Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Faini alipe j mlinzi wa Tff avune alichokipanda ni refa wake aliyomtoa kifungoni!
 
Ndo uchumi wa dunia ya 3 kaka..... hata serikali kuna mengi tu hawajatenda... tunashare kilichopo....
Uko sawa kabisa lakini naamini humaanishi ku-share na matokeo ya uhuni wa baadhi ya watu.Wakijitokeza wahuni tuna-share kuwaadhibu.Bado nasubiri adhabu ta tff kwa hizi timu.
 
Kuna watu mtaiponda serikali kwa hili lakini mimi naiunga mkono 100%. Watanzania imejaa wajinga wengi sana, viwanja vikiwa hamna wa kwanza kulaumu serikali, sasa vimetengenezwa mnaanza tabia za nyani mnavunja viti makusudi, alafu waafrika wakiitwa nyani wanakua wa kwanza kulalamika, hehehe! hizi tabia ni za myama gani sasa?
Ivi wewe n sokwe au nyani??
 
View attachment 410879 Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga,Nnauye anasema jana alipigiwa simu na Mh.Rais JPM na akawa amekasirika sana kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili,upande wa nje karibu mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 zimeharibiwa.

Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.

Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.

Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii"

.Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.Serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga.Mfumo ulionyesha kushindwa kabusa kabisa.Mpaka saa kumi jioni,upande niliokuwepo watu karibu 500 kadi zao zilikuwa zinagoma.

Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.


Hapa ndipo ninapompendea Magufuli kwamba mapato yote yatazuiwa ili kurudisha gharama, hakika Pombe Magufuli (PhD) ameletwa na Mungu!
 
Timu za Yanga na Simba ni za ovyo sana. Miaka zaidi ya 50 hawana hata pitch ya mazoezi? Yaani zina fan base kubwa sana hata kwa Afrika Mashariki lakini lakini zinaendeshwa kama Toto Afrika au Mbao FC.
Hiyo iongezwe maana haitoshi.
 
Nashauri wanasimba au viongozi wa simba wasishtuke sana ikija madai makubwa ya marekebisho tuna haki ya kuomba third party valuer na kupata thamani halisi siyo ya kuletewa tu na wizara
 
Naiomba serikali iwafungie tu hawa washenz wanaotuhalibia uwanja wetu kuna mijitu sijui ipoje mamakezao sijui ni laaaana ama nini hivi kweli uwanja umenjengwa kwa mabilion ya pesa kwa ajili yao afu lijitu linakuja kufanya ujinga ni kwa maslahi ya nani sasa. Halafu uwnja ukiharibika yao yenyewe ndio ya kwanza kuanza kulalamika ***** zao hawa[/QUOTE

binti mzuri hivyo unatukana, haifai bna.
 
Nashauri wanasimba au viongozi wa simba wasishtuke sana ikija madai makubwa ya marekebisho tuna haki ya kuomba third party valuer na kupata thamani halisi siyo ya kuletewa tu na wizara
Sawa
 
Hiyo tunaita tit for tat!! Natamani hapo aliposema "Rais alitaka adhabu iwe kali zaidi" nilitamani kuijua hiyo adhabu! Kutumia uwanja wa Taifa kwa Simba na Yanga ni ili kupata mapato mengi na kutangaza timu hizo nje ya nchi. Sidhani kama adhabu hiyo ya kuzifungia kuutumia huo uwanja ni sahihi.

Pili swala la kuzuia mapato ya timu hizo liangaliwe kwa umakini maana kuna wachezaji wengi hapo ndipo wanapoponea kwa swala la posho za hapa na pale kama kina Kichuya. Hivyo kuzuia mapato yote na hasa kwa style ya serikali ya Magufuli huenda tathimini hiyo ikachukua muda na baada ya hapo huenda wakaambulia hewa maana tutaambiwa mengi. Swala la kufanyika tathimini mpaka sasa lilitakiwa liwe limeisha. Pia mambo ya vurugu na vitu vya kwenye mipira ya miguu ni la FIFA na huwa wanakasirishwa sana pale serikali inapojiingiza moja kwa moja kama hivi.

