Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Wewe unaumwa. Waziri anasain regulations yeye hazitengenezi. Regulations zinatengenezwa na idara wenye sheria. Mfano, Sheria ya ardhi ikitungwa, regulations zake zinatengenezwa na Kamishana wa Ardhi hivyo waziri wa ardhi huperekewa kusain tu.
Wewe nawe ni mlevi mkuu,kwahiyo unashindwa hata kujua kwamba kutia saini ni kuidhinisha? Kutengeneza kanuni ni jukumu la waziri kupitia wizara yake,ukisikia waziri anatunga kanuni hatumaanishi anajifungia chumbani na kuzitunga bali wanatunga wengine yeye anakuja kumalizia tu kwa kuziingiza katika matumizi.

Mteteeni kivingine lakini sio kumchomoa katika hili!
 
JENISTER MHAGAMA MUST GO..

kabla hakujacha..

Huyo Jenista mganga wake ni huyo huyo wa Bashite. Huyo dada ni mshirikina balaa. Usiku huu huyo mganga lazima akalale hapo nyumbani kwake ili mkulu asimkumbuke kabisa
 
Kama vile naona
Dada Irene akipangiwa Uafisa Utendaji Kata

Baada ya Kuripoti kazini,
Kama namuona Dada Irene akilalamikia Kikokotozi cha 25% ya mafao kwa wastaafu.

Namuona staff mwenzie kutoka Mkoani Mara,
Kwa Jazba kali sana, Akimrukia na KUMZABA KOFI ZITO SHAVUNI.

So sad,
Afu Dada wa watu anabubujikwa na machozi[emoji24] [emoji24]

INAUMA SANA KWAKWELI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli huwa hapendi ujinga na watu kufanya kazi kwa mazoea. kauli ya hapa kazi tu inaendelea kuwa wazi na lazima ieleweke Magufuli anaposema hapa kazi anamaanisha nini anasema.

Alitia sahihi kukubali hiyo sheria ambayo mama wa watu alikuwa anaitekeleza, kosa la nani sasa kama sio la huyo anaejitia kutetea wastaafu leo? Kwani hayo malalamiko yalianza jana?
 
IMG_20181228_211934_062.jpg
 
Hivi alietakiwa kutumbuliwa ni alietunga mswada na kupeleka bungeni au wanao fanyia kazi kilichopelekwa na waziri ambacho.kimetoka kwa rais?huyu aliagizwa afuate sheria inasemaje yeye kafuata sheria ila alietunga sheria hiyo mbana haguswi?huu nao unaweza kuwa ni uonevu.angeanza na waziri ndo hao wadogo wafuate maana waliomdanganya ni mawaziri wake
 
Hawa watendaji ni shock absorbers tu wanasiasa wakichafua hawawajibishani.Mhagama na Katibu wake si wajiongeze tu ikibidi na bunge livunjwe warudi majimboni upya Ovyoo.
 
Bunge lilitunga sheria ambayo haina fomula ila waziri alipaswa kutunga kanuni ambazo zina fomula ikiwepo kikokotozi

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata huko bungeni, wabunge wa upinzani walipinga na kutoa tahadhari kwamba hiyo sheria ina nia ovu, na aliyeachiwa kutunga kanuni kapewa mwanya wa kutengeneza kanuni zenye nia ovu. Na hicho ndio kilichotokea. Rais, Bunge na wabunge wa ccm ni sehemu ya hii sheria mbovu, na sio hii tu, bali zilizopita na zitakazokuja. Kama hilo bunge litakosa wapinzani sheria nyingi kandamizi zitapita.
 
Ivi mfano dada Irene kama baada ya kikao kile akaamua kurudi zake nyumbani kupumzika,na jioni hii tumeona katumbuliwa inamaana iyo jumanne akienda ofisini kwake kwa zamani anaenda kuwa kama mgeni mwingine vile wa ofisi ama,Dada Irene kaumaliza mwaka vibaya kwa kutumbuliwa
 
Mfano irrelevant. Wapinzani walipiga kelele toka mwanzo. Unapokea nyumba mbovu, tena baada ya wataalamu (bunge) wako kupitia ubora wa nyumba na kusema wameridhika na ubora, wakati huo huo kuna wataalamu wengine (wapinzani) wanasema hiyo nyumba haina ubora, kwakuwa unaongozwa na upofu wa itikadi unaamua kuwasikiliza na kukubali kwa kuweka saini kwakuwa unawakubali hao wengi wajinga. Matokeo yake siku chache aibu inakukuta kwamba hiyo nyumba(sheria) kweli ni mbovu. Hapa wakulaumiwa ni rais na wabunge wa ccm. Ni sheria nyingi mbovu hupitishwa na wabunge wengi wajinga wa ccm.
Mfano unamhusu mkurugenzi. Najua masikio yako yanapenda kuambiwa kuwa rais ni mtu mbaya. Hili halishangazi! Ila kama rais angeingilia wakati wabunge wanapitisha wewe ungekuwa wa kwanza kusema analiendesha bunge kwa rimoti. Kwangu mimi rais amefanya vizuri sana kwani ameacha maji yafuate mkondo wake ili wengi tujue ni wapi kwenye ubovu na wapi kwenye ubora. Kwa hali hii wabunge waliopitisha hiyo sheria keshokutwa watatafakari kabla ya kupitisha mambo mengine.
 
Ajabu ni kwamba Maccm yalivyo ya hovyo ambayo yaliunga mkono Kikokotoo na Sheria Kandamizi yapo hapa Leo hii yakipongeza tena uamuzi wa Pombe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom