RELATED HISTORICAL EVENT: Mwaka 1980 kulitokea fujo uwanjani wakati wa mechi ya kimataifa kati ya Tanzania na Ethiopia katika Uwanja wa Taifa (kwa sasa Uhuru). Rais Nyerere alikuwa uwanjani kama mgeni rasmi. Rais Nyerere alipoona wachezaji wanaanza kushikana mashati alinyanyuka ghafla na kuondoka na hadi kifo chake hakukanyaga tena uwanjani kwa lengo la kuangalia mechi ya mpira.