Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,718
Reaction score
58,893
Lowassa aliletwa Chadema na TISS wakimtumia Apson na Gwajima bila Mbowe kujua ila baadae alikuja kugundua na hakutaka ajue chochote alifanya hivyo pia kwa Sumaye, Masha& Co. Mbowe baada ya kugundua alifanya makosa akaanza kuwafanyia ujasusi na kugundua wote walio kuja kutokea CCM na wimbi la Lowassa hakuna mwenye mapenzi na chama.

Sasa lile wimbi la Lowassa limegundua hawana nafasi mbele ya Chadema asili wameondoka wamebaki wale wachumia tumbo ambao walipata ubunge kwa upepo wa Lowassa, wanatafuta nguzo za chama wakiangamize lakini wapi Mbowe kasimama wamekwama.

Sasa Magufuli anatengeneza upinzani pure asili wa wafia chama ambao wapo tayari kwa lolote kuelekea uchaguzi mkuu, Anatengeneza mgogoro ndani ya ccm wa uteuzi wa wabunge mwaka 2020 kama ilivyokuwa kwa chadema mwaka 2015 yaani kiufupi yale waliyoyaita makapi na mafisadi watatumia muda mwingi kuyasafisha wakati chadema watakuwa na wagombea pure 2020.

Sasa wale mnaosubiri chadema ife subiri kura ya hasira ya wanachama wa ccm kwenye makapi.
 
Lowassa aliletwa Chadema na TISS wakimtumia Apson na Gwajima. bila Mbowe kujua ila badae alikuja kugundua na hakutaka ajue chochote alifanya hivyo pia kwa Sumaye, Masha& Co. Mbowe baada ya kugundua alifanya makosa akaanza kuwafanyia ujasusi na kugundua wote walio kuja kutokea ccm na wimbi la Lowassa hakuna mwenye mapenzi na chama.

Mkuu kwenye ujio wa Lowassa Mbowe alizingua. Ile haikuhitaji intelijensia ya juu kujua kuwa Lowassa alikuwa sio mtu sahihi kwa cdm kwa nafasi hata ya udiwani, achia mbali ya urais.

Mkuu kila siku huwa nasema humu ndani kiongozi mzuri wa kuchaguliwa mwisho ni miaka 10, ukiwa na bahati ya ajabu mwisho ni miaka 15, nje ya hapo ni mauzauza. Hivi majuzi wakati wa uchaguzi mkuu wa cdm nilikuwa wazi kabisa kuwa Mbowe hastahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm tena, sio kwakuwa sio kiongozi mzuri, ila aisingweza kuwa na jipya tena. Sababu kubwa ni kuwa kakaa madarakani zaidi ya miaka 15, na kosa la kipuuzi kabisa la kumchukua Lowassa.

Mbowe na cdm wamejiweka kwenye mazingira ya kushambuliwa kisiasa, na kufanyiwa hujuma za wazi kwa sababu ya Mbowe kung'ang'ania madaraka. Hao wabunge wachache wanaohama na kukichafua chama wanapata nguvu hiyo kwanza kwa kuhongwa, na kisha wanatumia hiyo weakness ya Mbowe kukaa madarakani kuhama na kuichafua cdm. Sikufichi hao, wanaohama na tuhuma wanazotoa hata kama zote sio kweli, lakini zaidi ya asilimia 50 zina ukweli. Sisi tuko humu mitandaoni tunaitetea cdm kama taasisi, maana tunajua umuhimu wa upinzani, lakini hatuna uwezo wa kutetea viongozi ving'ang'anizi wa madaraka. Mbowe ana kipi cha maana ambacho kashindwa kukileta ndani ya cdm kwa hiyo miaka 15,ila ataweza sasa? Tusipokuwa wawazi kwa hawa viongozi wa wanaong'ang'ania madaraka kisa tunaipenda taasisi husika, itakuwa ngumu kuwakemea hawa madictator uchwara. Ukweli ni kuwa Mbowe hakustahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm, vinginevyo tutajua yuko madarakani kulinda hayo anayochafuliwa nayo. Ni vyema Mbowe kama anaipenda cdm, akae pembeni maana miaka 15 inatosha kwa kiongozi muungwana.
 
