Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Nilichokiandika sijakiandika kwa bahati mbaya, na hata mleta uzi nadhani anaweza kushangaa kidogo na hiki nilichoandika. Nimeandika ambacho sina shaka nacho. Sina tatizo na mchango mkubwa wa Mbowe kwenye ujenzi wa cdm na hapa cdm alipoifikisha. Ila taka usitake Mbowe hakustahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm baada ya miaka 15. Cdm ni taasisi na sio Mbowe, kama unaishi kwenye zama za kusujudia watu, huko tulishatoka.
Mkuu kwa maoni yako unadhani nani angefaa kumpokea kijiti Mbowe katika wakati huu.
 
tindo, Kuna msemo usemao, "haijalishi uwezo ulionao katika kulitawala jukwaa, dansa mzuri ni yule anayejua muda sahihi wa kuondoka jukwaa"

Na pia kuna utafiti uliwa kuja na conclusion isemayo "binadamu ana muda wake wa kuwa makini kwenye jambo fulani, muda huo ukizidi umakini unapungua

Hata hivyo pamoja na ukweli wote huo, kwa pale CHADEMA kwa sasa hapakuwa na mtu sahihi wa kuachiwa uenyekiti hasa baada ya kina Prof. Safari na Marando kuonyesha dalili za kuchoka choka hivi

Ni bahati mbaya sana viongozi wengi hawawaandai viongozi wakubwa mapema

Hadi leo pamoja na uchovu wake, bado Mbowe hajapata mrithi!

Lisu, Lema, Heche, Msigwa, Mnyika hawa wote ni viongozi wazuri lakini hawajafikia kuwa watoa maamuzi wa mwisho. Hiyo position ina busara zake ambazo hawa hawajazifikia

Kwahiyo Mbowe bado anasafari ya kupata mrithi ambaye hatakuwa mamluki kama alivyotaka kujaribu Sumaye. Kosa wanalolifanya chadema ni kutoruhusu au kushawishi watu kujipima nguvu angalau kwa kuonyesha nia na kuruhusiwa kugombea. Haya mazoezi ni muhimu sana
 
Mkuu kwa maoni yako unadhani nani angefaa kumpokea kijiti mbowe katika wakati huu.

Wapo wengi sana, kama cdm haina mtu wa kuweza kuwa mwenyekiti nje ya Mbowe, basi hiyo sio taasisi, bali ni kikundi cha watu walio kwenye siasa. Na wala usithubutu kusema tena nani angestahili kuwa mwenyekiti. Chama kina miaka 28 sasa, kisiwe na uwezo wa mtu mwingine kuwa mwenyekiti zaidi ya mtu mmoja!?
 
Mbowe anajivunia sana kuwa na watu viazi kama wewe! Huyo uliyem quote hujamwelewa kabisa alichoandika
Bora miye kiazi kuliko wewe bumunda! Lazima umtetee kibama mwenzako kwani akili zenu zimekaa kibuku Saba na hamuwezi kufikiri wenyewe mpaka mfikirishwe! Uelewa wako wa kidarasa la tatu si hauwezi kufanana na wangu kwani sijafundwa kusifu na kumwabudu binadamu Wala madaraka na mabarabara!

Endeleeni kujificha chini ya maflyover na mareli na kuwasahau wananchi! Chadema ni akili kubwa isiyotegemea dola Wala pesa za wizi! Ipo kushinda na kuchukua uongozi bila shuruti! Upo bumunda?????
 
tindo, Kwa utawala huu kamanda ulitaka tumpe Sumaye? Kweli? Yaani tumpatie Mwambe kisa Mbowe kakaa madarakani kwa miaka 15?? Wewe jamaa wewe embu watathimini hao waliokuwa wagombea wko na uwalinganishe na Mbowe... mmmmuhhh naanza kukuogopa
 
Nilichokiandika sijakiandika kwa bahati mbaya, na hata mleta uzi nadhani anaweza kushangaa kidogo na hiki nilichoandika. Nimeandika ambacho sina shaka nacho. Sina tatizo na mchango mkubwa wa Mbowe kwenye ujenzi wa cdm na hapa cdm alipoifikisha. Ila taka usitake Mbowe hakustahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm baada ya miaka 15. Cdm ni taasisi na sio Mbowe, kama unaishi kwenye zama za kusujudia watu, huko tulishatoka.
Ndugu, Asante kwa mtazamo wako na ushauri wako usio na maana! Ni sawa na kusema kuwa babako baada ya kuwajengea nyumba nzuri mnayoishi na kuijivunia aondoke na kuwaacha ninyi watoto uongozi na utawala wa nyumba hiyo! Mbona ninyi pande hizo hamuishi kumwombea magu miaka mingi ili akamilishe aliyoyaanzisha? Why cdm na Mbowe wasipewe hiyo guess mnayomuombea mwenyekiti wenu? Hii siyo sawa!
 
