Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Magu yeye alitaka Jk alaumiwe aonekane alikuwa anauza nchi. Wakati Jk hakuusaini kwa sababu ulikuwa kwenye mchakato. Ndio maana Deus anasema hatujaukataa bali tumewapa nasisi masharti yetu tunawasubiri.
Unazungukia kule kule tu. Magufuli aliukataa ulipoletwa kuidhinishwa, akaurudisha kwenye mchakato. Kikwete aliondoka kabla hajauidhinisha, yaani ukiwa bado kwenye mchakato. Kwa hiyo kumleta Kikwete kwenye jambo hilo ni kutafusa sababu za kulaumiana tu. Hata kama alikuwa ameshiriki hatua za awali, mambo yanayohusu mikataba ya ardhi ya Tanzania huidhinishwa na rais aliyeko madarakani!
 
Jamani tuwekeeni mkataba mezani mezani, ili kila mtu ajisomee...msilete hearsay'... kazi iendelee.
 
Wschina kwenye uwekezaji wa Bandari popote walipowekeza ni matatizo makubwa.

Wachina ni wanyonyaji sana.
 
Miaka 33 mingi sana ukizingatia on worst case scenario return on investment inarudi ndani ya miaka 15 na ikiwa mambo yameenda kama ilivyotarajiwa wanarudisha investment ndani ya miaka 10 tu.

So katika miaka 33 wanaweza rudisha hela yao na kuvuna ziada kati ya $12-24 billion extra.

Hiyo aiwatoshi wanataka free land lease of 99 years. Hiyo sehemu iwe kama ardhi ya China ndani ya muda wa huo wa mkataba. Wawekezaji wajiamulie wao ardhi waitumie vipi, akija mchina au mwekezaji yoyote kwenye hilo eneo wao ndio waamue ardhi itumike vipi na kama watauza hela ni yao pia.

Ndani ya muda huo pia wasilipe kodi kabisa za serikali, umeme na maji wapewe kwa bei nafuu.

Ni proposal ambayo alitakiwa arushiwe usoni raisi wao kwa hasira papo hapo what do they take us for; stupid Chinese.
 
Sio mradi ulejeshwe bali wawekezaji warudi tuendelee kubargain kwa terms zinazotufaidisha sote.
Bado una hamu ya kuendelea kubembelezana na hao wanyonyaji? hii unayoonesha hapa ni mental slavery, you need to emancipate yourself.
 
Halafu kuna wajinga hapa wanakwambia wachina warudi tukae nao chini, akili za namna hii ndio wakina Ndugai wanazipenda, mimi sitaki hata kuwaona hao wachina kwa hizo terms zao walitudharau sana, walitaka kuigeuza Tanzania iwe na mkoa wa wachina waendeshe biashara zao and eveything, kama ambavyo imetokea Djibouti.
 
Mkataba uwekwe hadharani wote tuusome na tuujue
 
I agree na huyo Kakoko is not ignorant he is very smart and realistic ya kwamba ipo siku sometime in 15-20 years kwa eneo la Dar bandari itafikia saturation point so they need another long term port plan.

Lakini si kujenga kwa proposal ya mchina kama ilivyo. Vinginevyo huo uwekezaji ufanywe na serikali yenyewe and it’s within their means I totally I agree with him.

Hapo hakuna cha ku negotiate zaidi ya kuwataka wachina kwenda TIC kuwekeza kwa masharti ya Tanzania kwenye ivyo viwanda; ila proposal ya bandari on its own should be scrapped entirely.
 
Nimependa hapo alipoelezea sio kwamba hiyo bandari ya Bagamoyo itakuja kushindana na hii ya Dsm, bali hii ya Dsm inaelekea kuzeeka kwa maana kwamba muda utafika haitakuwa na eneo tena la kujiongeza kwa ajili ya kukidhi mahitaji, ndio maana wakata ya Bagamoyo iwepo, lakini sio kwa terms hizo za mchina huo ni utapeli walitaka kutuletea, ndio maana haya mataifa yanaendelea kwa kusaini mikataba ya ajabu kama hiyo na wajinga wengine duniani.
 
Yale Mashart ndani ya Mkataba wa bandari ya Bagamoyo ambayo hatujawai kuuona Mkataba zaidi ya kusimuliwa Sasa yanaelezwa hapa,
Jameni, mbona hakuna mkataba? Nani kaona au kasikia mkataba katika maelezo hayo?

Haya yalikuwa ni mapendekezo ya upande mmoja; hata kama yalikuwa ni mapendekezo ya kipuuzi; lakini sio mkataba.
 
Hakusema hivyo mzee, alikataa kuupitisha
Atapitishaje mapendekezo ya upande mmoja, hata kabla ya 'counter proposal'?

Haya ndiyo maajabu ya nchi hii.

Hapa hapakuwepo na mkataba wa kupitisha au kukataa, ni mapendekezo tu ya upande mmoja wa wachina. Tanzania haijajibu lolote juu ya mapendekezo hayo na kuwasilisha majibu yao kwa wachina wayaangalie.
 
Hapa ni swala la Tanzania na hao wawekezaji; Tanzania ndiyo iliyokataa mapendekezo ya wawezekezaji kuwa hayakulingana na interest za Tanzania, je kuna upande gani mwingine ambao Tanzania ilitakiwa kusikiliza tena kabla ya kutoa uamuzi?
 
