Rais Magufuli angefariki mwaka 2024, Samia angemalizia mwaka 1 uliobaki au angetawala miaka 5?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
9,504
Reaction score
20,293
Wakuu habari, baada ya Rais Magufuli kufariki, Samia Suluhu ambaye alikuwa makamu wake alikuwa Rais, sasa swali likaja kuibuka kuwa Samia anandeleza awamu ya Magufuli (AWAMU YA 5) au itakuwa ni awamu mpya? ikaamuliwa kuwa ni awamu mpya ila Serikali ikabaki ile ile ya Magufuli

Sasa nauliza ingekuwa ni mwaka mmoja umebaki au miwili kisha ndio Magufuli ndio akafariki, ingekuwa ni awamu ya 6 ya Samia au ingekuwa anamalizia awamu ya 5 ya Magufuli? na kama ni awamu mpya angepewa miaka 5 au angemalizia huo mwaka mmoja na mchakato wa kumpata Rais mwingine kuanza?
 



Sheria ni kwamba makamu anachukuwa kwa muda uliobaki halafu anaweza kugombea tena kwa muhula mmoja. Hiyo ndiyo sheria. Hata kama ni miezi.
 
 
Kikatiba angemalizia huo mwaka mmoja na kuwa na uwezo wa kugombea awamu mbili kwa miaka kumi.
 
Acheni kupotosha,huyu ni rais wa.sita lakini awamu.ya tano.Mnasema ni rais wa awamu ya sita kwani Kuna uchaguzi ulifanyika tofauti na ule wa October 2020 ?
sisi ndio tunaopotosha mkuu? au Bunge, Samia na serikali na CCM yao wote wanasema hii ni awamu ya 6
 
Kikatiba angemalizia huo mwaka mmoja na kuwa na uwezo wa kugombea awamu mbili kwa miaka kumi.
kwa hiyo tusema angekufa 2022 angemalizia miaka 3 kisha agombee tena miaka 10? na kwa mantiki hiyo, Magufuli alikufa 2021 Samia atamalizie miaka 4 iliyobaki kisha agombee 10
 
Acheni kupotosha,huyu ni rais wa.sita lakini awamu.ya tano.Mnasema ni rais wa awamu ya sita kwani Kuna uchaguzi ulifanyika tofauti na ule wa October 2020 ?
Awamu haifuati uchaguzi bali ni nani yuko madarakani. Kama ni chaguzi tu basi Tanzania ilishafanya chaguzi zaidi ya 10 tangu uhuru ... Ndiyo maana inapotajwa awamu ni lazima iendane na jina la mtu.
 
Mungu angemchelewesha kwa muda wote huo? Ni vile Mungu alitaka timing sahihi ya baada ya uchaguzi, angefanya kabla, sukuma gang wangesumbua, hasa kwenye transition, Sasa mama ana jukumu la kufagia na kumaliza kisiasa na kudhoofisha kundi lote la sukuma gang, sms na calls zinafanyiwa analysis maana kipindi kile walijiachia na kuchat bila wasiwasi
 
Awamu haifuati uchaguzi bali ni nani yuko madarakani. Kama ni chaguzi tu basi Tanzania ilishafanya chaguzi zaidi ya 10 tangu uhuru ... Ndiyo maana inapotajwa awamu ni lazima iendane na jina la mtu.
kwa hiyo ingekuwa mwaka 2024 ingekuwa awamu ya 6 pia? ambayo ingetekiwa kutawala miaka mingapi jumla?
 
Subiri Samia afariki 2024.Hapo ndo tutajua kama Mpango atamalizia mwaka mmoja awamu ya Saba then aendelee tena 2025 -2035
Hii ni ramli chonganishi!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…