Rais Magufuli, Anza na Kusaini Hati za Wote Waliohukumiwa Kifo, Wanyongwe Haraka Haraka Mpaka..

Rais Magufuli, Anza na Kusaini Hati za Wote Waliohukumiwa Kifo, Wanyongwe Haraka Haraka Mpaka..

hivi, ungekuwa na mtoto wako amehukumiwa kunyongwa, au hata amekamatwa china alafu unamsikia kiongozi wako uliyempigia kura anasema wanyongwe haraka, utajisikiaje? uchungu wa mwana anaujua mzazi. wakati mwingine mtu akiwa madarakani watoto wake wanasoma ulaya, wanakula vizuri, wanalindwa na mabodigadi hawapati shida yeyote anasahau kuwa kuna watu wameugua hadi bp kwasababu ya watoto.alafu leo unatangaza kwamba wanyongwe, si ndo wazazi wao bp zitapanda zaidi? tuwe wakweli tusipepese macho.

yatupasa kupigana vita hii kwa kukata mzizi. hao mapunda sio target kubwa sana na walitakiwa hata adhabu wapunguziwe, ila hao matajiri ndio wabaya. hata hivyo, hata kama angekuwa tajiri, kuamuru mtu anyongwe ni ukatili wa hali ya juu sana and i hope legal and human rights centre wanaopambana kupinga adhabu ya kifo kwamba ni ya kikatili watalisemea hili. badala ya kuokoa maisha ya mtu unaamuru anyongwe, halafu akinyongwa yule aliyedhurika atarudi kwenye hali yake?
acha upunda ndugu fanya lile lililo halali...naona unalalama lalama tu hapa mbona utuambii kuwa huyo aliekamatwa china pia alipeleka sumu ili wenzie wafe,ukiburi wako ndo umauti wako utachezea tanzi tu.
 
Muwe mna summary. Hakuna muda wa kusoma yote hayo. Cjui shule mlienda kufanya nini
 
Mkuu leo Wewe ni wa kusema kuwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ni " dhaifu katika mambo makubwa? " Hivi Wewe ni Pascal Mayalla huyu huyu ninayemjua au ni jina tu? Sasa naanza kuamini kuwa kumbe siyo kila Mtu anayekuchekea au kukusifia anakupenda kweli bali Wanadamu hasa Watanzania tumejaa ' Unafiki ' sana. Pascal Mayalla hivi zile ' favors ' zote huyo huyo uliyemdharau hapo alikuwa akikupa hadi kupelekea jina lako kukua na kupata ' michongo ' mingi ya ' kimtonyo ' na kutoka Kimaisha leo hii ndiyo ' Shukran ' yako Kwake? Hakyamungu Duh!
Mkuu Gentamycine, hapa duniani kuna sheria moja tuu ya haki bin haki inaitwa "karma", ambapo kila mtu atalipwa kwa kadri ya matendo yake, ukifanya mema unalipwa mema na ukifanya maovu unalipwa ubaya.

Vivyo hivyo sisi binadamu tunapaswa kutenda mema na kutendeana mema, ukitendewa mema kama ambavyo mimi nimetendewa na Kikwete, ninapaswa kumlipa mema, hivyo hata bandiko hili no matter nimeandika nini kumhusu Kikwete, kinachomatter kwenye karma ni dhamira, the motive behind, hata kama umeutaja udhaifu wa mtu kwa nia njema, hauhukumiwi na karma.

Nimeyaandika haya kwa nia njema na dhamira safi, yaani in good faith and clear conscious!.

NB. Paskali sio mtu wa kujikombakomba kwa yeyote wala kutegemea favours zozote toka kwa yeyote. Nimesoma darasa moja na mtoto wa Ben, nikiwa Chuo nilikuwa na R1, hapa nilipo kila nikienda Chato nafikia kwa Magufuli. Whatever I do, I do as a deserving and not as a favoured or under any preferential treatment!.

Paskali
 
Muwe mna summary. Hakuna muda wa kusoma yote hayo. Cjui shule mlienda kufanya nini
Mkuu Musoma Yenu, kama hii tuu umeona ndefu, makala kwenye magazeti utasoma kweli?,magazines jee utagusa?,vitabu jee? . Kiukweli Watanzania ni wavivu kusoma, jee uliwahi kusoma kitabu kinaitwa Alfu Lela U Lela? .
Headline imesema kila kitu, intro ikamalizia.
Hizi FB, insta na WhatsApp zinawaharibu sana vijana wetu.

Paskali
 
Mwandishi gani unaandika vitu kama hivi au unataka upigiwe pande na nakonda?? eti kikwete alikuwa dhaifu kwa mambo makubwa! you are not serious mkuu.