Lowassa aliletwa Chadema na TISS wakimtumia Apson na Gwajima. bila Mbowe kujua ila badae alikuja kugundua na hakutaka ajue chochote alifanya hivyo pia kwa Sumaye, Masha& Co. Mbowe baada ya kugundua alifanya makosa akaanza kuwafanyia ujasusi na kugundua wote walio kuja kutokea ccm na wimbi la Lowassa hakuna mwenye mapenzi na chama.

Sasa lile wimbi la Lowassa limegundua hawana nafasi mbele ya chadema asili wameondoka wamebaki wale wachumia tumbo ambao walipata ubunge kwa upepo wa fisadi Lowassa. wanatafuta nguzo za chama wakiangamize lakini wapi mbowe kasimama wamekwama.

Sasa Magufuli anatengeneza upinzani pure asili wa wafia chama ambao wapo tayari kwa lolote kuelekea uchaguzi mkuu, Anatengeneza mgogoro ndani ya ccm wa uteuzi wa wabunge mwaka 2020 kama ilivyokuwa kwa chadema mwaka 2015 yaani kiufupi yale waliyoyaita makapi na mafisadi watatumia muda mwingi kuyasafisha wakati chadema watakuwa na wagombea pure 2020.

Sasa wale mnaosubiri chadema ife subiri kura ya hasira ya wanachama wa ccm kwenye makapi.
Ccm chini ya JPM hakuna makundi. Hivyo mtu akipita kwenye kura za maoni tambua anakubalika.
Mliobaki Chadema ni vibaraka mnaoishi kwa kulipwa na Mbowe huku yeye akikwapua bil 8.
 
Chadema mnafurahisha kweli, Kwahiyo Mkuu na midevu yako unaamini Mbowe atashinda ubunge?
Asishinde kwasababu ipi? Kwani alivyoshinda mwanzo kitamzuia nini?
Wewe sio mpiga kura wake, usisumbuke atashinda kwa kura za watu wake! Acha kuumia, utakufa kibudu!
 
Lowassa aliletwa Chadema na TISS wakimtumia Apson na Gwajima. bila Mbowe kujua ila badae alikuja kugundua na hakutaka ajue chochote alifanya hivyo pia kwa Sumaye, Masha& Co. Mbowe baada ya kugundua alifanya makosa akaanza kuwafanyia ujasusi na kugundua wote walio kuja kutokea ccm na wimbi la Lowassa hakuna mwenye mapenzi na chama.

Sasa lile wimbi la Lowassa limegundua hawana nafasi mbele ya chadema asili wameondoka wamebaki wale wachumia tumbo ambao walipata ubunge kwa upepo wa fisadi Lowassa. wanatafuta nguzo za chama wakiangamize lakini wapi mbowe kasimama wamekwama.

Sasa Magufuli anatengeneza upinzani pure asili wa wafia chama ambao wapo tayari kwa lolote kuelekea uchaguzi mkuu, Anatengeneza mgogoro ndani ya ccm wa uteuzi wa wabunge mwaka 2020 kama ilivyokuwa kwa chadema mwaka 2015 yaani kiufupi yale waliyoyaita makapi na mafisadi watatumia muda mwingi kuyasafisha wakati chadema watakuwa na wagombea pure 2020.

Sasa wale mnaosubiri chadema ife subiri kura ya hasira ya wanachama wa ccm kwenye makapi.
Hakuna unachojua kaa kimya! Unadhani siasa rahisi kiasi hicho! Yani unatumwa then unatukanwa na huyohuyo alokutuma matusi yote duniani kisa hela au nini! Siyo huyo waIiyekuwa wanamwambia amevaa pampas!! Unajua kama Rais Nkurunzinza na Agaton walikuwa marafiki na waliwahi kulala chumba kimoja?
 
tindo,
Nahisi kama tindo umelewa K-vant na mbege. Point kama hizi umezitoa wapi?
Ila umeharibu kumuita mzalendo namba 1 dikteta uchwara. Kuwa na heshima. Leo usinge pita pale Ubungo interchange bila mzalendo kukomaa.
 
