident yoyote zaidi ya kutuambia anajenga miundombinu ya kiwanda chetu

Hivyo tunamtaka ajiandae kukabidhi office mapema mwishoni mwa mwezi huu pale mkataba wake utakapo koma

Hatutaki ujinga kabisa kwani kazi tuliyompa imemshinda.
 
Kazi gani iliyomshinda?
 
Back
Top Bottom