Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

wavuane uongozi sijui nini, mm nataka waniruhusu pesa yangu wanipe kabla sijafikisha miaka 65. Hawa mbuzi sana
 
Hii ni kawaida tuu, tengeneza tatizo, acha watu walalamike, halafu leta jibu linaloendana na malalamiko ya watu wengi na ikiwezekana tafuta mtu wa kutoa kafara...... Kwa jinsi hii umaarufu wako utaongezeka!
Ova.
 
watu wanamkejeli sana huyu mama wa watu....lakini amini hakuna kitu kigumu kama mtu mwingine kua na influence kwenye decisions zako
 
mbuzi wa kafara huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.

Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums

Irene Charles Isaka, Director General, Social Security Regulatory Authority - JamiiForums
mission imefeli,nani aangushiwe jumba bovu!!!!!
 
Baada ya kikao Rais alibaini kuwa walio kuwa wanamshauri akiwemo huyu Irene kuhusu Kikokotoo walikuwa wanampotosha sasa alipata ukweli kutoka kwa wahusika ndio maana aliamua kumtengua maana alipata ukweli halisi
Una uahkika aliwahi kumshauri Magu au ni Jenesta alimshauri Magu?
 
Magufuli huwa hapendi ujinga na watu kufanya kazi kwa mazoea. kauli ya hapa kazi tu inaendelea kuwa wazi na lazima ieleweke Magufuli anaposema hapa kazi anamaanisha nini anasema.
jamaa anatengeneza tatzo alaf analitatua. mbona jenista muhagama kabaki? jiwe hana akili na fisiem wenzake
 
Mawazo yangu yapo tofauti kidogo na wengi, wengi tunaangalia pale tulipodondokea na siyo pale tulipojikwaa. Nazani wote tulimsikia Raisi akisema mifuko haina pesa na ndio maana mamlaka husika(SSRA) ikaja na aina mpya ya kikokotoo ili kuokoa jahazi.

Swali la msingi la kujiuliza, Ilikuwakuwaje mpaka mifuko ikafilisika? Raisi aligusia kidogo kwamba kufilisika huko kulitokana na uwekezaji usio na tija mfano mradi wa Dege Eco village huko kigamboni.
Nilimsikia mhusika mmoja akisema mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa na kiasi cha trillioni 13 na hivi sasa wamebakia na trillioni 1 point something pekee, kwa kifupi trillioni 12 either zimewekezwa kwenye miradi ambayo haifanyi vizuri au kiasi kikubwa cha hizo fedha zimepigwa.
Hivi inakuingia akilini kweli trillioni 12 ziwekezwe kwenye miradi isiyofanya vizuri au zipigwe ilihali mamlaka zinazosimamia hii mifuko zipo(SSRA), waziri mwenye dhamana yupo, TAKUKURU IPO, CAG yupo, sasa kwa nini imechukua muda mrefu sana mamlaka zote hizi kugundua kwamba haina ya uwekezaji iliyokuwa inafanywa na hii mifuko haina tija?
Kumbuka kwamba hii mifuko inaendeshwa kwa kanuni na sheria, kwa hiyo sizani kama watendaji wa hii mifuko wanaweza kujiamulia tu kuchukua bilioni kadhaa na kuwekeza kwenye miradi kama wa Dege bila kuhusisha mamlaka husika zinazosimamia hii mifuko, na vile vile ndani ya hii mifuko kuna mavaluer na mauditors wakutathimini hii miradi na pia kutoa annual balance sheet kwa mamlaka husika inayoonyesha financial soundness of the fund, inakuwaje sasa hawa wote walishindwa kubaini hayo yote mpaka tunafikia huku?
Wengine wanasema hii mifuko ilikuwa sehemu ya serikali kujichotea pesa, binafsi sijui kama hilo Lina ukweli lakini swali langu, katiba ya hii mifuko inawaruhusu wao kuwakopesha waajiri wanaochangia katika hii mifuko au kuwekeza kwenye miradi ya waajiri?

Kama hayo yote yaliweza kufanyika hadi mifuko ikafilisika na hatujasikia watu kukemea au kupelekwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka au ufisadi sizani kama kutakuwa na maajabu katika hii mifuko simply because Dada Irene kapangiwa majukumu mengine.
 
Safi kabisa Mkuu kwa kusikiliza vzr..hii ndio sababu ya Irene kutolewa, na nyingine wakati tu Rais anaanza hotuba yake, aliponda utetezi wa SSRA kwa kikokotoo kipya..alisema maelezo ya Irene ni too academic, maana yake kiuhalisia hayawezekani, kama ni hivyo Irene hatoshi kwenye hiyo nafasi!! sasa watu hawasikilizi wanaleta sababu zao!
 
Kilicho mnusuru waziri yeye si mtaalamu wa masuala ya Mahesabu hebu kapitie CV za Irene halafu katizame CV za Jenister baadaye akili yako itakufahamisha kwanini Irene alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa mifuko ya hifadhi, alafu utafahamu alishindwaje kurekebisha mahesabu, pia utajiuliza kwanini alikuwa msemaji na mtetezi mkuu ktk kuitetea hiyo 25% ilikuwa ni kwa manufaa ya nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi huu ujinga wa mbeleko utaisha lini? Kwani hilo sakata c limeanzia bungeni? Irene alikuwepo uko ? Waziri c ndio alishikilia Bango mambo ya mafao calculation yasiwekwe kwenye sheria mama ili akayachakachue kwenye kanuni?
 
Huyu dada alikuwa anajichanganya sana alivyokuwa anatetea asilimia 25 as if yeye hatastaafu.

Mwache atumbuliwe tu huyu dada alijifanya anajua sana hata alifikia pahala hataki tena kushauriwa.kiburi kiliongezeka hivyo tu akae pending kwanza ili akili zimsogee sababu bado zilikuwa mbali hata kusoma alama za nyakati alishindwa.Hajui kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu?
 
Safi kabisa Mkuu kwa kusikiliza vzr..hii ndio sababu ya Irene kutolewa, na nyingine wakati tu Rais anaanza hotuba yake, aliponda utetezi wa SSRA kwa kikokotoo kipya..alisema maelezo ya Irene ni too academic, maana yake kiuhalisia hayawezekani, kama ni hivyo Irene hatoshi kwenye hiyo nafasi!! sasa watu hawasikilizi wanaleta sababu zao!

Rais yuko sahihi kabisa hawa maacademician warudi darasani kufundisha sababu mambo wanayotufikirisha hayapo kabisa katika real life so she has to go no way out.
 
Angezuia vipi? Unajua directives za hayo yote zinatoka wapi? Na yeye kazi yake ni kutekeleza yale aliyoagizwa na si vinginevyo.
Kwa mfano, serikali walipochota Tsh trilion 8.34 za wastaafu, walimwelekeza atoe hizo hela haraka na kama angekataa angefutwa kazi au hata kuzuliwa kesi au kupotezwa na watu wasiojulikana. Kwa hiyo Irene ametolewa kafara ili kuinusuru serikali iliyoifilisi hiyo mifuko.
 
Back
Top Bottom