Mawazo yangu yapo tofauti kidogo na wengi, wengi tunaangalia pale tulipodondokea na siyo pale tulipojikwaa. Nazani wote tulimsikia Raisi akisema mifuko haina pesa na ndio maana mamlaka husika(SSRA) ikaja na aina mpya ya kikokotoo ili kuokoa jahazi.
Swali la msingi la kujiuliza, Ilikuwakuwaje mpaka mifuko ikafilisika? Raisi aligusia kidogo kwamba kufilisika huko kulitokana na uwekezaji usio na tija mfano mradi wa Dege Eco village huko kigamboni.
Nilimsikia mhusika mmoja akisema mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa na kiasi cha trillioni 13 na hivi sasa wamebakia na trillioni 1 point something pekee, kwa kifupi trillioni 12 either zimewekezwa kwenye miradi ambayo haifanyi vizuri au kiasi kikubwa cha hizo fedha zimepigwa.
Hivi inakuingia akilini kweli trillioni 12 ziwekezwe kwenye miradi isiyofanya vizuri au zipigwe ilihali mamlaka zinazosimamia hii mifuko zipo(SSRA), waziri mwenye dhamana yupo, TAKUKURU IPO, CAG yupo, sasa kwa nini imechukua muda mrefu sana mamlaka zote hizi kugundua kwamba haina ya uwekezaji iliyokuwa inafanywa na hii mifuko haina tija?
Kumbuka kwamba hii mifuko inaendeshwa kwa kanuni na sheria, kwa hiyo sizani kama watendaji wa hii mifuko wanaweza kujiamulia tu kuchukua bilioni kadhaa na kuwekeza kwenye miradi kama wa Dege bila kuhusisha mamlaka husika zinazosimamia hii mifuko, na vile vile ndani ya hii mifuko kuna mavaluer na mauditors wakutathimini hii miradi na pia kutoa annual balance sheet kwa mamlaka husika inayoonyesha financial soundness of the fund, inakuwaje sasa hawa wote walishindwa kubaini hayo yote mpaka tunafikia huku?
Wengine wanasema hii mifuko ilikuwa sehemu ya serikali kujichotea pesa, binafsi sijui kama hilo Lina ukweli lakini swali langu, katiba ya hii mifuko inawaruhusu wao kuwakopesha waajiri wanaochangia katika hii mifuko au kuwekeza kwenye miradi ya waajiri?
Kama hayo yote yaliweza kufanyika hadi mifuko ikafilisika na hatujasikia watu kukemea au kupelekwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka au ufisadi sizani kama kutakuwa na maajabu katika hii mifuko simply because Dada Irene kapangiwa majukumu mengine.