Fisherscom
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 1,763
- 766
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mbuzi wa kafara huyo.
mission imefeli,nani aangushiwe jumba bovu!!!!!Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.
Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
Irene Charles Isaka, Director General, Social Security Regulatory Authority - JamiiForums
Una uahkika aliwahi kumshauri Magu au ni Jenesta alimshauri Magu?Baada ya kikao Rais alibaini kuwa walio kuwa wanamshauri akiwemo huyu Irene kuhusu Kikokotoo walikuwa wanampotosha sasa alipata ukweli kutoka kwa wahusika ndio maana aliamua kumtengua maana alipata ukweli halisi
jamaa anatengeneza tatzo alaf analitatua. mbona jenista muhagama kabaki? jiwe hana akili na fisiem wenzakeMagufuli huwa hapendi ujinga na watu kufanya kazi kwa mazoea. kauli ya hapa kazi tu inaendelea kuwa wazi na lazima ieleweke Magufuli anaposema hapa kazi anamaanisha nini anasema.
Unatamani umpe kikokotoo?Masikini Irene isaka dah napenda yule Dada kwakweli aje nimliwaze
Sent using Jamii Forums mobile app
Safi kabisa Mkuu kwa kusikiliza vzr..hii ndio sababu ya Irene kutolewa, na nyingine wakati tu Rais anaanza hotuba yake, aliponda utetezi wa SSRA kwa kikokotoo kipya..alisema maelezo ya Irene ni too academic, maana yake kiuhalisia hayawezekani, kama ni hivyo Irene hatoshi kwenye hiyo nafasi!! sasa watu hawasikilizi wanaleta sababu zao!Mawazo yangu yapo tofauti kidogo na wengi, wengi tunaangalia pale tulipodondokea na siyo pale tulipojikwaa. Nazani wote tulimsikia Raisi akisema mifuko haina pesa na ndio maana mamlaka husika(SSRA) ikaja na aina mpya ya kikokotoo ili kuokoa jahazi.
Swali la msingi la kujiuliza, Ilikuwakuwaje mpaka mifuko ikafilisika? Raisi aligusia kidogo kwamba kufilisika huko kulitokana na uwekezaji usio na tija mfano mradi wa Dege Eco village huko kigamboni.
Nilimsikia mhusika mmoja akisema mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa na kiasi cha trillioni 13 na hivi sasa wamebakia na trillioni 1 point something pekee, kwa kifupi trillioni 12 either zimewekezwa kwenye miradi ambayo haifanyi vizuri au kiasi kikubwa cha hizo fedha zimepigwa.
Hivi inakuingia akilini kweli trillioni 12 ziwekezwe kwenye miradi isiyofanya vizuri au zipigwe ilihali mamlaka zinazosimamia hii mifuko zipo(SSRA), waziri mwenye dhamana yupo, TAKUKURU IPO, CAG yupo, sasa kwa nini imechukua muda mrefu sana mamlaka zote hizi kugundua kwamba haina ya uwekezaji iliyokuwa inafanywa na hii mifuko haina tija?
Kumbuka kwamba hii mifuko inaendeshwa kwa kanuni na sheria, kwa hiyo sizani kama watendaji wa hii mifuko wanaweza kujiamulia tu kuchukua bilioni kadhaa na kuwekeza kwenye miradi kama wa Dege bila kuhusisha mamlaka husika zinazosimamia hii mifuko, na vile vile ndani ya hii mifuko kuna mavaluer na mauditors wakutathimini hii miradi na pia kutoa annual balance sheet kwa mamlaka husika inayoonyesha financial soundness of the fund, inakuwaje sasa hawa wote walishindwa kubaini hayo yote mpaka tunafikia huku?
Wengine wanasema hii mifuko ilikuwa sehemu ya serikali kujichotea pesa, binafsi sijui kama hilo Lina ukweli lakini swali langu, katiba ya hii mifuko inawaruhusu wao kuwakopesha waajiri wanaochangia katika hii mifuko au kuwekeza kwenye miradi ya waajiri?
Kama hayo yote yaliweza kufanyika hadi mifuko ikafilisika na hatujasikia watu kukemea au kupelekwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka au ufisadi sizani kama kutakuwa na maajabu katika hii mifuko simply because Dada Irene kapangiwa majukumu mengine.
Hivi huu ujinga wa mbeleko utaisha lini? Kwani hilo sakata c limeanzia bungeni? Irene alikuwepo uko ? Waziri c ndio alishikilia Bango mambo ya mafao calculation yasiwekwe kwenye sheria mama ili akayachakachue kwenye kanuni?Kilicho mnusuru waziri yeye si mtaalamu wa masuala ya Mahesabu hebu kapitie CV za Irene halafu katizame CV za Jenister baadaye akili yako itakufahamisha kwanini Irene alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa mifuko ya hifadhi, alafu utafahamu alishindwaje kurekebisha mahesabu, pia utajiuliza kwanini alikuwa msemaji na mtetezi mkuu ktk kuitetea hiyo 25% ilikuwa ni kwa manufaa ya nani?
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu dada alikuwa anajichanganya sana alivyokuwa anatetea asilimia 25 as if yeye hatastaafu.
Safi kabisa Mkuu kwa kusikiliza vzr..hii ndio sababu ya Irene kutolewa, na nyingine wakati tu Rais anaanza hotuba yake, aliponda utetezi wa SSRA kwa kikokotoo kipya..alisema maelezo ya Irene ni too academic, maana yake kiuhalisia hayawezekani, kama ni hivyo Irene hatoshi kwenye hiyo nafasi!! sasa watu hawasikilizi wanaleta sababu zao!
Swali zuri.Nieleweshe kosa la Irene Kisaka ni lipi?
Kwa mfano, serikali walipochota Tsh trilion 8.34 za wastaafu, walimwelekeza atoe hizo hela haraka na kama angekataa angefutwa kazi au hata kuzuliwa kesi au kupotezwa na watu wasiojulikana. Kwa hiyo Irene ametolewa kafara ili kuinusuru serikali iliyoifilisi hiyo mifuko.Angezuia vipi? Unajua directives za hayo yote zinatoka wapi? Na yeye kazi yake ni kutekeleza yale aliyoagizwa na si vinginevyo.