Rais Magufuli aongezewe Ulinzi

Rais Magufuli aongezewe Ulinzi

Huyu Rais wa Watu, Kipenzi cha Watu aongezewe Ulinzi wa nini???

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nashauri kwa vile yeye ni kipenzi cha watu basi tutumie ile mbinu ya Osare Otango itakayo mfanya wakati mwingine anaweza kupita mahali bila kuonekana. Au tumuulize mtoto wa shehe Yahaya jee ule ulinzi usioonekana hauwezi kupewa huyu mzee wetu? Wakipatikana majini kama ishirini hivi atakuwa salama kuliko hata yule wa Korea Kaskazini.
Tumempenda wenyewe, hivyo tufanye kila tuwezalo hata kama ikibidi asafiri kwa ungo
 
Ili mpotee harakaharaka nyinyi wabnafsi
Kama wapo wanaohitaji ulinzi ni Watanzania wanaodai utawala bora unaozingatia sheria na kuheshimu Katiba. Watanzania tunahitaji maombi na ulinzi dhidi ya vitendo vya dikteta uchwara.
 
Naviomba vyombo vya ulinzi nchini vimwongezee ulinzi rais Magufuli,apewe ulinzi mkali wa wanajeshi kutoka vikosi maalum waambatane naye popote anapokwenda kufanya ziara.

Hatua anazozichukua za kupambana na kila aina ya ufisadi dhidi ya fedha za umma na rasilimali za taifa zinaweletea maumivu baadhi ya watu,zinawafanya wapoteze ulaji waliouzowea,wanachukizwa na wanaweza kufanya lolote.

Tunaomba rais aimarishiwe ulinzi mzito.
Sawa mkuu tumekuskia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakuwa anatuma watu wake ili kuzijua nyumba za watu wa vyama vingine kisha anatuma watu wake kuzibomoa na zinapofikiwa za watu wa ccm anamtuma mtu wake eti alikuwa hajui kama kunazoezi la bomoa bomoa hivyo anasitisha ubomoaji kwa hao watu wa ccm wala asihofu yy abomoe tu wala hakuna mtu wa kumfanya chochote ila jibu atalipata kwa mwenyezi MUNGU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada kwanianjema aliyonayo angeongezwa kwenye kikosikazi cha ulinzi wa amirijeshi wetu
 
Kama anatafutwa hivyo ajiuzulu tu, asituharibie hela, hatuna uwezo wa kumlinda zaidi ya hapo hasa ukimwangalia rais mwenyewe sio productive ni mtafuta kick tu, huku akiliingiza taifa hasara.
 
What so special kwa kuitia nchi hasara.Aya endeleeni kutoa ushuzi kwakua amewapa ulaji.
 
When it comes to JPM you become something else brother.
Angekuwa mtu mwingine ungemwambia athibitishe.
Kwa nini nihitaji uthibitisho kwa kitu ambacho kina uthibitisho tayari?

JPM kauza nyumba za serikali kinyume cha utaratibu kwa mdogo wake na hawara wake, kama huo si ufisadi ni nini?

Hiyo ni case moja tu, sijaingia kwenye ujinga wa madeni aliyosababisha kwa serikali.

Unamtetea?
 
Usifikiri uko mbali sana! Angalia usijepotea!!
Nisijepotea wapi?

Angalia wewe usiwe ndiye uliyepotea katika pango la kiza ukiniasa mimi nisije potea.

Jenga hoja, usijenge hofu.
 
Mnapoteza muda bure, unamwomba nani sasa wakati yeye ndio amir jeshi, we usizunguke mwambie ajifunze kuishi na watu. Wenzie walikuwa wanakwenda kunywa gahawa uswahilini bila ulinzi.
 
Nisijepotea wapi?

Angalia wewe usiwe ndiye uliyepotea katika pango la kiza ukiniasa mimi nisije potea.

Jenga hoja, usijenge hofu.
Utapotea gizani kwa kuwa unaongea ya gizani..!!
 
Back
Top Bottom