Uchaguzi 2020 Rais Magufuli anaomba kuongeza mkataba wa kazi na Tundu Lissu anaomba kazi kwa upya, ipo tofauti hapo

hiv wewe umewah kuwa kiobgoz? ongoza kata tu ujue kaam uongoz ni kazi ngunu jinha
 
Sisi wananchi tunimani na JPM tushaamua tunampa kura zetu kisha tunaenda nyumbani kusherehekea ushindi.
 
Binafsi sijaona alichokifanya zaidi ya kudominate media ili kujitangaza. Tangu aingie madarakan Kila kada Hali ya kimaisha imekuwa mbaya. Mazao hayana Bei mfano mbaazi kutoka kilo 3000/- mwaka 2012 mpaka Sasa ni 400/ mwaka 2020. Vifaa vya ujenzi mwaka2015 50kg za cement ni 14500/- mwaka huu wa 2020 50kg imefiki 20,000/-tsh. Awamu ya Magufuli vifaa vya ujenzi Bei juu. Watumishi Ndiyo kada aliyoitelekeza kwa miaka mitano. Hakuna nyongeza ambayo kisheria lakin yeye kagoma. Hakuna kupanda daraja japo ipo kisheria. Hapo ujue uniambie CCM inapendwa. Uongo kamwe haiwezi pendwa wala kuchaguliwa labda waibe kura.
 
Kwani mwaka 2015 tulipomchagua alikuwa ameshatekeleza mambo yapi?? Mwajiri anaweza kukuongezea mkataba au kuusitisha kulingana na jinsi ulivyoutumikia sambamba na kutimiza malengo ya taasis.
Tulimpa mkataba ili atutumikie kama wananchi tupande maendeleo halisi ya wananchi, yeye kaendeleza vitu! Yupo tayari akajenge flyover watumishi na familia zao walale na njaa, watoto waache shule, watumishi wakaishi nyumba za kupanga! Je kuna sheria gani inamlazimisha kujenga flyover??? Lakini haki na stahiki za hawa watumishi mbona zipo kisheria? Kwanini anacha kutimiza mabo ambayo yapo kisheria anakimbilia vitu ambavyo halamishwi na sheria??? Miaka mitano kabomolea watu nyumba bila fidia, tena kukiwa na zuio la mahakama, je huyu bado tumpe mkataba mwingine??? Tangu yeye mwenyewe akiwa waziri wa uvuvi serikali imekuwa ikawachomea nyavu wavuvi kwa madai ya uvuvi haramu, je mpaka sasa bado hajaona namna ya kuwakwamua hawa wavuvi ili waweze kupata vibali. na hapa bado tumpe miaka mingine 5 ??? Tangu tupate uhuru wa nchi yetu tulitangaza kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu, lakini mpaka leo soko la mazao limekuwa ni lakubahatisha, hakuna njia wala mbinu mbadala iliyobuniwa na serikali hadi sasa, wakulima wanakopwa mazo yao wanabaki kusotea malipo! Je bado tuumpe mkataba mwingine!???
Hapana , nazani hapa ni bora tukampa kazi mtu mpya aliyeonyesha maona na mtazamo mpya wa kutuvusha tulipo kwama!
Nakuunga mkono 100%
 
Sisi wananchi tunimani na JPM tushaamua tunampa kura zetu kisha tunaenda nyumbani kusherehekea ushindi.
Jisemee nafsi yako usituchanganye sisi wenye akali zetu timamu.Mimi na familia yangu jamaa zangu na watumishi wenzangu tutampigia kura TUNDU LISU.
 
Kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli ni miundombinu,yaani reli, barabara, na ndege, barabara za juu licha ya hayo bado watu hali yetu ni mbaya kiuchumi tuna njaa hatuna pesa, mishahara hafifu mzee ana shangaa yote niliyo wafanyia bado hawana shukurani ana sahau kua ni maendeleo ya vitu na si watu.
Kuna mwalimu wa sekondari nilimuuliza kuwa serikali zilizopita zilikuwa na utaratibu gani wa kuongeza mishahara na kwa asilimia ngapi/shilingi ngapi ?alinijibu unadhani basi ni hela 10,000/= au inazidi kidogo ila kila baada ya miaka mitatu ndio utaona imeongezeka.Akasema sijui hizi kelele za mishahara zinakuwaje ajenda tena kodi tumepunguziwa ,Magufuli na serikali yake wakaliona hilo kwakupunguza kodi ambayo ilikiwa ni mzigo pia kwa wafanyakazi hivyo 270,000/= hakuna kodi 1,000,000/= kodi ni 105,000/= hata mimi nilipongeza kwa kodi niliyokuwa nakatwa ilikuwa ni maumivu ila sasa kuna kaunafuu .Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni serikali hii imejitahidi sana.Nikamlima swali vipi hapo shuleni kwenu mtampa nani kura wakasema hapo kuna makada wa Ccm wengi tutampa Magufuli nikasema hongereni na leo umeniambia kitu nilichokuwa sijui kuhusu mishahara kumbe nyongeza ilikuwa ndogo.

