Rais Magufuli angefariki mwaka 2024, Samia angemalizia mwaka 1 uliobaki au angetawala miaka 5?

mkuu na wewe hebu tupe nmaoni yako kuhusu hilo swali
 
Kufa kufaana mjomba acha vitisho bwasheee, nikikumbuka kipindi cha Hayati Magufuli nyimbo za kuongezewa miaka ya kuongoza na alivyozima ghafla..

Ya Mungu mengi, ngoja na huyu aanze kupambwa uone ukuu wa Mungu..
 
mkuu na wewe hebu tupe nmaoni yako kuhusu hilo swali
Limeisha jibiwa vizuri kabisa. Watu hawasomi katiba. Katiba imetamka rais anapofariki, VP anaapishwa kuwa rais. Kama muda uliobaki ni zaidi ya miaka mitatu, then itahesabiwa ndio awamu ya kwanza ya rais mpya, bado atakuwa na fursa ya kugombea awamu yake ya pili.

Lakini muda uliobakia kama ni pungufu ya miaka miwili, then rais mpya anashika madaraka Kumalizia awamu iliyotangulia, kisha ana awamu zake mbili za kugombea.

Kuhusu mgombea wa 2025, naendelea kusisitiza...
P
 
Kwa uelewa wangu awamu ni miaka kumi au zadi(Nyerere),au Raisi mpya,whatever comes first!!.
Alianza Nyerere(10+yrs)Mwinyi(10),Mkapa(10),Kikwete(10)JPM(6),kabla haija Ishakumi akafa,amekuja Raisi mwingine,ni awamu nyingine maana Raisi kabadirika,hata tukifnya uchaguzi 2025,akipita Samia ni Raisi wa awamu ya sita,haiwi ya saba,maana ni mtu Yule Yule,lakini akishinda Mbowe anakuwa Raisi wa awamu ya saba!sio sita Tena.
Na tukumbuke,kila baada ya miaka 5 ni Uchaguzi mkuu,whatever happen,
 
Subiri Samia afariki 2024.Hapo ndo tutajua kama Mpango atamalizia mwaka mmoja awamu ya Saba then aendelee tena 2025 -2035
Mimi sitaki urais asilan iwapo watu watazungumza kiurahisi hivi kuhusu kufa kwangu!
 
ni Rais aliyetokana na katiba, anaongoza kwa kumalizia kipindi alichoacha mwenzake hata kama ni mwezi mmoja, nafikiri unasahihisha yakuwa atakuwa ni wa awamu gani, bado tupo katika awamu ya5 ila tuna Rais wa6 kwa orodha ya Marais waliongoza nchi.
 
Awamu haifuati uchaguzi bali ni nani yuko madarakani. Kama ni chaguzi tu basi Tanzania ilishafanya chaguzi zaidi ya 10 tangu uhuru ... Ndiyo maana inapotajwa awamu ni lazima iendane na jina la mtu.
Awamu ni mchanyiko wa mambo mengi. Siyo rais tu. Rais akifariki anayepokea anaendeleza ile awamu. Awamu mpya inakuja na uchaguzi mpya, sera mpya na rais mpya.
 
kwa hiyo tusema angekufa 2022 angemalizia miaka 3 kisha agombee tena miaka 10? na kwa mantiki hiyo, Magufuli alikufa 2021 Samia atamalizie miaka 4 iliyobaki kisha agombee 10

Kikatiba. Rais akifa ikiwa muda umebaki miaka mitatu na zaidi, makamu wa Rais anaruhusiwa kugombea kipindi kimoja tu. Ila Kama Ni Chini ya miaka mitatu, basi makamu wa Rais anaruhusiwa kugombea miaka 10 zaidi. Ndio maana Rais Samia atagombea kipindi kingine Cha miaka mitano basi, kwasababu amerithi urais muda ukiwa zaidi ya miaka mitatu.
 
