Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Utatumika na Taifa Stars.. Habari njema ni kwamba Uwanja Hauwezi kuoza kama wali wa nazi ulio changanywa na maharagwe.

Hiyo Taifa Stars yako inacheza hapo Uwanja wa Taifa mara ngapi kwa mwaka? Hizi ndizo AKILI mbovu ambazo kila kukicha huwa ' nagombana ' nazo humu JF. Labda kwa faida yako tu na wale ' wavivu ' wenzio wa KUFIKIRI ni kwamba Kiufundi kabisa ' uimara ' wa Uwanja wowote hasa katika zile ' nyasi ' zake pia hutegemea kutumika mara kwa mara. Mtafute hapo ulipo ' Mtaalam ' yoyote wa masuala haya ya Uwanja akuelimishe zaidi juu ya matumizi ya Uwanja wa kuchezea mpira.
 
Baada ya Uharibifu mkubwa wa Viti vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliokuwa unafanywa mara kwa mara na Mashabiki wanaoongozwa kwa Mihemko, Hasira na Matumizi yatokanayo na vilevi vikali kama Bange, Mirungi, Viloba n.k yaani Mashabiki wa Simba SC kwa nyakati Tofauti Tofauti umesababisha wizara husika kupitia waziri Nape Nnauye kupiga Marufuku klabu za Simba SC na YANGA SC kutumia uwanja huo kwa mechi za LigiKuu kuanzia hivi leo.
Haipiti mwezi mmoja utafunguliwa
 
image.jpeg
Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga,Nnauye anasema jana alipigiwa simu na Mh.Rais JPM na akawa amekasirika sana kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili,upande wa nje karibu mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 zimeharibiwa.

Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.

Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.

Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii"

.Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.Serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga.Mfumo ulionyesha kushindwa kabusa kabisa.Mpaka saa kumi jioni,upande niliokuwepo watu karibu 500 kadi zao zilikuwa zinagoma.

Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.
 
Timu za taifa zitatumia.......na ndo lengo lake haswaa...Simba na Yanga zinapaswa kuwa na viwanja vyao

Kuufungia uwanja wa Taifa ni maamuzi ya kiprofesa Maana hapa nchini maprofesa ni watu wanaoongoza kwa maamuzi ya kipumbavu zaidi mfano yule profesa aliyejifungia pale Buguruni.

Timu unazozifungia zisiutumie uwanja wa Taifa ndizo zinazowamiliki wachezaji wanaolitumikia Taifa kwenye timu ya Taifa,itakuaje sasa na timu zikiamua kuzuia wachezaji wake wasitumike kwenye timu ya Taifa?Ikiwa timu zetu zikiichukulia marufuku hiyo positively,na zikaamua kuwekeza nguvu zao kwenye ujenzi wa viwanja vyao,uwanja wa Taifa unaweza kuwa gofu na kutumika kwenye matukio ya serikali tu.

Serikali lazima itambue kuwa hao inaodhani inawakomoa ndiyo wenye mpira wao,wakiamua na wao kutunisha msuli yanaweza kutokea makubwa zaidi.
 
the order to be reversed, I am thinking toward that corner
 
Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga,Nnauye anasema jana alipigiwa simu na Mh.Rais JPM na akawa amekasirika sana kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili,upande wa nje karibu mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 zimeharibiwa.

Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.

Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.

Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii".Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.

Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.
duuuuuuuuuuuuh
 
Wapuuzi sana hawa Mashabiki wa Simba aisee! Sijui waling'oa viti kumkomoa Yanga, TFF au Serikali?

Na bado ' tutang'oa ' sana tu na hivyo Viti vikiisha sasa ' tutang'oa ' hadi meno ya Marefarii na Washika vibendera. Martin Sanya na TFF ya Malinzi hili wanahusika nalo 100%. Tutaheshimiana sasa ' kudadadeki '.
 
Uhamus wa propesa lipumba!

Mechi gani yenye uwezo kujaza mashabiki kama hiyo ya SIMBWA na NDALA!
Ungewapiga fain na wafanye matengenezo! Afu unawapiga ban ya muda na sio kuzuia moja kwa moja!

Huu uwanja labda uwe matamasha!
 
Kuufungia uwanja wa Taifa ni maamuzi ya kiprofesa Maana hapa nchini maprofesa ni watu wanaoongoza kwa maamuzi ya kipumbavu zaidi mfano yule profesa aliyejifungia pale Buguruni.

Timu unazozifungia zisiutumie uwanja wa Taifa ndizo zinazowamiliki wachezaji wanaolitumikia Taifa kwenye timu ya Taifa,itakuaje sasa na timu zikiamua kuzuia wachezaji wake wasitumike kwenye timu ya Taifa?Ikiwa timu zetu zikiichukulia marufuku hiyo positively,na zikaamua kuwekeza nguvu zao kwenye ujenzi wa viwanja vyao,uwanja wa Taifa unaweza kuwa gofu na kutumika kwenye matukio ya serikali tu.

Serikali lazima itambue kuwa hao inaodhani inawakomoa ndiyo wenye mpira wao,wakiamua na wao kutunisha msuli yanaweza kutokea makubwa zaidi.
Wachezaji kutoka azam, mtibwa nk watacheza timu ya taifa na sio lazima watoke simba na yanga. Kumbuka club yoyote hairuhusiwi na FIFA kumkataza mchezaji kuitumikia timu yake ya taifa. Hivyo basi simba wala yanga hawana uwezo wa kumkataza mchezaji asichezee Taifa stars endapo mchezaji mwenyewe akiamua. Uwanja wa taifa si wa simba wala yanga kwa hiyo ni jukumu lao hizo timu husika kutafuta viwanja vyao. We huwezi kukodi nyumba ya mtu uanze kuharibu miundo mbinu yake halafu mmiliki akuvumilie tu.
 
Wakati mwinyi yupo rais wa tanzania aliwahi kuhudhuria mechi ya simba na yanga

Ile mechi haikumalizika mwenyekiti wa yanga wakat huo bw tarimba aliamuru timu yake itoke nje kabla ya mpira kwisha

Mwinyi alichukulia ni hali ya mpira tu

Magu angefanyaje...
 
Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga,Nnauye anasema jana alipigiwa simu na Mh.Rais JPM na akawa amekasirika sana kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili,upande wa nje karibu mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 vimeharibiwa.

Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.

Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.

Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii"

.Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.Serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga.Mfumo ulionyesha kushindwa kabusa kabisa.Mpaka saa kumi jioni,upande niliokuwepo watu karibu 500 kadi zao zilikuwa zinagoma.

Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.
Hapo mkulu kakamapa pabaya simba na yanga huwa hawajalibiwi.
 
Back
Top Bottom