Magu yeye alitaka Jk alaumiwe aonekane alikuwa anauza nchi. Wakati Jk hakuusaini kwa sababu ulikuwa kwenye mchakato. Ndio maana Deus anasema hatujaukataa bali tumewapa nasisi masharti yetu tunawasubiri.
Huu ndio ukweli uliousema hapa.

Mkataba ulikuwa haujaandikwa na wala haukuwepo, na hata majadiliano yalikuwa bado hayajafanyika.

Lakini waTanzania leo tunapiga kelele hadi sauti inakataa kutoka kwa kitu ambacho hakikuwepo.

Haya mapendekezo yalikuwa ni mabovu, na inaeleweka, kwa sababu ni ya upande mmoja, ndiyo kwanza hatua za mwanzo kabisa.

Sasa tatizo ni hao waTanzania ambao wangiingia kwenye mazungumzo hayo, kwa sababu hiki kilikuwa ni chambo kwao kuwanasa na kuwalainisha..., hapa ndipo akina Ndugai walipo na maslahi napo.

Sasa watuonyeshe na yale mapendekezo ya mchina aliyokuwa ameyaweka kujenga SGR nayo tuyasikie.

Magufuli kadai alikataa "Mkataba" mbovu wa Bandari; lakini pamoja na kuwanyang'anya wachina ujenzi wa SGR kwa kukataa mapendekezo waliyoyatoa kwa ujenzi huo; lakini mbona aliwatafuta tena na kuwapa kipande cha reli wajenge kwa makubaliano mapya!
 
Hapa ni swala la Tanzania na hao wawekezaji; Tanzania ndiyo iliyokataa mapendekezo ya wawezekezaji kuwa hayakulingana na interest za Tanzania, je kuna upande gani mwingine ambao Tanzania ilitakiwa kusikiliza tena kabla ya kutoa uamuzi?
Kwa hiyo yalikuwa ni "Mapendekezo" sio "Mkataba" kama inavyodaiwa kila sehemu hapa.

Ndiyo, Tanzania ilikuwa na haki ya kukataa mapendekezo ya mwekezaji; lakini si katika kuwasilisha mapendekezo kuna majadiliano, au hakuna? Unaletewa mapendekezo, unayakataa hata kabla ya kuyajadili na kutoa maoni ya upande wako ili mwekezaji naye aelewe unasimamia wapi?
 
Kwani huo wa bandari ya Bagamoyo umewekwa wazi ?
 
JF kwenye hili la bagamoyo mnatumika kila siku uzi huu unapandishwa.
 
Semantics tu za kutokukukubali facts; ni mapendekezo ya kuweka mkataba! Magufuli hakufuta mkataba bali alikaa kuingia mkataba huo kwa mapendekezo hayo.
 
Ningekuelewa kama ungesema umeuina huo mkataba na kuusoma na hayo ndiyo mashariti yake. Lakini habari ya kusema Magufuli kasema huwezi kunishawishi niamini kuwa huo ndio ukweli.

Mara zote wanasiasa wetu wamekuwa sio wakweli wa kauli zao. Nikikumbuka jinsi mradi wa gesi ya mtwara ulivyopigiwa debe mpaka watu kuumizwa waliojaribu kuamdamana ili kuupinga inanifanya nikose imani na viongozi wanasiasa wa ccm haijalishi nani yuko madarakani.

Magufuli unayemsema wakati wa mradi wa gesi ya Mtwara hakuwahi hata siku moja kutuambia huo mradi haufai licha ya kuwa alikuwemo serikali na yeye alikuwa ni mmojawapo aliyekuwa anaupigia debe.

Alipopata Urais tu akaamua kuachana na huo mradi na kuelekeza nguvu kwenye mradi wa stieglers akisema kwamba huo ndio mradi mzuri kwani gharama za umeme zitakuwa nafuu ukilinganisha na umeme wa gesi. Umeme wa gesi wenyewe tuliambiwa utaleta nafuu sana lakini mpaka leo kuna nafuu yoyote uliyoiona?

Kama jibu ni hapana kwanini unaamini huu wa sieglers utakuwa nafuu? Je kwakuwa Magufuli kasema?

Turudi kwenye hoja ya msingi, miradi iliyoanzisha na Magufuli mashariti ya mikataba yake unayajua? Umeiona hiyo mikataba umeisoma ili uwe kwenye nafasi ya kulinganisha na hiyo mikataba mingine iliyoanzishwa na watangulizi wake?

Kama mikataba ya Magufuli hujaiona na yeye mwenyewe hakutaka iwekwe wazi kama mikataba mingine ya waliomtangulia je huo ujasiri wa kumwamini Magufuli unaupata wapi?

Usiongozwe na mapenzi yako kwa Magufuli kwenye masuala ya msingi. Siutetei mradi wa Bagamoyo lakini nashindwa siwezi kuyachukulia maneno ya Magufuli kuwa ndio ukweli wenyewe kwa asilimia 100 wakati yeye mwenyewe hajathubutu kutuonyesha tujue mashariti yake yakoje.
 
Kaka hawa jamaa ni wapuuzi sana.
 

Ni kweli kabisa Hongkong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…