No, japo hii, ilikuwa ni serikali ya awamu ya 5, JPM alipofariki ghafla in less than a year madarakani, amehitimisha awamu yake ya 5 kwa kuikatisha, na Samia japo amepokea tuu, ndio ameanzisha awamu yake ya 6. Tena ilipaswa kuwa, baada tuu ya Samia kuapishwa, kuwa rais wa JMT, ilikuwa 1. Ama Waziri Mkuu alipaswa kujiuzulu ili kuihitimisha serikali ya awamu ya 5, ama, 2. Samia alipaswa kulivunja Baraza la Mawaziri kuihitimisha serikali ya awamu ya 5, na kuunda Baraza jipya la serikali ya awamu ya 6, hata kama angewateua Mawaziri wale wale.
Endapo rais JPM angefariki baada ya miaka mitatu madarakani, then ndipo Samia angeapishwa kwa kuwa rais wa 6, na kuiendeleza serikali ya awamu ya 5 hadi kuihitimisha ile 2025. Hapa ndipo serikali haikupaswa kuvunjwa. Na Samia baada ya kuihitimisha ngwe ya pili ya serikali ya awamu ya 5, 2025 ndipo angeanza na serikali yake ya awamu 6 yenye vipindi vyake viwili adi 2035!.
Kuna watu wanadhani rais Samia ni lazima agombee 2025 ili kukamilisha awamu yake ya pili, no!. Kufikia 2025 Samia anaweza kuona imetosha na akaamua 2025 hagombei urais, ila Watanzania tumeamua 2025 twende na mgombea mwanamke not necessarily Samia.
Wanabodi, Kati ya maeneo magumu sana kwenye tasnia ya habari ambayo kwa sisi Tanzania tumelikosa, tunaendelea kulikosa, na kama hawatajitokeza watu wenye uwezo wa kulifanya, tutaendelea kulikosa, ni eneo la "news analysis" uchambuzi wa habari. Kazi kuu za traditional media ni kuhabarisha...
www.jamiiforums.com
P