Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Kwanini asingejiondoa kwenye hiyo nafasi ya ukurugenzi, kuendelea kuwepo hapo ina mana alikubaliana na mambo aliyoletewa kuyasimamia kuhusu mafao ya watumishi.
Kwani yupo pale kupingana na Waziri? Yeye ni mtekelezaji wa maagizo toka serikalini na kikawaida ni jambo lilikubaliwa kwa maslahi ya wanasiasa na siyo wastaafu.
 
PHD ya mkorogo, huwezi kuwa na ujasiri wa kutetea ushetani kama ule, hata kama ulikuwa unatumwa na wanasiasa duh! Ona walivyokuruka utabaki na aibu yako mama!.waliokuwa wanakutuma Jiwe na Jennister(Double J) wanaendelea kupeta tena watakuwa wanakuponda kweli na PHD yako ya mkorogo, unaweka njaa mbele kuliko maslahi ya wengi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu dada angekuwa ni mtu anayejielewa angeachia tu ile nafasi ya ukurugenzi lakini akawa kiherehere kwa kutetea ujinga
 
Mimi siko kwenye hizo complication zenu za kichadema! kudandia kila kinachopita mbele yenu. Ona wenzako mpaka sasa hawaoni kuwa wanatetea suala la fastjet na wanasema bila haya waruhusiwe kurusha ndege na suala la usalama lifumbiwe macho!

Umevurugwa ww, naona unazuia risasi kwa debe. Ushapotea kwenye game. Kajikite kwenye mada moja ili usionekane unarukia kila kinachopita mbele yako. Huku mitandaoni kunajadiliwa chochote, kwani ni utashi wa kila mtu. Huku ni kama ukumbi wa disco, unacheza mziki wowote unaokufurahisha. Kama unataka kuspecialize nenda kwenye wizara huko kila wizara imejikita kwenye eneo moja tu.
 
Hilo haliwezi kufanyika. Viongozi wengi hawatetei ukweli, wapo kwa ajili ya maslahi yao kwanza yakigushwa ndio wanapiga kelele lakini kwa raia wa kawaida wanaufyata mkia kama jibwa koko. Watu wa namna hiyo hawafai kabisa kuwa viongozi. Hawa ndio wanafanya watu wenye akili na upeo mkubwa waishi maisha magumu na kuonekana wasaliti
Aliekua mkurugenzi wa Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii ametenguliwa cheo chake baada ya sakata la Pension.
Ushauri:Rais tusaidie wabunge wote wa CCM ambao hawakuwatetea wananchi kuhusu mafao wasirudi bungeni tena 2020. Maana kila ujinga wao ni kusupport

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu dada atakuwa ametumbuliwa kwa kushindwa kufanikisha jaribio la kuwaibia wafanyakazi kwa kuwa yeye ni mjumbe tu wakupeleka kile kilichoandaliwa na kupitishwa na wengine.

Kwani haiingii akili muswada upelekwe bungeni na kupitishwa, ubarikiwe kwa kusainiwa na mtumbuaji,halafu ajekutumbuliwa mpiga debe ambaye alikabidhiwa kuupigia debe kwa watumishi wa umma.
 
Kwani yupo pale kupingana na Waziri? Yeye ni mtekelezaji wa maagizo toka serikalini na kikawaida ni jambo lilikubaliwa kwa maslahi ya wanasiasa na siyo wastaafu.
Kiongozi usitetee upuuzi wa yule dada, kwa hilo sikubaliani na wewe, it is better to resign a job kuliko kuendelea kutekeleza ujinga wa wajinga nadhani elimu zetu bado hazijatukombowa na haziwezi kutukomboa. unamkumbuka Mafuru aliyekuwa msajili wa Hazina mbona alipingana na jiwe wazi wazi issue ya fixed account yeye huyo dada alishindwa nini?
 
Mfano unamhusu mkurugenzi. Najua masikio yako yanapenda kuambiwa kuwa rais ni mtu mbaya. Hili halishangazi! Ila kama rais angeingilia wakati wabunge wanapitisha wewe ungekuwa wa kwanza kusema analiendesha bunge kwa rimoti. Kwangu mimi rais amefanya vizuri sana kwani ameacha maji yafuate mkondo wake ili wengi tujue ni wapi kwenye ubovu na wapi kwenye ubora. Kwa hali hii wabunge waliopitisha hiyo sheria keshokutwa watatafakari kabla ya kupitisha mambo mengine.
This is polishing a turd the likes of which I haven't seen before. Load of bollocks.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana hata maprof huonekana kama std 7! Tengua tengua kama hii hakuna mtaalamu atakayesubutu!
 
Umevurugwa ww, naona unazuia risasi kwa debe. Ushapotea kwenye game. Kajikite kwenye mada moja ili usionekane unarukia kila kinachopita mbele yako. Huku mitandaoni kunajadiliwa chochote, kwani ni utashi wa kila mtu. Huku ni kama ukumbi wa disco, unacheza mziki wowote unaokufurahisha. Kama unataka kuspecialize nenda kwenye wizara huko kila wizara imejikita kwenye eneo moja tu.
Tunajadili chochote ni sawa lakini kwa hoja, tena tukitumia akili na siyo kwa kufuata mkondo kama nyumbu! Wewe kila kitu unafuata mkondo bila kuwa na hoja za msingi. Kwako wewe mwenye akili ni yule anayesema Magufuli ni mbaya. Sasa kama kusema ukweli ni kuvugwa basi acha nivurugwe lakini jua hii ni awamu nyingine siyo ile uliyokuwa umezoea!
 
"Hapa ndipo huwa namkubali Mkuu. Wajinga wajinga kama hawa ni kufyekelea mbali"
 
Kiongozi usitetee upuuzi wa yule dada, kwa hilo sikubaliani na wewe.
Mimi sitetei alichokifanya, bali sikubaliana kuhusu kubebeshwa lawama za kikokotoo cha mafao. Yeye kazi yake ni kupendekeza kwa waziri na kama waziri akikataa basi hapo ndipo tungepima ni kwa nini hakujiuzulu.

Wanasiasa ndiyo hupeleka mawazo yao kwa wataalamu na wataalamu hutengeneza mambo kutokana na mahitaji ya wanasiasa. Ukiwa mjamaa utatengenezewa jambo la kijamaa na ukiwa bepari utatengenezewa jambo la kibepari hata kama mtaalamu ni yule yule mmoja!!
 
Back
Top Bottom