Mimi niko hapa mkisema maendeleo ya vitu sijui mnamaanisha nini hivi mfano ukinunua sofa ukaweka sebuleni sofa itakuingizia pesa na ukisikia jirani anasema huyu anafanya maendeleo ya vitu ni mjinga ila ni kweli maendeleo ya vitu lakini mbona tunanunua ! Basi ndivyo ilivyo kama mnavyopenda kununua vitu vya ndani na magari na kujenga nyumba mtambue ni maendeleo ya vitu kwa ajili ya watu,madarajaa ,reli ndege ,Meli ,umeme ni kwa ajili ya watu .
Chagua Magufuli Kazi Iendelee.
 
Jisemee nafsi yako usituchanganye sisi wenye akali zetu timamu.Mimi na familia yangu jamaa zangu na watumishi wenzangu tutampigia kura TUNDU LISU.
Wewe na jamaa zako na familia yako ni wachache sana,ila sisi wanchi ni wengi.
Tukutane tar 28 October sisi wananchi tatampa kura za"Ndio"JPM.[[emoji818]]
 
Kiukweli kuomba kuongeza mkataba wa kazi ni tofauti na kuomba kazi kwa mara ya kwanza.

Rais Magufuli ana sifa nyingi za ziada katika kinyang'anyiro cha urais ukilinganisha na washindani wake akina Lissu nk.

Dr Magufuli anazungumza habari ya "nimefanya" wakati Tundu Lissu anazungumza habari ya "nitafanya"

Dr Magufuli anazungumza kwa kutuonyesha ushuhuda na mifano lakini Tundu Lissu anazungumza kinadharis zaidi na hata tukienda pale Ufipa hatuoni mifano hata midogo midogi ya matumizi bora ya ruzuku.

Nitaendelea...

Maendeleo hayana vyama!
Yote fanya ila hil nikiboko
1 uhuru . Haki na maendeleo yawatu
Sio unakuja kwamuda mfupi ujui watuwameangaika miaka mingapi unabomoa nyumbazao .unachoma nyavu nakuteka mali zawavuvi.unafukuza vyeti feki ambaowamekuzalishia wataalam uajiri wako wakusuasua upandishi mishahara wala madaraja
Utegemee kuchaguliwa kwa kujenga uwanja chato.flyover.rell.mandege.tutakula hivyo unatengeneza sisi tuwe nanjaa tumainiletu lisu kwasasa ni yeye
 
Kuna mwalimu wa sekondari nilimuuliza kuwa serikali zilizopita zilikuwa na utaratibu gani wa kuongeza mishahara na kwa asilimia ngapi/shilingi ngapi ?alinijibu unadhani basi ni hela 10,000/= au inazidi kidogo ila kila baada ya miaka mitatu ndio utaona imeongezeka.Akasema sijui hizi kelele za mishahara zinakuwaje ajenda tena kodi tumepunguziwa ,Magufuli na serikali yake wakaliona hilo kwakupunguza kodi ambayo ilikiwa ni mzigo pia kwa wafanyakazi hivyo 270,000/= hakuna kodi 1,000,000/= kodi ni 105,000/= hata mimi nilipongeza kwa kodi niliyokuwa nakatwa ilikuwa ni maumivu ila sasa kuna kaunafuu .Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni serikali hii imejitahidi sana.Nikamlima swali vipi hapo shuleni kwenu mtampa nani kura wakasema hapo kuna makada wa Ccm wengi tutampa Magufuli nikasema hongereni na leo umeniambia kitu nilichokuwa sijui kuhusu mishahara kumbe nyongeza ilikuwa ndogo.