Safari hii Tiss itawaletea membe

Nje ya mada unadhani Mbowe yupo sirias sana?
Usilegeze sauti hapa! Kinara wa mipango yote ya kumnunua na kupanga vurugu kazikwa juzi na hakuna aliyemkaimisha nafasi yake! Au hukumwona mwenyekiti alivyomlilia wakati wa kuagwa Dodoma?
Kwa kifupi CCM shughuli hakuna imebaki yatima!
Na Mbowe anakwenda kuibuka shujaa October!
 
Mbowe anaibuka shujaa wa nini [emoji2]
Usilegeze sauti hapa! Kinara wa mipango yote ya kumnunua na kupanga vurugu kazikwa juzi na hakuna aliyemkaimisha nafasi yake! Au hukumwona mwenyekiti alivyomlilia wakati wa kuagwa dodoma?
Kwa kifupi ccm shughuli hakuna imebaki yatima!
Na Mbowe anakwenda kuibuka shujaa October!
 
Hivi unadhani hata mwamba ana mapenzi ya kweli na cdm? Labda siku na yy akiunga mkono juhudi ndo utajua hata hao unawaamini wote ni mamluki... mpinzani wa kweli nchi hii alikuwa mchungaji Christopher mtikila r.i.p wengine wote wachumia tumbo akiwemo na huyo mwamba
 
tindo,
Hebu Soma ulichoandika Kama nawe utakielewa! Utopolo mtupu! Huyo Magufuli kaachive Nini ndani ya miaka mitano?
Heri ya Mbowe kaijenga Chadema bila dola na fedha za umma.

Kama CCM haimuogopi Mbowe kwanini haimpi nafasi ya kufanya siasa Kama magu et al anavyofanya kwa miaka mitano na hajadeliver lolote kwa wananchi zaidi ya kuwatisha?
 
Usilegeze sauti hapa! Kinara wa mipango yote ya kumnunua na kupanga vurugu kazikwa juzi na hakuna aliyemkaimisha nafasi yake! Au hukumwona mwenyekiti alivyomlilia wakati wa kuagwa dodoma?
Kwa kifupi ccm shughuli hakuna imebaki yatima!
Na Mbowe anakwenda kuibuka shujaa October!
Labda atakuwa shujaa wa kula michango ya wabunge
 
Hebu Soma ulichoandika Kama nawe utakielewa! Utopolo mtupu! Huyo Magufuli kaachive Nini ndani ya miaka mitano?
Heri ya Mbowe kaijenga Chadema bila dola na fedha za umma.

Kama CCM haimuogopi Mbowe kwanini haimpi nafasi ya kufanya siasa Kama Magufuli et al anavyofanya kwa miaka mitano na hajadeliver lolote kwa wananchi zaidi ya kuwatisha?

Nilichokiandika sijakiandika kwa bahati mbaya, na hata mleta uzi nadhani anaweza kushangaa kidogo na hiki nilichoandika. Nimeandika ambacho sina shaka nacho. Sina tatizo na mchango mkubwa wa Mbowe kwenye ujenzi wa Chadema na hapa Chadema alipoifikisha. Ila taka usitake Mbowe hakustahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm baada ya miaka 15. Chadema ni taasisi na sio Mbowe, kama unaishi kwenye zama za kusujudia watu, huko tulishatoka.
 
Hebu Soma ulichoandika Kama nawe utakielewa! Utopolo mtupu! Huyo magu kaachive Nini ndani ya miaka mitano?
Heri ya Mbowe kaijenga cdm bila dola na fedha za umma.
Kama ccm haimuogopi Mbowe kwanini haimpi nafasi ya kufanya siasa Kama magu et al anavyofanya kwa miaka mitano na hajadeliver lolote kwa wananchi zaidi ya kuwatisha?
Mbowe anajivunia sana kuwa na watu viazi kama wewe! Huyo uliyem quote hujamwelewa kabisa alichoandika
 
Back
Top Bottom