Hapo kwenye adhabu Kali nawaza labda alipanga kuzifuta Simba na Yanga nini?

Any way adhabu kama hizi kwenye mataifa yenye misimamo mikali zilikuwa za kawaida na baada ya muda michezo kwenye mataifa hayo ikafutikia mbali!!

Kama ni kutangaza hizo timu nje ya nchi basi hayo ni matangazo gani yasoisha miaka nenda rudi?

Pili, si lazima wachezaji walipwe mapato yanayotokana na mechi kama ya jana, kwani huo utakuwa ni uswahili.

Tatu, inaonekana huelewi miongozo ya FIFA kwa vyama vya soka, kwani kilichofanyika ni kosa la jinai la uharibifu na hilo halihusiani na kwenda uwanjani kuangalia mpira.

Mkuu, usiwe mrahisi kiasi hicho hata kwa upumbavu huu ulofanywa na hawa wahuni.

Uamuzi wa kuzuia timu hizo zisitumie uwanja huo ni uamuzi sahihi na unawapa timu hizo changamoto kujenga viwanja vyao na zianze kujitegemea kimapato.

Pia, unatoa elimu kwa hao wapumbavu na malofa kuheshimu na kuthamini kila kizuri kinachofanywa na serikali.
 
Ivi wewe n sokwe au nyani??
Hehe sina tabia za kuvunja viti kisa mpira, mtu mzima ana akili ya kujua hivyo vitu viwili havina relationship yoyote ile, ila nyani hatambui yeye ni fujo tu.
 
Kama ni kutangaza hizo timu nje ya nchi basi hayo ni matangazo gani yasoisha miaka nenda rudi?

Pili, si lazima wachezaji walipwe mapato yanayotokana na mechi kama ya jana, kwani huo utakuwa ni uswahili.

Tatu, inaonekana huelewi miongozo ya FIFA kwa vyama vya soka, kwani kilichofanyika ni kosa la jinai la uharibifu na hilo halihusianoi na kwenda uwanjani kuangalia mpira.

Mkuu, usiwe mrahisi kiasi hicho hata kwa upumbavu huu ulofanywa na hawa wahuni.
Kwani wapi nimeonyesha urahisi? Napinga uharibifu wa Mali na ni lazima walipe gharama ila natoa tu angalizo kuwa mambo yasiende kama kule kwa kina Mushobozi.. Kulipa ni lazima ila kwa swala la tathimini ni siku moja tu na siku ya pili taratibu za kukatana mapato zinafuata.. Sio kufanya mchakato wa mamiezi tena.
 
Tuko wanachama tuko tiyari kuchangia pakubwa tu kwenye faini ya timu yetu pendwa mnyama ila kilichofanyika ni fundusho kwa upuuzi wa ma refarii
 
Kwani wapi nimeonyesha urahisi? Napinga uharibifu wa Mali na ni lazima walipe gharama ila natoa tu angalizo kuwa mambo yasiende kama kule kwa kina Mushobozi.. Kulipa ni lazima ila kwa swala la tathimini ni siku moja tu na siku ya pili taratibu za kukatana mapato zinafuata.. Sio kufanya mchakato wa mamiezi tena.

Manji na Dewji wajenge viwanja vya hizi timu ili kama wakivunja viti kwenye viwanja vyao, basi linakuwa ni suala lao wenyewe bila kuwahusisha watu wengine.

Hivi mkuu, unafikiri yule mkandarasi aliejenga huo uwanja na hata mabalozi wa nchi mbalimbali ambao wamekwenda kukaa pale uwanjani hivi sasa wanatufikiria vipi sisi waafrika?

Uvunje viti mara uvunje vyoo!
 
Back
Top Bottom