Rais Magufuli ataka Polisi kumwachia mmiliki wa shule ya Waislamu Byamungu iliyoungua Kyerwa wakati wakiendelea na upelelezi

Rais Magufuli ataka Polisi kumwachia mmiliki wa shule ya Waislamu Byamungu iliyoungua Kyerwa wakati wakiendelea na upelelezi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Magufuli amelitaka Jeshi la polisi kumtoa mahabusu mmiliki wa shule ya Waislamu iliyoungua moto huko Kyerwa mkoani Kagera wakati wakiendelea na upelelezi.

Rais Magufuli amesema siyo rahisi mzee huyo anayemiliki shule kuwahujumu watoto anaowalea hivyo ni vema uchunguzi wa kina wa tukio hilo ufanyike yeye akiwa nje.

Juzi IGP Sirro aliagiza kukamatwa kwa mkuu huyo wa shule, afisa elimu na wakaguzi wa elimu kama sehemu ya upelelezi.

Chanzo: ITV

Maendeleo hayana vyama
 
Rais wa Tanzania, Dkt. @MagufuliJP
ameliagiza jeshi polisi kumuachia Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Islamic Byamungu, Kagera, ambaye anashikiliwa baada ya wanafunzi 10 kufariki kwa ajali ya moto. Amesema kumshikilia wakati uchunguzi ukiendelea kumuongezea uchungu zaidi.

Chanzo: swahili Times

Watoto 10 wamepoteza maisha baada ya Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyoko Kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera, kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2020.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa umri wa wanafunzi waliofariki ni kati ya miaka sita hadi 12.
Bweni lililoungua ni la wanafunzi wa kiume ambapo majeruhi 6 wamepelekwa Hospital ya Nyakahanga.

Screenshot_20200916-100737_Twitter.jpg
 
Back
Top Bottom