Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.
Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
>
Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
Irene Charles Isaka, Director General, Social Security Regulatory Authority - JamiiForums
Rais JPM alichosahau na watu wote wameanza kukisahau, wanasiasa wote wanaendelea kukisahau akiwezo Zitto Kabwe na Esther Bulaya mwanzishaji wa hoja ya kikokotoo ni suala zima la DENI LA TRILIONI 8 za uliokuwa Mfuko wa PSPF. Deni hilo halisemwi tena. Deni alilosema JPM kuwa limelipwa ni michango ya kawaida iliyokuwa imecheleweshwa kwa miezi kama 7 hivi kwa mifuko yote. Michango hiyo ipatayo shilingi 1.2 Trilioni haikuwa imewasilishwa kwa zaidi ya miezi 7 ya mwaka 2015 kutokana na Serikali kuwa busy na uchaguzi wa 2015. Hiyo michango haikuwa deni lote la Mifuko hasa PSPF. Michango ya shs 1.2 trilioni ni malimbikizo tu ya michango ya mwaka 2015 na siyo deni la zamani la PSPF na mifuko mingine tangia 1999. Kwa hiyo, wanaotoa taarifa kwa Rais ni vyema kumweleza taarifa zote kwa usahihi ili asije akawaza kuwa madeni yote ya Mifuko imekwisha na hivyo Mifuko inapaswa kulipa mafao kwa fomula kuuubwa ambayo haipo duniani kote kama alivyosema Rais mwenyewe.
Watu wanapaswa kukumbuka kwamba, mwaka 1999 Mfuko wa PSPF ulipoanzishwa kuna fedha serikali ilikubali kuzilipa ili kuwezesha Mfuko huo kuweza kujiendesha bila wasiwasi. Zaidi ya Bilioni 700 zilipendekezwa na watalaam ziingizwe PSPF mwaka huo 1999 ili Mfuko uweze kufidia naksi (deficit) ya michango ya wanachama wa PSPF waliokuwa hawachangii Mfuko wowote kabla ya Julai 1999 Mfuko huo wa PSPF ulipoanzishwa. Fedha hizo zaidi ya bilioni 700 zimeendelea kukua kwa asilimia na kufikia zaidi ya Trilioni 6 hadi sasa. Kwa nini wanasiasa wanasahau hoja hii?
Hoja nyingine muhimu ni hii hapa. Wanachama wa PSPF hadi kufikia 2017 Mfuko wao ulikuwa umefiliska kabisa kwa sababu ya tatizo hilo la tangu 1999 pamoja na Kikokotozi kinachochota fedha nyiiiiiingi kwa mtu mmoja anapostaafu kuliko uhalisia wa uchangiaji wake. Mfuko wa PSPF haukuwa na fedha kabisa hadi 2018 mifuko yote ilipounganishwa pamoja kuunda PSSSF. Kinachosumbua akili za wengi ni kwamba wanachama wa PSPF walioingizwa PSSSF wakiwa hawana fedha tena ili wakasaidiwe mafao yao kutoka mifuko ya wenzao LAPF, PPF, na GEPF, iweje sasa waendelee kulipwa kwa Formula ambayo inaendelea kuchota fedha nyingi sana kutoka kwa mifuko ya wenzao PPF, LAPF na GEPF? Na mbaya zaidi watu wanajiuliza; kwa nini wanachama wa Mifuko iliyokuwa imara kifedha hasa Mfuko wa PPF walipwe kwa Fomula ndogo wakati wenzao wanalipwa kwa fomula kuuuuubwa tena kwa kutumia fedha za PPF? Wadadisi wanaona kwamba hakuna usawa. Hakuna haki hapo.
Hoja nyingine inayopotoshwa ni hii hapa. Kwamba wanachama walipwe zote wakafe wenyewe na kwamba haingii akilini mstaafu kulipwa kwa 25% na nyingine alipwe polepole. Ukweli ni kwamba hii ndiyo kanuni ya uchumi. Kwenye kanuni ya uchumi haishauriwi wafanyakazi na wastaafu walipwe fedha zao zote wanazostahili kwa mkupuo kwani itaathiri mzunguko wa fedha na kuongeza mfuko wa bei nchini. Wastaafu ukiwalipa fedha zote wanazotakiwa kulipwa wakistaafu inaongeza mfuko wa bei (Inflation) na hatimaye wastaafu hao wanaingia kwenye matumizi ya anasa nyiiiiiingi tofauti na kama wangelipwa kidogokidogo. Hebu fikiria kama wafanyakazi walioajiriwa kwa mkataba wa miaka 5 kama wangelipwa mishahara yao yote ya miaka 5 halafu wakatakiwa wasikose kazini kila siku. Kama mtu analipwa shs 1,000,000 kwa mwezi alipwe fedha zake zote shs 60,000,000 sasa hivi na kisha atakiwe kuwepo kazini kila siku????? Inaingia akilini kweli. Sasa fikiria mstaafu anayestaafu leo na hatujui atafariki lini alipwe shs 150,000,000 zote badala ya 25% ya hizo unaona nini wewe kama mwanauchumi????
Nashauri masuala ya kitalaam waachiwe watalaam. Hifadhi ya Jamii yanahitaji utalaam. Wanasiasa waache watalaam wafanye kazi yao. Vyama vya wafanyakazi visiingilie ushauri wa kitalaam na waache watalaam wafanye kazi yao kitalaam. Wanasiasa wasiwe wa kwanza kuvuruga uendeshaji wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa sababu bila utalaam mifuko hii haitaweza kujiendesha kwa miaka mingi ijayo.
Mfuko mpya wa PSSSF naamini kwamba usipoendeshwa kitalaam utakufa mapema hata kabla ya kuanza kazi. Kama wastaafu wapatao 58,000 watastaafu miaka 5 ijayo hii tafsiri yake rahisi ni kwamba serikali inapaswa kuajiri watumishi wapya kwenye sekta ya umma wasiopungua 58,000 x 4 = 232,000 kwa miaka 5 ijayo kufikia mwaka 2023. Hii maana yake ni kwamba kwa mwaka watastaafu wapatao 11,600 watastaafu ambapo replacement yake (Retirees replacement ratio) kwa mwaka ni sawa na wafanyakazi wapatao 46,400 waajiriwe kwenye sekta ya umma na waingie PSSSF ili Mfuko uwe imara in terms of member-base ya Mfuko huo. Kama Mfuko utakosa wanachama wapya wapatao 46,600 kwa mwaka Mfuko huo wa PSSSF utaanguka mapema kabisa. Wote tujiulize swali; Je kuna ajira kwenye sekta ya umma sasa hivi? Je, kuna uwezekano wa PSSSF kupata wanachama wapya 46,600 kila mwaka kama replacement kwa wanaostaafu kwa mwaka?
Siasa na utalaam ni vitu viwili visivyofanana. Tuwe makini na maamuzi yetu.