Kwa utawala huu kamanda ulitaka tumpe sumaye??? Kweli??? Yaani tumpatie Mwambe kisa mbowe kakaa madarakani kwa miaka 15?? Wee jamaa ww embu watathimini hao waliokuwa wagombea wko na uwalinganishe na mbowe... mmmmuhhh naanza kukuogopa

Mkuu usidhani nilichokiongea nimeongea kwa bahati, nina akili zangu timamu, niulize leo, kesho na hata keshokutwa uone kama nitabadilika katika haya niliyoandika. Nina uwezo wa kutenganisha uwezo wa Mbowe katika siasa, na nafasi ya uenyekiti ndani ya cdm. Katika watu waliopinga na watakaoendelea kupinga ujio wa wanaccm ndani ya cdm na kupewa nafasi za ugombea kwa mtindo wa mwendo Fasta ni mimi.

Katika mapendekezo yangu huko siku za nyuma ili yaingizwe katika katiba ya cdm ilikuwa kama ifuatavyo hapo chini, hasa baada ya Shibuda kuingia cdm na kuleta upuuzi wa ccm ndani ya cdm
  1. Mtu yoyote anayetaka kugombea udiwani au ubunge ni lazima awe amekaa cdm sio chini ya miaka mitano na achunguzwe mwenendo wake.
  2. Anayetaka kugombea urais asiwe amekaa cdm chini ya miaka 10. Na sio kukaa tu, bali awe na sifa stahiki za kugombea nafasi hiyo, tena kwa mchakato ulio wazi.
  3. Mwanachama yoyote asishike nafasi yoyote ya juu ndani ya cdm mpaka awe amemaliza miaka 10, na awe na sifa stahiki.
  4. Mwanachama yoyote anayetoka chama kingine chochote cha siasa kwa sababu zozote zile, asishike nafasi yoyote ndani ya chama, mpaka amalize miaka mitatu
Pitia hayo mapendekezo yangu unionyeshe ni wapi hizo taka ngumu toka ccm, zingepata nafasi iwapo hayo mapendekezo yangu yangekuwa ndani ya katiba ya cdm.
 
Nahisi kama tindo umelewa K vant na mbege. Point kama hizi umezitoa wapi?
Ila umeharibu kumuita mzalendo namba 1 dikteta uchwara. Kuwa na heshima. Leo usinge pita pale ubungo interchange bila mzalendo kukomaa.

Kwa bahati mbaya situmii kilevi chochote. Nina akili timamu. Mimi sio bendera fuata upepo kama ww, na siasa naijua vyema. Kama kujenga ubungo interchange Ni kipimo cha uzalendo, basi wazungu waliojenga reli hapa nchini, walikuwa wazalendo kuliko mtanzania yoyote wa asili.
 
Mkuu usidhani nilichokiongea nimeongea kwa bahati, nina akili zangu timamu, niulize leo, kesho na hata keshokutwa uone kama nitabadilika katika haya niliyoandika. Nina uwezo wa kutenganisha uwezo wa Mbowe katika siasa, na nafasi ya uenyekiti ndani ya cdm. Katika watu waliopinga na watakaoendelea kupinga ujio wa wanaccm ndani ya cdm na kupewa nafasi za ugombea kwa mtindo wa mwendo Fasta ni mimi.

Katika mapendekezo yangu huko siku za nyuma ili yaingizwe katika katiba ya cdm ilikuwa kama ifuatavyo hapo chini, hasa baada ya Shibuda kuingia cdm na kuleta upuuzi wa ccm ndani ya cdm
  1. Mtu yoyote anayetaka kugombea udiwani au ubunge ni lazima awe amekaa cdm sio chini ya miaka mitano na achunguzwe mwenendo wake.
  2. Anayetaka kugombea urais asiwe amekaa cdm chini ya miaka 10. Na sio kukaa tu, bali awe na sifa stahiki za kugombea nafasi hiyo, tena kwa mchakato ulio wazi.
  3. Mwanachama yoyote asishike nafasi yoyote ya juu ndani ya cdm mpaka awe amemaliza miaka 10, na awe na sifa stahiki.
  4. Mwanachama yoyote anayetoka chama kingine chochote cha siasa kwa sababu zozote zile, asishike nafasi yoyote ndani ya chama, mpaka amalize miaka mitatu
Pitia hayo mapendekezo yangu unionyeshe ni wapi hizo taka ngumu toka ccm, zingepata nafasi iwapo hayo mapendekezo yangu yangekuwa ndani ya katiba ya cdm.
Haya mkuu nimekusoma
 
Laana ya DK Slaa aliyomwachia Mbowe na Chadema yake haitawaacha salama

Laana gani Dr. Slaa ataweza kuiachia Chadema? Au umesikia maneno ya propaganda mfu na wewe unakuja kuyatapika hapa jukwaani kama ulivyokariri nyimbo za Diamond?
 
Back
Top Bottom