Hili huwa nawaambia humu kila siku kwamba mahusiano baina ya mataifa hayana cha undugu wala nini ila maslahi, nyie ndio mnapenda kuwaita Wachina na kila taifa ndugu zenu, mnafaa mfahamu linapokuja suala la kujadili/negotiations biashara baina ya mataifa huwa ni mwendo wa kununiana hadi mahesabu yaende ipasavyo, ndio baada ya hapo watu wote mnakenua meno na kunywa divai na mvinyo.
Lakini hili suala la Bagamoyo limefanya nimeona kweli CCM yenu haina huruma na nchi hiyo yenu, humo kuna watu wapo tayari kuimaliza nchi ibaki mahandaki na majivu ilmradi wao wapate 10%, nafahamu hakuna mfumo dunia hii ambao hauna mafisadi ndani yake, hata huku kwetu wapo tu, lakini sikutegemea Kikwete na watu wa CCM walifikia kwenye level ya kuachia mikataba kama hiyo ya kuimaliza nchi nje nje.