Mimi niko hapa mkisema maendeleo ya vitu sijui mnamaanisha nini hivi mfano ukinunua sofa ukaweka sebuleni sofa itakuingizia pesa na ukisikia jirani anasema huyu anafanya maendeleo ya vitu ni mjinga ila ni kweli maendeleo ya vitu lakini mbona tunanunua ! Basi ndivyo ilivyo kama mnavyopenda kununua vitu vya ndani na magari na kujenga nyumba mtambue ni maendeleo ya vitu kwa ajili ya watu,madarajaa ,reli ndege ,Meli ,umeme ni kwa ajili ya watu .
Chagua Magufuli Kazi Iendelee.
Acha kudanganya watu nyongeza ya Kila mwaka wakati wa JK ni Kati ya 60 elfu mpaka 120elfu. JK ndani ya miaka 3 ya utumishi wa ndugu yangu alipata nyongeza ya zaidi ya laki mbili hiyo ni nje na kupandishwa daraja lakini miaka mitano ya Jpm amepata nyongeza ya elfu kumi tu na hajapanda daraja Sasa Ana miaka 7.
 
Naunga mkono hoja
 
Umeshajichanganya hajapandishwa miaka 7 then unamsifia Jk mbona hakumpandisha ,alikuambia hiyo 60 elfu ni asilimia ngapi ya mshahara wake.
 
Kiukweli kuomba kuongeza mkataba wa kazi ni tofauti na kuomba kazi kwa mara ya kwanza.

Rais Magufuli ana sifa nyingi za ziada katika kinyang'anyiro cha urais ukilinganisha na washindani wake akina Lissu nk.

Dr Magufuli anazungumza habari ya "nimefanya" wakati Tundu Lissu anazungumza habari ya "nitafanya"

Dr Magufuli anazungumza kwa kutuonyesha ushuhuda na mifano lakini Tundu Lissu anazungumza kinadharia zaidi na hata tukienda pale Ufipa hatuoni mifano hata midogo midogi ya matumizi bora ya ruzuku.

Nitaendelea...

Maendeleo hayana vyama!

Ulikuwa una lengo la kutuma hii Habari hapa jf au umekosea?
 
Kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli ni miundombinu,yaani reli, barabara, na ndege, barabara za juu licha ya hayo bado watu hali yetu ni mbaya kiuchumi tuna njaa hatuna pesa, mishahara hafifu mzee ana shangaa yote niliyowafanyia bado hawana shukurani anasahau kuwa ni maendeleo ya vitu na si watu.

Copy and paste na Ethiopia
 
Mimi sina chama ila nikiangalia CCM inapendwa sana na Magufuli anapendwa sana

Ninaona dalili kuwa CCM itashinda sana
Nasikia Meko anatukana tu wale wenye tume yao maana wamepigwa chenga ya mwili na walimuhakikishia mwamba atanasa kwenye mtego. Sa sijui itakuwaje! Patamu hapo!
 
Maendeleo ya mtu yanapatikana darasani.

Elimu ya chini bure.

Elimu ya juu mikopo kibao.....unataka nini tena manka?!

Dah!! ,sawa Mkuu.
2537449_IMG_20200925_113059.jpg
 
Umeshajichanganya hajapandishwa miaka 7 then unamsifia Jk mbona hakumpandisha ,alikuambia hiyo 60 elfu ni asilimia ngapi ya mshahara wake.
Tatizo uelewa wako ni mdogo Sana. Mtumishi wa uma anapanda cheo/ daraja Kila baada ya miaka mitatu. Sasa kwa Mara ya mwisho mtumishi aliyepanda cheo 2013 anatakiwa apande Tena lini? JK angeaweza kumpandisha huyo 2016? Bila shaka haiwezekani. Lakini Jpm alipoingia tu Kuna waliobakisha mwaka moja kupanda lakin hajapasha so ikafika Kuna miaka 7 Kuna miaka 6 Kuna 5 Kuna 4 wote Bila Bila. Hiyo ya % najua huelewi chochote Cha msingi ni kwamba package inayoongezwa ni kubwa na ni Kila mwaka imagine mtu alianza kazi na mshahara 532,000/- hapo ni 2013 mpaka kufikia 2015 nyongeza imemfikishia 716,000/. lakin kwa Jpm ndani miaka 5 kutoka 716,00/ mpaka 733,000/ miaka 5 ameongeza only 17000/ very big shame. Now make comparison btn them.
 
Back
Top Bottom