johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mimi pia sina chama ila nikiangalia Lissu anavyokubalika na sera zake hadi CCM wanadandia hoja zake basi naamini Lissu atashinda mapema labda CCM na tume waibe kura.Mimi sina chama ila nikiangalia CCM inapendwa sana na Magufuli anapendwa sana
Ninaona dalili kuwa CCM itashinda sana
Uungwana ni pamoja na kuheshimu mawazo ya mwingine hata kama hukubaliani nayo na isilete chuki baina yenu.Mimi sina chama ila nikiangalia Ccm inapendwa sana na Magufuli anapendwa sana
Ninaona dalili kuwa CCM itashinda sana
Uungwana ni pamoja na kuheshimu mawazo ya mwingine hata kama hukubaliani nayo na isilete chuki baina yenu.
Mh. Rais amefanya aliyojaaliwa kuyafanya na yeye ni binadamu kama wengine na anazo sifa za kibinadamu.
Maendeleo ya mtu yanapatikana darasani.Kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli ni miundombinu,yaani reli, barabara, na ndege, barabara za juu licha ya hayo bado watu hali yetu ni mbaya kiuchumi tuna njaa hatuna pesa, mishahara hafifu mzee ana shangaa yote niliyo wafanyia bado hawana shukurani ana sahau kua ni maendeleo ya vitu na si watu.
Kiukweli kuomba kuongeza mkataba wa kazi ni tofauti na kuomba kazi kwa mara ya kwanza.
Rais Magufuli ana sifa nyingi za ziada katika kinyang'anyiro cha urais ukilinganisha na washindani wake akina Lissu nk.
Dr Magufuli anazungumza habari ya "nimefanya" wakati Tundu Lissu anazungumza habari ya "nitafanya"
Dr Magufuli anazungumza kwa kutuonyesha ushuhuda na mifano lakini Tundu Lissu anazungumza kinadharis zaidi na hata tukienda pale Ufipa hatuoni mifano hata midogo midogi ya matumizi bora ya ruzuku.
Nitaendelea...
Maendeleo hayana vyama!
Ni kweli kuna tofauti kubwa saana
Nimefanya
Nitafanya
Nimetengeneza
Nitatengeneza
nakadhalika
Nimekuelewa bwashee!Kila mmoja kati ya "mitano tena" na mitano kwanza ana advantages na disadvantages
Mitano tena kweli kafanya na anayo ya kuonyesha kwa hiyo atapimwa kwa kigezo cha aliyoyafanya kayafanya sawa? Yanatosha kulingalisha na "rasilimali na nyezo alizokabidhiwa kama dhamana? Amekidhi matarajio ya Watanzania kuleta umoja, udugu na mshikamano? Amefuata katiba aliyoapishwa kuilinda na sheria zake?
Mitano kwanza yeye ana ainisha makosa na mapungufu ya mwenzake. Je mapungufu hayo ni makubwa kiasi cha kufanya wananchi wamuelewe kua mitano tena hafai kuongezewa?
Yote kwa yote mitano tena ana kitu wanachoita incumbency advantage na mitano kwanza ana imani na huruma ya watu
Kazi gani iliyomshinda?Sisi body ya wadhamini tumeamua hatutaongeza mkataba wa huyu mkurugenzi anaemaliza muda wake kwani kwa miaka mitano hatujapata divident yoyote zaidi ya kutuambia anajenga miundombinu ya kiwanda chetu
Hivyo tunamtaka ajiandae kukabidhi office mapema mwishoni mwa mwezi huu pale mkataba wake utakapo koma
Hatutaki ujinga kabisa kwani kazi tuliyompa imemshinda.