You better repent and turn back to your creator!
 
ha! we inakufaidisha nini..?
halafu mbona umekomalia au una lako jambo..
ingelikuwa mmoja wa ndugu yako yuko kwenye hilo kundi ungejisikiaje.. haya mambo hayahitaji haraka wengine humo usikute wamebambikiwa na wewe unasapoti tu.

kwa maamuzi ya mkulu jinsi yalivyo mi naomba apunguziwe baadhi ya madaraka maana tutaisoma kwelikweli
Unatakiwa uende xtra mile kuelewa fasihi aliyotumia Pascal Mayalla ,nadhani anajaribu kusema ukiwa Rais unatakiwa uwe makini na kauli zako!
 
Kuna hatari akapiga risasi watu adharani has a nyie mnaoandika vitu mbofu mbofu kama hivi vya kumfundisha kazi paskali ohoo shauri yako mi simo!
 
Mkuu Gentamycine, hapa duniani kuna sheria moja tuu ya haki bin haki inaitwa "karma", ambapo kila mtu atalipwa kwa kadri ya matendo yake, ukifanya mema unalipwa mema na ukifanya maovu unalipwa ubaya.

Vivyo hivyo sisi binadamu tunapaswa kutenda mema na kutendeana mema, ukitendewa mema kama ambavyo mimi nimetendewa na Kikwete, ninapaswa kumlipa mema, hivyo hata bandiko hili no matter nimeandika nini kumhusu Kikwete, kinachomatter kwenye karma ni dhamira, the motive behind, hata kama umeutaja udhaifu wa mtu kwa nia njema, hauhukumiwi na karma.

Nimeyaandika haya kwa nia njema na dhamira safi, yaani in good faith and clear conscious!.

NB. Paskali sio mtu wa kujikombakomba kwa yeyote wala kutegemea favours zozote toka kwa yeyote. Nimesoma darasa moja na mtoto wa Ben, nikiwa Chuo nilikuwa na R1, hapa nilipo kila nikienda Chato nafikia kwa Magufuli. Whatever I do, I do as a deserving and not as a favoured or under any preferential treatment!.

Paskali

Yale Mashati yako ya PPRA huna hata ya akiba unipe na Mimi mojawapo? Nayapenda sana Mkuu japo naona yote ni XXL wakati Mimi ni ' Kimbaumbau ' tupu.
 
paschal ungekuwa wewe mfano uko gerezani na umehukumiwa kunyongwa ,halafu nje kuna debate inaendelea unyongwe Au usinyongwe, nadhani ungeelewa na kwa akili yako ungekubali bora unyongwe ,ila sikufichi kuna waliohukumiwa kunyongwa bado wanaamini IPO Siku wataachiwa huru, inahitaji uvae uhusika then ndo utoe mchango wako
 
kwa mheshimiwa na Mimi namuomba awAnyonge tu kama wale wa ughaibuni kwa sheria za nchi husika huko
 
Mkubwa mmoja aliyepungukiwa akili na kwa sababu ni limbukeni kila kitu anakimbilia ku sign haraka haraka ha ha kasheria ka vyombo vya habari aisee
 
Hoja ya Paskal ni kwamba Rais karuhusu watanzania walioshikiliwa nje ya nchi na kuhukumiwa kunyongwa basi wanyongwe na balozi zetu zisihusike kabisa kufuatilia. Maana yake ni machungu kwa wale wenye ndugu zao huko nje hata kama walikosa.

Ila kuonesha jinsi dhana ya unyongwaji ilivyo ngumu kwenye utekelezaji Mh Rais ameombwa na PAskal aanze yeye kutekeleza hukumu z kifo kwa wafungwa waliopo nchini.

"Dont do unto others what you wouldnt like them to do unto you" maana yake Usimfanyie mwenzio kile ambacho wewe usingependa Kufanyiwa
 
Wenzetu ulaya na marekani waliokubuhu kwenye sayansi,hasa ya upelelezi,matumizi ya DNA wameanza kuwaachia baadhi ya waliohukumiwa kunyongwa,

Uchunguzi wa DNA ukifanyika upya,wanakuta aliyehukumiwa kunyongwa si muhusika taking accounpt uwezo mkubwa wa polisi kupika kesi.

Kama yeye anasahau idadi ya sheria(ile ya madawa)sembuse hii human justice inayofanywa na majaji
Hapo kwenye kupika kesi... Well said brother. Lakini mkumbuke huu uzi mnausoma kwa macho mawili... Pasco kaandika kifilosofia zaidi... Inahitaji jicho la tatu kumwelewa. Kwa wenye akili tumekuelewa Pasco... Yale mahubiri ya Mwakasege yaliyosambaa sana mtandaoni yanahusika hapa
 
Thread ya kumwaga damu hii.

Pascal kila siku Ninasema, nina wasi wasi na kiwango chako cha elimu.

Huwezi kuwa msomi alafu uandike na kushadadia dhambi kama hii
 
Hakuna binadamu mwenye haki ya kumuua binadamu mwenzio hata kama amekosea
 
Back
Top Bottom