Huwa nasoma sana katiba, na sijaona popote katiba inapozungumzia habari za awamu! Sana sana inazungumzia suala la vipindi ambavyo mtu anaweza kuchaguliwa na kushikilia kiti cha urais.
Lakini kwa kuangalia muktadha wa thread hii, Ibara ya 37(5) inaeleza wazi kwamba:-
Na tena kwa kuangalia muktadha wa thread husika, Ibara ya 40 iliyotajwa hapo juu inahusisha kifungu kidogo cha 4, yaani Ibara ya 40(4) inayosema kwamba:-
Hivyo basi, sehemu ambayo sija-highlight hapo juu ndiyo inajibu swali lako kwamba:-
Kwamba, kwavile katiba yetu inatoa ruhusa ya mtu kugombea MARA MBILI TU, na kwavile SSH kwa sasa katiba inamruhusu kugombea MARA MOJA TU, basi tukiendekeza habari za AWAMU hii tutaita AWAMU MPYA (ya 6)!
Ni kutokana na hilo, na ndo maana katiba itamhuruhusu kugombea mara MOJA TU, kwa sababu muda atakaokaa madarakani kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) unatosha kuwa awamu inayojitegemea.
Na haiwezi kuingia akilini kwa mfano, 2025 SSH asimame jukwaani halafu mapungufu ya serikali yake yeye akiwa kama Rais aje kumdondoshea jumba bovu JPM kwa sababu atakuwa ameongoza kwa muda wa kutosha kurekebisha pale ambapo anadhani alikuta pana kasoro!
Kinyume chake, kama JPM angefariki 2024 na hivyo SSH kushika kiti kwa mwaka mmoja tu, muda huo hautoshi kuwa awamu inayojitegemea na ndo maana anapewa fursa ya kugombea upya mara mbili.
Hapo hata angetaka kumdondoshea jumba bovu JPM in 2025, angekuwa na uhalali wa kufanya hivyo bila kujali kwamba alikuwa VP.