Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Kama kweli wewe ni mwana CHADEMA na unakipenda chama chako, then, huna option maana Mbowe ndiye mwenyekiti wako, ni lazima ufanye naye kazi tu...!

Katika demokrasia, kanuni ya "wengi wape" na "wachache waheshimiwe" ndiyo inayofanya kazi. Sijui kama unalijua hili...

Ukitaka kubadilisha mambo kwenye taasisi yoyote, huwezi kufanya hivyo kwa kukaa sehemu na ku - violate taratibu na kanuni za kuiongoza taasisi hiyo kwa kutofuata utaratibu....

Ukitaka ubadilishe mfumo fulani wa kitaasisi ikiwemo hili la namna ya kupata viongozi na muda wao wa kukaa madarakani, fuata taratibu za kikatiba. INAWEZEKANA....

Nina hakika Ndugu, Freeman A. Mbowe hakujiweka kwenye hiyo nafasi ya Unyekiti....

Amechaguliwa na wengi kwa miaka yote unayoweza kuihesabu na kwa utaratibu wenu wa kikatiba mliojiwekea wenyewe....

Kama yeye mwenyewe Mbowe alitaka aendelee na kufanikwa kushawishi watu, nao wakashawishika na kukubali kumchagua tena na tena, kosa lake ni nini? Je, ni kwa sababu wewe humpendi?

Hilo ni tatizo lako binafsi zaidi...!!

Hata hivyo, ulikuwa na nafasi ya kukutana naye na kumshawishi haya uyasemayo kwa kumwambia;

".........Bwana Mbowe, uzuri wako ni wa miaka 10 tu ama ikizidi ni 15. Kwa sasa huna uzuri tena, huna mbinu, huna mikakati, kaa pembeni mwachie mtu mwingine........"

Lakini hukufanya hivyo.....!!

Na kama ulifanya, basi maana yake ushawishi wako ulikuwa dhaifu na kukataliwa....

Uungwana ni kukubaliana na kushindwa maana asiyekubali kushindwa si mshindani. Huyo ni mtaka fujo na mtafuta maneno tu....!!

Kwa hiyo, inawezekana wewe ulikuwa katika kambi ya "MBOWE ASIENDELEE KWA ZAIDI YA MIAKA 10 AU 15" kama ulivyosema katika andiko lako orijino....

Lakini, kambi ya wenzenu walioona anafaa aendelee zaidi ya muda huo ILIWASHINDA na hivyo Mr Mbowe kuwa mwenyekiti wako...

Kisiasa hapo ndipo tunasema "WENGI WAPE" na kubaliana na maamuzi ya wengi.....

Kuendeleza malumbano kama hayo huku ukiwa ndani ya chama kwa vyovyote vile hii inakuwa siyo saw a na hii inaitwa "uasi ndani ya chama" na siku zote tabia hizi zina adhabu yake KISHERIA na KIKANUNI ndani ya taasisi yoyote.....

Ndani ya chama kama CCM hususani huwezi kuona mwanachama akipinga maamuzi ya chama halali na yaliyofuata taratibu zote kikatiba halafu akabaki salama....

Kisiasa na kistaarabu, mtu anapokuwa hajakubaliana na maamuzi ya kitaasisi, ili awe huru kusema na kukosoa, hutoka ndani ya taasisi hiyo ili asemee nje huko....

Vivyo hivyo wewe, kama hukubaliani na maamuzi halali ya kikatiba ya chama, ondoka ndani ya chama hicho kisha tafuta kinachoweza kukidhi mahitaji yako....

Nakuhakikishia hutakipata chama hicho katika nchi yoyote hapa duniani....!!

Hivi vyama vya siasa tunaweza kuvifananisha na maisha ya ndoa ya mume na mke....

Kiasili hakuna MUME PERFECT KWA 100% na vivyo hivyo hayupo MKE PERFECT KWA 100%...

Lakini hii haizuii watu kuoana. Cha muhimu ni wanandoa kuijua principle muhimu ya ndoa ya; Kuvumiliana na kuheshimiana kwa kila mmoja kubeba mapungufu ya mwingine....

