Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

RELATED HISTORICAL EVENT: Mwaka 1980 kulitokea fujo uwanjani wakati wa mechi ya kimataifa kati ya Tanzania na Ethiopia katika Uwanja wa Taifa (kwa sasa Uhuru). Rais Nyerere alikuwa uwanjani kama mgeni rasmi. Rais Nyerere alipoona wachezaji wanaanza kushikana mashati alinyanyuka ghafla na kuondoka na hadi kifo chake hakukanyaga tena uwanjani kwa lengo la kuangalia mechi ya mpira.
 
Adhabu mkurupuko kwann wasicheze Neutral ground hata mwaka???
Tuone kama akina kichuya watapanda jukwaani kung'oa viti
 
Hizi simba na yanga zifungiwe hata ule uwanja wa Uhuru.Ni aibu kwa hivu vilabu kutegemea viwanja vya serikali.
 
Ukiangalia sana hiyo ni sehemu ya hujuma, hivyo kila timu igharamie ukarabati wa hivyo viti na mechi zao wacheze uwanja wa Uhuru mpaka hapo kila timu itakapokamilisha ujenzi wa uwanja wake.

Pili, huyo mzabuni hawezi kujaribu tiketi kwa mechi kubwa kama hiyo, na kwanini ajaribu tiketi?

Yaani kuna baadhi ya watanzania ni watu wa ajabu sana.
 
Si kuna fedha zilipatikana katika viingilio kabla ya kugawana zighalimie matengenezo.
Lakini pia mashabiki waache mambo ya kizamani.
 
Hiyo tunaita tit for tat!! Natamani hapo aliposema "Rais alitaka adhabu iwe kali zaidi" nilitamani kuijua hiyo adhabu! Kutumia uwanja wa Taifa kwa Simba na Yanga ni ili kupata mapato mengi na kutangaza timu hizo nje ya nchi. Sidhani kama adhabu hiyo ya kuzifungia kuutumia huo uwanja ni sahihi.

Pili swala la kuzuia mapato ya timu hizo liangaliwe kwa umakini maana kuna wachezaji wengi hapo ndipo wanapoponea kwa swala la posho za hapa na pale kama kina Kichuya. Hivyo kuzuia mapato yote na hasa kwa style ya serikali ya Magufuli huenda tathimini hiyo ikachukua muda na baada ya hapo huenda wakaambulia hewa maana tutaambiwa mengi. Swala la kufanyika tathimini mpaka sasa lilitakiwa liwe limeisha. Pia mambo ya vurugu na vitu vya kwenye mipira ya miguu ni la FIFA na huwa wanakasirishwa sana pale serikali inapojiingiza moja kwa moja kama hivi.

Hapo kwenye adhabu Kali nawaza labda alipanga kuzifuta Simba na Yanga nini?

Any way adhabu kama hizi kwenye mataifa yenye misimamo mikali zilikuwa za kawaida na baada ya muda michezo kwenye mataifa hayo ikafutikia mbali!!
 
Watatumia uwanja gani? Wekeni njia mbadala za
kutatua matatizo kama ya kadi, kuwaelimisha mashabiki na wakifanya uharibifu basi mzuie pesa zao lakini sio kusema wote waadhibiwe kuto tumia uwanja wa taifa sabb ya wavuta bangi wachache.....
Washabiki wa Dar wapewe adhabu, mechi za simba na yanga zipelekwe mikoani ambako hamna viti kama kirumba, waende wakabomoe lile zege la kukalia.
 
Waamuzi nao wanachangia kwa kiasi kikubwa huu ujinga kutokea. Nao wapewe adhabu kali. Na hasa kufungiwa maisha.
 
ila wale mashabiki wa simba ni watu wa ajabu sana ustaarabu zero, walipe tu
 
Simba ijenge uwanja wake ili wapate mapato ya kutosha tofauti na hapo watakuwa wanainufaisha nchi tu kila mechi yao ichezwapo
 
Wakati Al marhum Mzee Karume alipokuwa Rais wa ZNZ aliamuru timu ya Mwadui waondoke haraka ZNZ kwa kucheza rafu uwnjani.Mpira ulikuwa bado kwisha wakapelekwa Airport moja kwa moja bila ya kupitia hotelini
 
Naiomba serikali iwafungie tu hawa washenz wanaotuhalibia uwanja wetu kuna mijitu sijui ipoje mamakezao sijui ni laaaana ama nini hivi kweli uwanja umenjengwa kwa mabilion ya pesa kwa ajili yao afu lijitu linakuja kufanya ujinga ni kwa maslahi ya nani sasa. Halafu uwnja ukiharibika yao yenyewe ndio ya kwanza kuanza kulalamika ***** zao hawa
 
Duuh hapo itabidi waende uhuru ambako pitch yake ni mbovu sana ile.
Na vilabu vyetu vipate akili vijenge viwanja zao sasa naamini ule ungekuwa uwanja wa simba ingekuwa ni ngum washabiki kung'oa viti hata kama wana hasira kias gani
wajenge vyao , wao kazi ni kula hela tu.
 
Mimi nilikuwapo uwanjani Jana... Kuna shida sana pale katika logistics za kuingia uwanjani.. Yaani ili uingie ni mapambano.. Mashabiki, walinzi na polisi.. Inakosesha hata hamasa ya kwenda pale uwanjani. Huwezi kwenda na familia yenye watoto wadogo kwenye mechi za aina ile, ni hatari.

Nafikiri taratibu za namna za kuingia ziboreshwe ili kuondoa kero. Itafutwe namna nzuri ya mashabiki kuingia haraka bila kusababisha misururu mirefu isio na lazima, coz kwa maoni yangu ndio kitu kilichosababisha mageti kuharibiwa. Hili la viti nafikiri tukiwafungia mashabiki watajifunza. Kuzifungia timu sioni kama itasaidia, na vile vile ule uwanja utakuwa underutilised.. Kumbuka ni Yanga na Simba tu wanaweza kuujaza uwanja ule ukiondoa matamasha..
 
Watatumia uwanja gani? Wekeni njia mbadala za
kutatua matatizo kama ya kadi, kuwaelimisha mashabiki na wakifanya uharibifu basi mzuie pesa zao lakini sio kusema wote waadhibiwe kuto tumia uwanja wa taifa sabb ya wavuta bangi wachache.....
Kwani ni jukumu la serikali kuwatafutia Simba na Yanga mahali pa kuchezea.Klabu hizi zimekuwepo miaka mingi na zimelala kwa sababu serikali inafanya majukumu yao badala ya wao kujitegemea.Watacheza hata viwanja vya tandika huko ambako hakuna viti.Wanaudhi sana. Pesa yote hiyo ingeweza kufanya mambo ya maana kabisa.
 
Back
Top Bottom