asante ila kama ungeweza kuweka hicho kifungu au screenshot ningeshukuru sana
 
Awamu ni mchanyiko wa mambo mengi. Siyo rais tu. Rais akifariki anayepokea anaendeleza ile awamu. Awamu mpya inakuja na uchaguzi mpya, sera mpya na rais mpya.
kwa hiyo hii haikupaswa kuwa awamu ya 6, ilipaswa kuwa awamu ya 5 na Samia anaruhusiwa kuimalizia na kugombea miaka yake 10 ya awamu ya 6?
 
kwa hiyo hii haikupaswa kuwa awamu ya 6, ilipaswa kuwa awamu ya 5 na Samia anaruhusiwa kuimalizia na kugombea miaka yake 10 ya awamu ya 6?
No, japo hii, ilikuwa ni serikali ya awamu ya 5, JPM alipofariki ghafla in less than a year madarakani, amehitimisha awamu yake ya 5 kwa kuikatisha, na Samia japo amepokea tuu, ndio ameanzisha awamu yake ya 6. Tena ilipaswa kuwa, baada tuu ya Samia kuapishwa, kuwa rais wa JMT, ilikuwa 1. Ama Waziri Mkuu alipaswa kujiuzulu ili kuihitimisha serikali ya awamu ya 5, ama, 2. Samia alipaswa kulivunja Baraza la Mawaziri kuihitimisha serikali ya awamu ya 5, na kuunda Baraza jipya la serikali ya awamu ya 6, hata kama angewateua Mawaziri wale wale.

Endapo rais JPM angefariki baada ya miaka mitatu madarakani, then ndipo Samia angeapishwa kwa kuwa rais wa 6, na kuiendeleza serikali ya awamu ya 5 hadi kuihitimisha ile 2025. Hapa ndipo serikali haikupaswa kuvunjwa. Na Samia baada ya kuihitimisha ngwe ya pili ya serikali ya awamu ya 5, 2025 ndipo angeanza na serikali yake ya awamu 6 yenye vipindi vyake viwili adi 2035!.

Kuna watu wanadhani rais Samia ni lazima agombee 2025 ili kukamilisha awamu yake ya pili, no!. Kufikia 2025 Samia anaweza kuona imetosha na akaamua 2025 hagombei urais, ila Watanzania tumeamua 2025 twende na mgombea mwanamke not necessarily Samia.

P
 
Asante mkuu, nilikuwa naomba kifungu cha Katiba
 
Katiba inasema kama amerithi zaidi ya nusu,ataweza kugombea mara moja tu... ila kama angekuwa amerithi chini ya nusu, angegombea mara mbili. Kwahiyo Mama kama mambo yataenda sawa sawa atagombea mara moja tu mwaka 2025. Mwaka 2030 tutakuwa na Rais mpya, unless watuletee habari za "atake asitake"
 
JF the great thinker? Bado siamini kama kweli JF Ina great thinker.
 
Kweli watanzania ukitaka kuwaficha kitu kiweke kwenye kitabu.
Kumbe watu hamna kitu kabisa
Wanataka Katiba mpya hata hii ya zamani hawaijui.
Wacha tu niwasaidie bure.
Samia amechukua kipindi Cha Magufuli kikiwa fresh kabisa
Kwa hiyo kile kinahesabiwa ni utawala wake alafu atagombea tena miaka 5
Atakuwa amemaliza kama akishinda

Ila ingekuwa Jiwe kafa 2024 Mama angemalizia 1 wa kipindi Cha mpito tuingie kwenye uchaguzi akishinda anaanza her fresh period akishindwa anaenda kulala
 
Acheni kupotosha,huyu ni rais wa.sita lakini awamu.ya tano.Mnasema ni rais wa awamu ya sita kwani Kuna uchaguzi ulifanyika tofauti na ule wa October 2020 ?
Hii ndio sahihi

Rais wa sita awamu ya tano
 
Awamu ya samia itaanza after 2025 yaani awamu ya sita kipindi cha kwanza

Nae hatoimaliza atakuja rais wa 7 awamu ya sita kipindi cha pili

Mfano rahisi tu refa anacheza dakika 90 sasa kwa bahati mbaya katika ya mchezo akapata jeraha refa mwingine ataingia sio!? Sasa inamaana mchezo uanze tena dakika ya kwanza[emoji2]

Wanazi mnatabu sana[emoji2]


Tuelewane hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…