Rais Magufuli angefariki mwaka 2024, Samia angemalizia mwaka 1 uliobaki au angetawala miaka 5?

Hakuna cha awamu ndugu, CCM ni walewale tu.
 
Acheni kupotosha,huyu ni rais wa.sita lakini awamu.ya tano.Mnasema ni rais wa awamu ya sita kwani Kuna uchaguzi ulifanyika tofauti na ule wa October 2020 ?
Rais akishakula kiapo inaanza awamu nyingine. Anaingia na timu mpya kabisa, na anakuwa na hulka zake za kisiasa anazoziamini hivyo unakuwa ni mwanzo wa awamu nyingine.
 
Nipe basi hicho kifungu mkuu wangu, usitujaze maneno tu
 
Hicho kifungu kinachosema hivyo mbona hamkitaji? Kuna mwingine kaniwekea kifungu feki
 
Ma wewe ukifariki 2024 utatawaliwa miaka mingapi na yeyote yule?
 
Ne hatomaliza muda wake [emoji85]
 
Usishangae wakamng'oa 2025 wana hasira naye mbaya
 
Usishangae wakamng'oa 2025 wana hasira naye mbaya
Hawana ubavu huo, majalada ya kufungulia kesi za utakatishaji hayajaisha, Sasa hivi wanakusanyiwa compromising information, akinyanyua kichwa anaonyeshwa uhalifu wake wote, na maoni ya DPP kwamba jalada liende mahakamani, na dhamana imetolewa hati ya kuizuia
 
Hakuna ziwa na kaskazini zitamng'oa maza hana mvuto kabisa wa kisiasa tukiacha unazi japo wana jaribu kumbrand lakini hakuna kitu
 
Endelea kuota, ziwa asilimia 79 ni kijani, labda wale walima bangi wa Tarime
Thubutu, wale jamaa wajanja sn hawaitaki CCM walikuwa wanamtaka jiwe sababu ya ukabila, kuna sumu ya ubara na uzanzibar inatembea utaona.
 
Huwa nasoma sana katiba, na sijaona popote katiba inapozungumzia habari za awamu! Sana sana inazungumzia suala la vipindi ambavyo mtu anaweza kuchaguliwa na kushikilia kiti cha urais.

Lakini kwa kuangalia muktadha wa thread hii, Ibara ya 37(5) inaeleza wazi kwamba:-
Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40
Na tena kwa kuangalia muktadha wa thread husika, Ibara ya 40 iliyotajwa hapo juu inahusisha kifungu kidogo cha 4, yaani Ibara ya 40(4) inayosema kwamba:-
Hivyo basi, sehemu ambayo sija-highlight hapo juu ndiyo inajibu swali lako kwamba:-
Kwamba, kwavile katiba yetu inatoa ruhusa ya mtu kugombea MARA MBILI TU, na kwavile SSH kwa sasa katiba inamruhusu kugombea MARA MOJA TU, basi tukiendekeza habari za AWAMU hii tutaita AWAMU MPYA (ya 6)!

Ni kutokana na hilo, na ndo maana katiba itamhuruhusu kugombea mara MOJA TU, kwa sababu muda atakaokaa madarakani kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) unatosha kuwa awamu inayojitegemea.

Na haiwezi kuingia akilini kwa mfano, 2025 SSH asimame jukwaani halafu mapungufu ya serikali yake yeye akiwa kama Rais aje kumdondoshea jumba bovu JPM kwa sababu atakuwa ameongoza kwa muda wa kutosha kurekebisha pale ambapo anadhani alikuta pana kasoro!

Kinyume chake, kama JPM angefariki 2024 na hivyo SSH kushika kiti kwa mwaka mmoja tu, muda huo hautoshi kuwa awamu inayojitegemea na ndo maana anapewa fursa ya kugombea upya mara mbili.

Hapo hata angetaka kumdondoshea jumba bovu JPM in 2025, angekuwa na uhalali wa kufanya hivyo bila kujali kwamba alikuwa VP.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…