Rais Magufuli angefariki mwaka 2024, Samia angemalizia mwaka 1 uliobaki au angetawala miaka 5?

Rais Magufuli angefariki mwaka 2024, Samia angemalizia mwaka 1 uliobaki au angetawala miaka 5?

Mungu angemchelewesha kwa muda wote huo? Ni vile Mungu alitaka timing sahihi ya baada ya uchaguzi, angefanya kabla, sukuma gang wangesumbua, hasa kwenye transition, Sasa mama ana jukumu la kufagia na kumaliza kisiasa na kudhoofisha kundi lote la sukuma gang, sms na calls zinafanyiwa analysis maana kipindi kile walijiachia na kuchat bila wasiwasi
Kumbee

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Acheni kupotosha,huyu ni rais wa.sita lakini awamu.ya tano.Mnasema ni rais wa awamu ya sita kwani Kuna uchaguzi ulifanyika tofauti na ule wa October 2020 ?Nini maana ya awamu? Neno awamu lipo katiba ya muungano? Wengine tunakumbuka fika ni raisi ali hassan alienzisha mtindo wa kuiita serikali ya awamu ya tatu. Ajabu baina ya utawala wa hayati karume na jumbe kulifanyika chaguzi zaidi ya tatu, sasa kwa nini serikali ya ali hassan akawa anaiita serikali ya tatu? Kama matumizi ya neno awamu linaendana na uchaguzi kama unavyosema basi kwa sasa hii itakuwa labda awamu ya 19 maana wakati wa nyerere kulifanyika uchaguzi zaidi ya mara 9 na ofcourse Nyerere alishinda mara zote
 
Haya ndio matatizo ya kudohowa maneno ya lugha nyengine na kutaka kuyafanya maneno hayo kuwa official ya lugha yetu.
 
Huwa nasoma sana katiba, na sijaona popote katiba inapozungumzia habari za awamu! Sana sana inazungumzia suala la vipindi ambavyo mtu anaweza kuchaguliwa na kushikilia kiti cha urais.

Lakini kwa kuangalia muktadha wa thread hii, Ibara ya 37(5) inaeleza wazi kwamba:-

Na tena kwa kuangalia muktadha wa thread husika, Ibara ya 40 iliyotajwa hapo juu inahusisha kifungu kidogo cha 4, yaani Ibara ya 40(4) inayosema kwamba:-

Hivyo basi, sehemu ambayo sija-highlight hapo juu ndiyo inajibu swali lako kwamba:-

Kwamba, kwavile katiba yetu inatoa ruhusa ya mtu kugombea MARA MBILI TU, na kwavile SSH kwa sasa katiba inamruhusu kugombea MARA MOJA TU, basi tukiendekeza habari za AWAMU hii tutaita AWAMU MPYA (ya 6)!

Ni kutokana na hilo, na ndo maana katiba itamhuruhusu kugombea mara MOJA TU, kwa sababu muda atakaokaa madarakani kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) unatosha kuwa awamu inayojitegemea.

Na haiwezi kuingia akilini kwa mfano, 2025 SSH asimame jukwaani halafu mapungufu ya serikali yake yeye akiwa kama Rais aje kumdondoshea jumba bovu JPM kwa sababu atakuwa ameongoza kwa muda wa kutosha kurekebisha pale ambapo anadhani alikuta pana kasoro!

Kinyume chake, kama JPM angefariki 2024 na hivyo SSH kushika kiti kwa mwaka mmoja tu, muda huo hautoshi kuwa awamu inayojitegemea na ndo maana anapewa fursa ya kugombea upya mara mbili.

Hapo hata angetaka kumdondoshea jumba bovu JPM in 2025, angekuwa na uhalali wa kufanya hivyo bila kujali kwamba alikuwa VP.
mkuu asante kwa maelezo marefu na ya kina...nimeelewa
 
Hicho kifungu kinachosema hivyo mbona hamkitaji? Kuna mwingine kaniwekea kifungu feki
1646228597370.png
 
Hii ni ramli chonganishi!.
P
Naunga mkono hoja tuachane na hayo
 
Wakuu habari, baada ya Rais Magufuli kufariki, Samia Suluhu ambaye alikuwa makamu wake alikuwa Rais, sasa swali likaja kuibuka kuwa Samia anandeleza awamu ya Magufuli (AWAMU YA 5) au itakuwa ni awamu mpya? ikaamuliwa kuwa ni awamu mpya ila Serikali ikabaki ile ile ya Magufuli

Sasa nauliza ingekuwa ni mwaka mmoja umebaki au miwili kisha ndio Magufuli ndio akafariki, ingekuwa ni awamu ya 6 ya Samia au ingekuwa anamalizia awamu ya 5 ya Magufuli? na kama ni awamu mpya angepewa miaka 5 au angemalizia huo mwaka mmoja na mchakato wa kumpata Rais mwingine kuanza?
...na huo mwaka mmoja angesema ni awamu ya sita?
 
Maswali mengine bana, haya huo mwaka ungemalizia wewe, . Happy now?
 
mkuu naonaga unaanzisha uzi zednye hoja nzuri sana, usijishushie heshima kwa mambo kama haya
Katika uhalisia wa mambo wakati mwingine huwa tunajiondoa kwenye picha nzima na kufikiri hayatuhusu.
Katika mahesabu tunafundishwa kufikiri in collaterally inverse terms na effects zake.
Fikiria hilo.
 
Katika uhalisia wa mambo wakati mwingine huwa tunajiondoa kwenye picha nzima na kufikiri hayatuhusu.
Katika mahesabu tunafundishwa kufikiri in collaterally inverse terms na effects zake.
Fikiria hilo.
kivipi, nimeuliza swali kuhusu mambo ya kikatiba, wewe unatoa majibu ya kejeli, kama hujui si unakaa kimya? mbona wengi wamejibu kistaarabu tu,
 
kivipi, nimeuliza swali kuhusu mambo ya kikatiba, wewe unatoa majibu ya kejeli, kama hujui si unakaa kimya? mbona wengi wamejibu kistaarabu tu,
Sasa hebu tuone swali lako la "kikatiba".
Wewe nikuulize kwanza, mtawaliwa ulikuwa maamuzi gani katika kuingia urais mama Samia, uwepo au usiwepo.
 
Back
Top Bottom