Ndivyo ilivyo ktk vyama vya siasa na hata mahusiano ya kawaida ya mtu na MTU....
Basi usitegemee kupata kipya
 
Tunajadili bila dili yoyote CDM. Hicho chama angekabidhiwa Mwambe au Sumaye? Ni wawili waliotia nia kuwania uwenyekiti labda kwa kuona Mbowe hatoshi. Au kwa sababu nyingine ovu na kubwa kuliko zote ya umamluki. Kuna siku ulimi wa Sumaye uliteleza ukamaka hadharani: Nawashangaa CCM wengine hawajui kuwa nalienda upinzani kwa faida ya CCM. Hiyo kauli hajapata kuifafanua wala hakuna aliyewahi kumuuliza maana yake. Kurudi kwake CCM ni jibu tosha!
Upinzani wenyewe upo kwaajili ya CCM sasa hapo hujaelewa nn kuhusu kauli ya Sumaye
 
Ccm iliwahi kujenga ofisi ipi na wapi? Tatizo ninyi watoto wadogo ambao bado mnajifuta makamasi kwenye pembe ya shavu mnajidanganya kuijua Sana ccm ilihali mnalishwa ujinga!
Ofisi za ccm tulizijenga sisi kwa michango ya lazima na mengine yaliporwa kutoka serikalini! Ccm haijawahi kujenga hata choo!
Hilo la elimu Bure hujui lilikoanzia. Sisi ndio tuliosoma Bure burashi kwa kupewa uji wa bulga SAA nne na ugali au ngano iliyofungwa vyema SAA name. Madaktari ya Bure na lijaa inakwenda stop kupewa jipya. Penseli, mfutio na founterpen na kudai Cha wino bure! Hatukukaa chini ya miembe Wala kukalika mawe na mikeka Bali dawati moja mtu mmoja! Vitabu vilitosha kwani kila mtu na vyake!
Hiyo ndio elimu bure niijuayo na siyo hii yako ya kumpa mwanafunzi sh Mia tatu kwa mwezi!
Mliidandia hoja ya cdm juu ya elimu bure bila kuwauliza wangeiimplement vipi na matokeo yake mnaishia kuwadanganya wananchi! Una hoja Tena nikuongeze nondo?
Kama mlijenga ofisi za CCM na bado mnazipenda rudini CCM
 
Lowassa aliletwa Chadema na TISS wakimtumia Apson na Gwajima bila Mbowe kujua ila baadae alikuja kugundua na hakutaka ajue chochote alifanya hivyo pia kwa Sumaye, Masha& Co. Mbowe baada ya kugundua alifanya makosa akaanza kuwafanyia ujasusi na kugundua wote walio kuja kutokea CCM na wimbi la Lowassa hakuna mwenye mapenzi na chama.

Sasa lile wimbi la Lowassa limegundua hawana nafasi mbele ya Chadema asili wameondoka wamebaki wale wachumia tumbo ambao walipata ubunge kwa upepo wa Lowassa, wanatafuta nguzo za chama wakiangamize lakini wapi Mbowe kasimama wamekwama.

Sasa Magufuli anatengeneza upinzani pure asili wa wafia chama ambao wapo tayari kwa lolote kuelekea uchaguzi mkuu, Anatengeneza mgogoro ndani ya ccm wa uteuzi wa wabunge mwaka 2020 kama ilivyokuwa kwa chadema mwaka 2015 yaani kiufupi yale waliyoyaita makapi na mafisadi watatumia muda mwingi kuyasafisha wakati chadema watakuwa na wagombea pure 2020.

Sasa wale mnaosubiri chadema ife subiri kura ya hasira ya wanachama wa ccm kwenye makapi.
Hapo Chadema nani mfia chama? Baada ya bunge kuvunjwa kila mtu anakula kona. Mkulu ana bil 8 ana uhakika wa kuishi hata dubai.
 
Mkuu kwenye ujio wa Lowassa Mbowe alizingua. Ile haikuhitaji intelijensia ya juu kujua kuwa Lowassa alikuwa sio mtu sahihi kwa cdm kwa nafasi hata ya udiwani, achia mbali ya urais.

Mkuu kila siku huwa nasema humu ndani kiongozi mzuri wa kuchaguliwa mwisho ni miaka 10, ukiwa na bahati ya ajabu mwisho ni miaka 15, nje ya hapo ni mauzauza. Hivi majuzi wakati wa uchaguzi mkuu wa cdm nilikuwa wazi kabisa kuwa Mbowe hastahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm tena, sio kwakuwa sio kiongozi mzuri, ila aisingweza kuwa na jipya tena. Sababu kubwa ni kuwa kakaa madarakani zaidi ya miaka 15, na kosa la kipuuzi kabisa la kumchukua Lowassa.

Mbowe na cdm wamejiweka kwenye mazingira ya kushambuliwa kisiasa, na kufanyiwa hujuma za wazi kwa sababu ya Mbowe kung'ang'ania madaraka. Hao wabunge wachache wanaohama na kukichafua chama wanapata nguvu hiyo kwanza kwa kuhongwa, na kisha wanatumia hiyo weakness ya Mbowe kukaa madarakani kuhama na kuichafua cdm. Sikufichi hao, wanaohama na tuhuma wanazotoa hata kama zote sio kweli, lakini zaidi ya asilimia 50 zina ukweli. Sisi tuko humu mitandaoni tunaitetea cdm kama taasisi, maana tunajua umuhimu wa upinzani, lakini hatuna uwezo wa kutetea viongozi ving'ang'anizi wa madaraka. Mbowe ana kipi cha maana ambacho kashindwa kukileta ndani ya cdm kwa hiyo miaka 15,ila ataweza sasa? Tusipokuwa wawazi kwa hawa viongozi wa wanaong'ang'ania madaraka kisa tunaipenda taasisi husika, itakuwa ngumu kuwakemea hawa madictator uchwara. Ukweli ni kuwa Mbowe hakustahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm, vinginevyo tutajua yuko madarakani kulinda hayo anayochafuliwa nayo. Ni vyema Mbowe kama anaipenda cdm, akae pembeni maana miaka 15 inatosha kwa kiongozi muungwana.
Bunge likivunjwa lazima utafute pa kujibanza.
 
Upinzani ulipaswa kuwa na viongozi wengi wenye mitazamo kama hii. Tatizo wengi wao ndiyo wale wa "zidumu fikra za mwenyekiti".
 
tindo,
Hebu Soma ulichoandika Kama nawe utakielewa! Utopolo mtupu! Huyo Magufuli kaachive Nini ndani ya miaka mitano?
Heri ya Mbowe kaijenga Chadema bila dola na fedha za umma.

Kama CCM haimuogopi Mbowe kwanini haimpi nafasi ya kufanya siasa Kama magu et al anavyofanya kwa miaka mitano na hajadeliver lolote kwa wananchi zaidi ya kuwatisha?
Hiki ndicho jinachoutesa upinzani. Hamtaki kabisa kukosolewa. Yaani kama chama tawala tu. Huyo tindo ni mpinzani mpaka kwenye damu ila kwa kuwa kasema ukweli unamletea maneno ya kejeli. Ndiyo maana wenye macho wanaona namna chama chenu kinavyoelekea shimoni.
 
Upinzani wenyewe upo kwaajili ya CCM sasa hapo hujaelewa nn kuhusu kauli ya Sumaye
Upinzani upo kwa ajili ya CCM na CCM je, ipo kwa ajili ya nini? Unakimbilia kushangaa sielewi nini ktk kauli ya Sumaye! Kauli yako mwenyewe unaielewa? Unakuwa CCM kwa ajili ya CDM kama mpelelezi/mamluki au kwa afya na ustawi wa CCM? CDM waliotakiwa kumwelewa,na si wewe, walimwelewa na kumpiga chini!
 
s
Lowassa aliletwa Chadema na TISS wakimtumia Apson na Gwajima bila Mbowe kujua ila baadae alikuja kugundua na hakutaka ajue chochote alifanya hivyo pia kwa Sumaye, Masha& Co. Mbowe baada ya kugundua alifanya makosa akaanza kuwafanyia ujasusi na kugundua wote walio kuja kutokea CCM na wimbi la Lowassa hakuna mwenye mapenzi na chama.

Sasa lile wimbi la Lowassa limegundua hawana nafasi mbele ya Chadema asili wameondoka wamebaki wale wachumia tumbo ambao walipata ubunge kwa upepo wa Lowassa, wanatafuta nguzo za chama wakiangamize lakini wapi Mbowe kasimama wamekwama.

Sasa Magufuli anatengeneza upinzani pure asili wa wafia chama ambao wapo tayari kwa lolote kuelekea uchaguzi mkuu, Anatengeneza mgogoro ndani ya ccm wa uteuzi wa wabunge mwaka 2020 kama ilivyokuwa kwa chadema mwaka 2015 yaani kiufupi yale waliyoyaita makapi na mafisadi watatumia muda mwingi kuyasafisha wakati chadema watakuwa na wagombea pure 2020.

Sasa wale mnaosubiri chadema ife subiri kura ya hasira ya wanachama wa ccm kwenye makapi.
siasa bhn
 
Upinzani upo kwa ajili ya CCM na CCM je, ipo kwa ajili ya nini? Unakimbilia kushangaa sielewi nini ktk kauli ya Sumaye! Kauli yako mwenyewe unaielewa? Unakuwa CCM kwa ajili ya CDM kama mpelelezi/mamluki au kwa afya na ustawi wa CCM? CDM waliotakiwa kumwelewa,na si wewe, walimwelewa na kumpiga chini!
Wakati mwingine usitumie akili sana kuwaelewesha hao, unaweza pia kumpa "like" afurahi.
 
Back
Top Bottom